Ama kweli...hii kali sasa..
Siku ya kufa nyani miti yote huteleza...!!
Nimetumia muda wangu, tokea jana jioni, KUWAPIGIA watu 42 simu, nikiwa MIMI sijaonyesha kabisa msimamo wangu wa kisiasa, au nampendelea nani...!!! Na niweke wazi, watu hawa, ni wale ambao, SIJAWAHI ONGEA NAO mambo ya siasa, yaani sio wale ambao hata mimi najua wako chama gani...!!!
SIKUAMINI... eeeehh...!!!
Watu 38 wanasema CCM haifai kabisaaa... na watampa kura Lowassa, na kati ya hao 38, watu 9 walisema wazi
wao ni CCM, ila KURA ZAO KWA LOWASSA TU na UBUNGE watawapa UKAWA TU.... nao wameichoka CCM, nikasema kwnn msihame..? Wakasema kuhama sisi hatutangazi ktk vyombo vya habari sbb hatuna coverage, so TUSHAHAMA KIROHO NA KIMWILI TUKO UKAWA... NI CCM JINA TU...!!! NILISHANGAA SANA...
Na, hao 4 waliobakia, wawili wanasema wako CCM na watabaki CCM,
ila wana Imani na Magufuli, na wawili waliobakia wanasema, wanaona heri URAIS wampe Lowassa, ila UBUNGE hawajaamua bado...!!!
Wengine walikuwa wanatoa hadi maneno machafu sana juu ya CCM.. na kuniambia ww uko kwa LOWASSA, UKAWA au CCM... nikasema, mm ni LOWASSA TU... nikaona hasira inawapungua .. daaah..!!!
Mzee mmoja wa CCM, anasema, AMEICHUKIA CCM sana sbb KAMPENI ZAO ZOTE zinetawaliwa na MATUSI MENGI, na wamesahau kunadi sera zao, wamebakia kumtusi Lowassa kila kona, hadi anashikwa na hasira kila siku, nikamuuliza mfano ni nani..? Akasema kwani hujamsikia Mkapa, Kibajaji, Mwigulu, Nape, Makongoro, wao ni matusi tu... hawana huruma na maisha ya wananchi... mara Pumbavu nyie, malofa nyie, Oil chafu nyie, Makapi, mara MBUMBUMBU nyie.... HIZI ni fedhuli kuu za Viongozi wa CCM, wamejitenga na MAISHA ya maskini, sasa wanawatusi tena.... huyo mzee kakasirika sana daah..!!! eti kampeni za CCM, asilimia kubwa ni MATUSI, kisha MIZIKI TU, au FIESTA... anawashangaa CCM kukosa kabisa mwelekeo...!!!
Aiseee, nimeshangaaa, kweli WATU wameichoka CCM sanaa...!!!
Yaani, CCM najua hawataki KUJUA huu UKWELI...!!! Nikaunganisha na ile ya UWANJA WA TAIFA wakati wa halftime ya mechi kati ya TAIFA STARS vs NIGERIA... nikasema hii sasa ni kweli...!!!
Asanteni CCM wanaojielewa kutu support...big up kwenu..!!! UKOMBOZI ni kwa wote...!!!
LET'S VOTE... TALKING IS OVER...!!!
LET'S VOTE.... CCM kwisha kabisa..!!!
Lowassa, Ukawa, ni mpango wa Mungu....!!!
✌✌✌✌✌✌✌✌✌✌✌✌✌