UKAWA wamsusia Magufuli

UKAWA wamsusia Magufuli

Dar es Salaam. Vyama vya upinzani vimesusia hafla iliyoandaliwa Ikulu kwa ajili ya Rais Paul Kagame wa Rwanda.

Rais John Magufuli alikuwa ameandaa dhifa ya kitaifa kwa ajili ya mgeni huyo ambaye aliwasili nchini juzi kwa ziara ya siku mbili, iliyohusisha kufungua Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara jijini Dar es Salaam.

Baada ya kuzindua maonyesho hayo, Rais Kagame aliandaliwa hafla hiyo ambayo ingeweza kumkutanisha na viongozi wengine wa kisiasa na wafanyabiashara, lakini hali ikawa tofauti baada ya viongozi wa vyama vya upinzani vinavyounda Ukawa kutoshudhuria.

“Kuna mgogoro huo wa kuzuia mikutano ya hadhara, lakini hawajali. Suala la Zanzibar, watu wanakufa lakini hawajali, bungeni kuna mpasuko kwa muda wote lakini hawajali,” amesema Mwenyekiti wa Chadema, Freeman

Mbowe, ambaye ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na mbunge wa Hai akizungumzia uamuzi wao wa kugoma.
kwani kujali ndio serikali ifuate jinsi chadema inataka kwa hoja dhaifu za upinzani? cdm sio chama tawala hivyo wajifunze kutambua nafasi yao sio kudhani wataongoza nchi huku serikali kwa kila hali imeonyesha kufanya kile wananchi wanataka.
 
Dr. Tulizo akihudhuria haitoshi mpaka sie?
 
Please muwe na ADABU... neno DICTATOR lisitumike kumchafua Rais wetu Magufuli..!! Mh. Rais hajawahi na sio DICTATOR..!!

Hii ndio jina kweli la kumuita Rais wetu aliyechaguliwa kwa kura za wananchi..? Inaudhi sana...

Hivi mnajua DICTATOR yukoje..? ✘✘ Lissu kaniudhi sana kwa kweli...

Mh. Rais Magufuli kapatikana kwa njia ya demokrasia, kwa kupigiwa kura, na yeye ndio Rais halali kwa mujibu wa Katiba yetu, kaunda SERIKALI halali, na anawatumikia WANANCHI WOTE bila kujali vyama, dini, rangi, kabila au wanaompinga hadharani majimbo yao yamepewa budget inayostahili...!!

KUZUIWA kwa MIKUTANO YA HADHARA ndio UKAWA kweli muuanze fujo, dharau, vurugu, kumtukana Rais ni DICTATOR, kisa kuzuiwa kwa mikutano ya HADHARA..?

Kampeni zilishaisha, period, aliyepata kuchaguliwa kapewa kijiti, aliyekosa ajipange baada ya miaka 5 kaombe kura... sasa ni wakati wa KUPIGA KAZI... kutimiza ahadi za wananchi... ila sio sasa hv kuanza KAMPENI na mikutano ya HADHARA, maendeleo yatafanyika saa ngapi.?

Mh. Rais Magufuli, piga kazi... wakisusa wewe ongeza speed, matokeo yataonekana SOON, na WANANCHI WATAONA... usife moyo... twende tuko nyuma yako...!!

Kazi kutafuta fujo tu.....!!
Hata hivyo jay one mbona mi naona huyo lissu hata hatambui alichosema anamaanisha nini maana unapompa mtu sifa ya uchwara it meanz anajifanya na sio halisi
 
UKAWA wanatakiwa wafikirie matokeo ya maamuzi wanayofanya na waachane kufanya mambo kwa mazoea. Mgomo waliounza bungeni sasa hivi unawamaliza. Kwa haraka haraka mtu anaweza kudhani wamegoma kuhudhuria hafla Ikulu lakini ukweli walijua kama wangeenda kwenye mnuso wakati wametoka bungeni ingeleta picha mbaya. Kwa maneno rahisi, kususa bunge kunaanza kuathiri nafasi ya UKAWA kuhudhuria mambo mengine ya kitaifa.

Sasa huko tuendako watamalizaje huo usanii wa kususa?
Unajua ukweli lakini mahaba yanakufanya upotoshe. Ukawa wamemgomea NS. Serikali ilitakiwa kuingilia kati kumaliza tofauti hiyo lakini kwa makusudi wamekaa kimya na siku zote tuna wasikia viongozi wa ukawa wakisema kuna mpasuko unahitaji wajadili lakini ccm hawapo tayari kumaliza suala hilo kitu kinacho niaminisha nikweli NS anatumba kukandamiza wabunge wa upinzani bungeni.
 
Please muwe na ADABU... neno DICTATOR lisitumike kumchafua Rais wetu Magufuli..!! Mh. Rais hajawahi na sio DICTATOR..!!❌❌❌❌

Hii ndio jina kweli la kumuita Rais wetu aliyechaguliwa kwa kura za wananchi..? Inaudhi sana...❌❌❌❌

Hivi mnajua DICTATOR yukoje..? ✂✂✘✘ Lissu kaniudhi sana kwa kweli...

Mh. Rais Magufuli kapatikana kwa njia ya demokrasia, kwa kupigiwa kura, na yeye ndio Rais halali kwa mujibu wa Katiba yetu, kaunda SERIKALI halali, na anawatumikia WANANCHI WOTE bila kujali vyama, dini, rangi, kabila au wanaompinga hadharani majimbo yao yamepewa budget inayostahili...!!

KUZUIWA kwa MIKUTANO YA HADHARA ndio UKAWA kweli muuanze fujo, dharau, vurugu, kumtukana Rais ni DICTATOR, kisa kuzuiwa kwa mikutano ya HADHARA..?

Kampeni zilishaisha, period, aliyepata kuchaguliwa kapewa kijiti, aliyekosa ajipange baada ya miaka 5 kaombe kura... sasa ni wakati wa KUPIGA KAZI... kutimiza ahadi za wananchi... ila sio sasa hv kuanza KAMPENI na mikutano ya HADHARA, maendeleo yatafanyika saa ngapi.?

Mh. Rais Magufuli, piga kazi... wakisusa wewe ongeza speed, matokeo yataonekana SOON, na WANANCHI WATAONA... usife moyo... twende tuko nyuma yako...!!

Kazi kutafuta fujo tu.....!!
Aliyesema raisi dictator ni nani?? Mbona mnajishtukia
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Aliyesema raisi dictator ni nani?? Mbona mnajishtukia

Tundu Mughway Lissu...!!❌❌❌

Hivi Mh. Rais Magufuli angekuwa DICTATOR, hata Lissu angefikishwa MAHAKAMANI KWELI..? Angepata hata podium ya kurudia rudia kusema Rais ni DICTATOR UCHWARA..? Si angempoteza tu wala asingejulikana yuko wapi..
Jamani, lazima Rais aheshimike... sio OMBI ni lazima.. Rais SIO MWENZAKO... Lazima tumheshimu na adabu tele iwepo..!! Haiwezekani mtu kama Lissu, pamoja na UHAMAHIRI WAKE KTK SHERIA, but he has to RESPECT and DISPLINE himself hata kabla ya Dola kuingilia, kuwa Rais sio wa KUDHARAULIWA TU HOVYO HOVYO... hili halikubaliki..!! hapana tuseme..!!❌❌❌❌ Heshima ni lazima, kwa Rais... hapana, sio kumtukana hovyo hovyo.. hapana hapana..!!

Inauma..!! Mh. Rais lazima aheshimiwe.. lazima..!!✔✔✔
 
UKAWA wanatakiwa wafikirie matokeo ya maamuzi wanayofanya na waachane kufanya mambo kwa mazoea. Mgomo waliounza bungeni sasa hivi unawamaliza. Kwa haraka haraka mtu anaweza kudhani wamegoma kuhudhuria hafla Ikulu lakini ukweli walijua kama wangeenda kwenye mnuso wakati wametoka bungeni ingeleta picha mbaya. Kwa maneno rahisi, kususa bunge kunaanza kuathiri nafasi ya UKAWA kuhudhuria mambo mengine ya kitaifa.

Sasa huko tuendako watamalizaje huo usanii wa kususa?
Kiungo gani umetumia kufikiri hiki ulichoandika
 
kumbe mlio choka kufikiri mpo wengi! endelea kujipendekeza akupe ukuu wa kijiji.
 
Hili neno "DICTATOR" lafaa kupigwa marufuku hapa jukwaani. Hatuwezi kuendelea kumdhihaki rais kiasi hiki.
Acha mambo ya ajabu ww!! Kwahiyo Magufuli ni dikteta wa kwanza hapa Duniani?
Au yy ndie muanzilishi wa hili neno?
 
Nini maana ya dikteta? Nielewesheni

Maana yake ni mtu ambaye anawasomea wanafunzi maandishi halafu wao wanayaandika kwenye karatasi zao za kujibia maswali ya mtihani. Kwani we mkuu hujawahi kufanya mtihani wa namna hii wakati ukiwa shule ya msingi au sekondari hapa TZ? Neno dictator limetokana na neno Dictation. Na hiyo dictation ndiyo kuwasomea wanafunzi maandishi fulani halafu wao wanayaandika lengo lake likiwa ni huyo dictator kutaka kujua kama wanafunzi husika wanaijua vizuri lugha yenye maneno hayo.
 
Dar es Salaam. Vyama vya upinzani vimesusia hafla iliyoandaliwa Ikulu kwa ajili ya Rais Paul Kagame wa Rwanda.

Rais John Magufuli alikuwa ameandaa dhifa ya kitaifa kwa ajili ya mgeni huyo ambaye aliwasili nchini juzi kwa ziara ya siku mbili, iliyohusisha kufungua Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara jijini Dar es Salaam.

Baada ya kuzindua maonyesho hayo, Rais Kagame aliandaliwa hafla hiyo ambayo ingeweza kumkutanisha na viongozi wengine wa kisiasa na wafanyabiashara, lakini hali ikawa tofauti baada ya viongozi wa vyama vya upinzani vinavyounda Ukawa kutoshudhuria.

“Kuna mgogoro huo wa kuzuia mikutano ya hadhara, lakini hawajali. Suala la Zanzibar, watu wanakufa lakini hawajali, bungeni kuna mpasuko kwa muda wote lakini hawajali,” amesema Mwenyekiti wa Chadema, Freeman

Mbowe, ambaye ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na mbunge wa Hai akizungumzia uamuzi wao wa kugoma.
We Vipi....nani anawahitaji UKAWA! hawana mchango wowote kwa ajili ya maslahi mapana ya nchi hii! wataendelea kusota vijiweni!
 
UKAWA wanatakiwa wafikirie matokeo ya maamuzi wanayofanya na waachane kufanya mambo kwa mazoea. Mgomo waliounza bungeni sasa hivi unawamaliza. Kwa haraka haraka mtu anaweza kudhani wamegoma kuhudhuria hafla Ikulu lakini ukweli walijua kama wangeenda kwenye mnuso wakati wametoka bungeni ingeleta picha mbaya. Kwa maneno rahisi, kususa bunge kunaanza kuathiri nafasi ya UKAWA kuhudhuria mambo mengine ya kitaifa.

Sasa huko tuendako watamalizaje huo usanii wa kususa?

Unawamaliza kivipi Mkuu?
 
"Mualiko ni hiyari kuja au kutokuja na wao waliitwa kula tu hakuna kingine. Wengi waliitikia wito na wengi hawakuitikia na hakuna kilichoharibika kwa kuwa Hakuna chakula kilichobaki kiasi cha kuona pengo lao"- Mtu mmoja Mashuhuri namhifadhi jina
 
Back
Top Bottom