UKAWA wamsusia Magufuli

UKAWA wamsusia Magufuli

Hivi kwanini JPM hajiulizi ilikuwaje KJ akawa na urafiki wa mashaka na Kagame??
Nijuavyo mimi JK alikuwa anasaidia kuwaondoa waasi DRC na bwana Kagame hataki waondoke kuna tetesi kwamba Kagame anawasaidia.
Sasa tujiulize JPM anamuunga Kagame mkono kama kweli anawasaidia waasi?
Kagame ameona uhodari wa jeshi la Tanzania lililopo DRC anataka kumuingia jamaa yetu ili awaondoe makamanda wetu huko Kongo kwa manufaa yake.
Nashauri JPM awe makini na huo undugu wake na KAGAME
Halafu hata mimi swala hili linanitatiza kweli: eti Ukawa walikuwa wanataka raisi mkali na mwenye kuchukia hatua za kijasili. Leo amepatikana wanaaza kuogopa ogopa!! Kana kwamba wao ndiyo wanachukua hatua hizo za kijasili. Eti bora angekuwa yule yule ..huu ni unafiki uliokidhiri!!
 
Dar es Salaam. Vyama vya upinzani vimesusia hafla iliyoandaliwa Ikulu kwa ajili ya Rais Paul Kagame wa Rwanda.

Rais John Magufuli alikuwa ameandaa dhifa ya kitaifa kwa ajili ya mgeni huyo ambaye aliwasili nchini juzi kwa ziara ya siku mbili, iliyohusisha kufungua Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara jijini Dar es Salaam.

Baada ya kuzindua maonyesho hayo, Rais Kagame aliandaliwa hafla hiyo ambayo ingeweza kumkutanisha na viongozi wengine wa kisiasa na wafanyabiashara, lakini hali ikawa tofauti baada ya viongozi wa vyama vya upinzani vinavyounda Ukawa kutoshudhuria.

“Kuna mgogoro huo wa kuzuia mikutano ya hadhara, lakini hawajali. Suala la Zanzibar, watu wanakufa lakini hawajali, bungeni kuna mpasuko kwa muda wote lakini hawajali,” amesema Mwenyekiti wa Chadema, Freeman

Mbowe, ambaye ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na mbunge wa Hai akizungumzia uamuzi wao wa kugoma.
Mbowe anajishaua tu, nani aliwaalika? Mnapenda kudeka deka tu. Nani anamuitaji mwingine kati ya Magu na nyie?
 
Chadema mnaenda kua chanzo cha mashoga wengi zaidi dar, huku kususa susa ni moja ya symptoms za umama mama, na sio vyema kufundisha bavicha hivyo
I see!!....

1467540352095.jpg
 
Mheshimiwa Rais hawezi kupoteza muda kushughulikia mambo ya kuhuni yanayofanywa na vyama Fulani! Kumbukeni anayo Mamlaka ya kushughulikia wahuni wote wanaomkashifu hapa jamvini maana tunawajua!!
 
Slaa ndiyo alikuwa anajua kuendesha kile chama, sasa hivi hali ni tete.. mawazo ya kinyumbu ndiyo yametawala!!
 
Mimi Ningeshauri hawa wakuu wa siasa wadumishe upendo kwani chuki ikienea hata wtt wao hawatasalimika,
 
Toeni na waraka wa kukosa mwaliko kama yule meya wa kinondoni
 
Mheshimiwa Rais hawezi kupoteza muda kushughulikia mambo ya kuhuni yanayofanywa na vyama Fulani! Kumbukeni anayo Mamlaka ya kushughulikia wahuni wote wanaomkashifu hapa jamvini maana tunawajua!!
Haya ndio mawazo ya kidikteta, Rais hana mamlaka unayodhani anayo.

Tuna mihimili mitatu, Bunge, serikali na mahakama, ni hasara kwa Taifa kuwa vijana wenye upeo finyu na dhaifu kama wewe. Hopeless kabisa.
 
Dar es Salaam. Vyama vya upinzani vimesusia hafla iliyoandaliwa Ikulu kwa ajili ya Rais Paul Kagame wa Rwanda.

Rais John Magufuli alikuwa ameandaa dhifa ya kitaifa kwa ajili ya mgeni huyo ambaye aliwasili nchini juzi kwa ziara ya siku mbili, iliyohusisha kufungua Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara jijini Dar es Salaam.

Baada ya kuzindua maonyesho hayo, Rais Kagame aliandaliwa hafla hiyo ambayo ingeweza kumkutanisha na viongozi wengine wa kisiasa na wafanyabiashara, lakini hali ikawa tofauti baada ya viongozi wa vyama vya upinzani vinavyounda Ukawa kutoshudhuria.

“Kuna mgogoro huo wa kuzuia mikutano ya hadhara, lakini hawajali. Suala la Zanzibar, watu wanakufa lakini hawajali, bungeni kuna mpasuko kwa muda wote lakini hawajali,” amesema Mwenyekiti wa Chadema, Freeman

Mbowe, ambaye ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na mbunge wa Hai akizungumzia uamuzi wao wa kugoma.

Wao walale na kuamka asubuhi na maigizo alafu wayaite mgogoro kisha walazimishe kila mtu aseme na kuamini ni mgogoro.....! Nani Ana muda wa kuendekeza siasa za kitoto namna hiyo...
 
Haya ndio mawazo ya kidikteta, Rais hana mamlaka unayodhani anayo.

Tuna mihimili mitatu, Bunge, serikali na mahakama, ni hasara kwa Taifa kuwa vijana wenye upeo finyu na dhaifu kama wewe. Hopeless kabisa.

Hivi Nani mwenye mamlaka ya kuvunja Bunge?!
 
Kwani huo mwaliko haukuwa wa kisiasa? Bahati yao wangeenda tuu wangeambiwa wamefuata ubwabwa hivyo mkusanyiko wao ni haramu.
 
Back
Top Bottom