Ukeketaji dhidi ya wanawake na mabinti

Mema Tanzania

Member
Feb 23, 2020
66
65
Kila mwaka ifikapo tarehe 6, Februari dunia huadhimisha siku ya kimataifa ya kupinga ukeketaji.

Je, unatambua wanawake na mabinti takribani milioni 7.9 wamepitia ukeketaji Tanzania?

FGM.png


Licha ya serikali na wadau mbalimbali kupambana vilivyo na ukeketaji, kuna maeneo bado ukeketaji dhidi ya wanawake na wasichana umeendelea kufanyika kwa kiwango cha juu hasa mikoa ya Manyara, Dodoma na Arusha imeendelea kuongoza.

FGM1.png


Ukeketaji ni moja ya ukatili mkubwa wa kijinsia na waathirika wamekumbwa na kadhia kadhaa ikiwemo maambukizi ya virusi vya UKIMWI, kuathirika kisaikolojia kupoteza damu nyingi na kupelekea kifo kwa baadhi yao.

FGM2.png


Kila mmoja wetu anayo nafasi ya kumaliza ukatili wa kijinsia kwa kupaza sauti, kutoa elimu hasa kwa maeneo yenye kiwango kikubwa na kutoa taarifa pindi uonapo vitendo/ viashiria vya kufanyika ukeketaji.

FGM BARS.png

-
🔗 BMC Public Health 2015 & TDHS-MS 2015/16
#SayNoToFGM #ZuiaUkatili
 
Back
Top Bottom