Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Dar es Salaam. Vyama vya upinzani vimesusia hafla iliyoandaliwa Ikulu kwa ajili ya Rais Paul Kagame wa Rwanda.
Rais John Magufuli alikuwa ameandaa dhifa ya kitaifa kwa ajili ya mgeni huyo ambaye aliwasili nchini juzi kwa ziara ya siku mbili, iliyohusisha kufungua Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara jijini Dar es Salaam.
Baada ya kuzindua maonyesho hayo, Rais Kagame aliandaliwa hafla hiyo ambayo ingeweza kumkutanisha na viongozi wengine wa kisiasa na wafanyabiashara, lakini hali ikawa tofauti baada ya viongozi wa vyama vya upinzani vinavyounda Ukawa kutoshudhuria.
“Kuna mgogoro huo wa kuzuia mikutano ya hadhara, lakini hawajali. Suala la Zanzibar, watu wanakufa lakini hawajali, bungeni kuna mpasuko kwa muda wote lakini hawajali,” amesema Mwenyekiti wa Chadema, Freeman
Mbowe, ambaye ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na mbunge wa Hai akizungumzia uamuzi wao wa kugoma.