UKAWA wamsusia Magufuli

Haya ndio mawazo ya kidikteta, Rais hana mamlaka unayodhani anayo.

Tuna mihimili mitatu, Bunge, serikali na mahakama, ni hasara kwa Taifa kuwa vijana wenye upeo finyu na dhaifu kama wewe. Hopeless kabisa.
Wewe kama unajifanya hodari jaribu ushughulikiwe!! Badala ya kujishughulisha kwenye shughuli za maana unabwia viroba kuandika upuuzi wako!!
 
Hili neno "DICTATOR" lafaa kupigwa marufuku hapa jukwaani. Hatuwezi kuendelea kumdhihaki rais kiasi hiki.
Huyo anayedhani kuwa ni Dictator Uchwara aje mahakamani na apinge kuwa yeye sio Dictator Uchwara!
 
Huyo anayedhani kuwa ni Dictator Uchwara aje mahakamani na apinge kuwa yeye sio Dictator Uchwara!
Ulishawahi kujiuliza kwanini Zitto mbwembwe zake hazisikiki tena ndiyo utajua Magufuli ni nouuuumeeer
 
Hata mwewe hushinda angani ila kujua likizama lazima atue.
 
Mwenzako Lissu anatetewa Na Mawakili 17 Na wote wanalipwa Na Chama....

Sasa sijui wewe utasimamisha Mawakili wangapi Na huku chama hakikutambui.!
umejuaje km na mimi sio mmojawapo wa Mawakili hao 17.Acheni kutumika km mapulizo ya kiume.Ukuu wa Wilaya umeshapita unahangaika na nini sasa?.au hizo buku 2
 
Endeleeni kususa. Lakini kumbukeni siku zinazidi kwenda, Mheshimiwa rais Magufuli anaendelea kufanya mambo mazuri yanayowagusa wananchi moja kwa moja na ninyi kwa ufahamu wenu mnaendelea kufanya mambo ambayo hayawasaidii wananchi. Kumbukeni mwisho wa siku mnatakiwa kuwaeleza wananchi waliowapigia kura majimboni mwenu mlichokifanya tangu mlipochaguliwa. TAFAKARINI UPYA JUU YA MNAVYOENENDA.
 
Kiongozi wetu kuteua sio kazi, maana inaanza kuonekana akiteua au kutimua ndio kafanya kazi.
Watu kama wewe ndio mnampotosha kiongozi kwa maana anadhani yupo sahihi kwa vimaneno vyenu eti "usife moyo tupo nyuma yako"
TAIFA LINAKOSA UMOJA KWA UZEMBE UZEMBE TU.
 
The opposite is true.
 
Mtasubili sana nyie UKAWA, jueni kuwa mmepotea
Nyinyi ccm mmepotea na mbaya zaidi hamjui kuwa mmepotea kwahiyo subirini mviringishwe na chatu ndio mjitambue.
 
Reactions: BAK
Wagome mpaka 2020
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Mtakumbuka ni muda sasa sijaonekana wala kusikika katika harakati za kisiasa. Leo nimependa kuweka bayana ili umma wa watanzania ufahamu kwani kumekuwa na upotoshwaji mkubwa juu ya ukimya wangu.

Napenda umma wa watanzania ufahamu yafuatayo:-

1. Msimamo wangu wa kuitaka serikali imkamate Mh Edward Lowassa, imhoji na imchukulie hatua kwa mujibu wa sheria kutokana na ushiriki wake katika kashfa ya RICHMOND haujabadilika kama ambavyo niliwahi kusema nikiwa mkurugenzi wa vijana wa CHADEMA tar 25 Februari 2008 na kipindi chote nikiwa Mbunge wa Ubungo.

Hivyo nategemea kuanzishwa kwa mahakama ya mafisadi Lowassa ndiyo atakuwa wa kwa. Siwezi kusaliti msimamo wangu bora nipoteze ubunge wangu.

2. Sikukubaliana na utaratibu uliotumika kumpata mgombea urais ndani ya Chama changu hususani ujio wa Mh Edward Lowassa mmoja wa watu ambao ni mizizi ya ufisadi hapa nchini. Hali hii ilinilazimu nikae kimya kutokana na kutokuamini kilichokuwa kinatokea hususani kwa Chama kama CHADEMA kilichojijenga na kujipatia umaarufu kwa kuongoza mapambamo dhidi ya rushwa, ubadhirifu, ufisadi na uwajibikaji mbovu wa serikali halafu tukasaliti msimamo wetu kwa uharaka wa kuipata dola! Sikukubaliana na sijakubaliana hata sasa.

3. Napenda kuzungumzia utendaji wa serikali ya Dkt Magufuli. Naomba Ifahamike nimekuwa mara zote nikisema matatizo ya msingi ya nchi yetu hayasababishwi na mapungufu ya sheria ila Kwa kiasi kikubwa yanasababishwa na kulegea kwa misingi ya utawala wa sheria na uwajibikaji miongoni mwa viongozi. Hivyo kwa asilimia kubwa naona Dkt Magufuli ameweza kujibu nilichokuwa nikikilalamikia kwa muda sasa. Haya mengine yanazungumzika.

4. Sikubaliani pia na mtazamo wa baadhi ya viongozi wakiwemo wa Chama changu wanaotaka fedha za walipa kodi ziendelee kuteketea kwa ufisadi na ubadhirifu huku wahusika ambao ni wachache wakilindwa kwa kisingizio cha haki za binadamu. Kwa hili nampongeza Mh Rais kwa msimamo na hatua anazochukua japo apanue wigo ili watanzania maskini wanufaike na utajiri wa rasilimali walizojaliwa.

5. Vile vile naomba kuzungumzia mwenendo wetu kambi rasmi ya upinzani bungeni au UKAWA binafsi sifurahishwi na maagizo na maelekezo ya viongozi wetu juu ya kuingia na kutoka bungeni kwa hoja ambazo haziwagusi wananchi moja kwa moja kiasi cha kutufanya tushindwe kutimiza majukumu yetu kama wabunge kwa mujibu wa Ibara ya 63 (2) na (3) katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kutunga sheria, kuisimamia serikali, kuwawakilisha wananchi na kupitisha mipango ya maendeleo. Sifurahishwi sababu kutoka Kwetu hakuna la msingi tunalofanya kwa ajili ya wananchi waliotutuma huko bungeni. Tusipobadilika itatugharimu!

Mwisho nawatakia waumini wote wa kiislamu mfungo mwema wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Imetolewa leo tar 3 Julai 2016.

John Mnyika (Mb)
0754 694 553
 
Hili neno "DICTATOR" lafaa kupigwa marufuku hapa jukwaani. Hatuwezi kuendelea kumdhihaki rais kiasi hiki.
Kweli kabisa. Kama unatofautiana na Rais kwa jambo fulani zungumzia hilo jambo. Siyo kumwita "dictator". Ni sawa na kutokubaliana na mzazi wako kwa jambo fulani. Huwezi kuanza kumpandikizia vineno vya kijinga. Huyu ni Rais ambaye alichaguliwa na wengi hata kama wewe hukumchagua. Hiyo ndiyo demokrasia: wengi wape.
 
Hakuna utafiti unaoonyesha watu wakifanya mikutano hawatafanya kazi. Aidha, hakuna utafiti unaoonyesha kama watu hawatafanya mikutano watafanya kazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…