UKAWA vs CCM katika urais, piga Kura hapa

UKAWA vs CCM katika urais, piga Kura hapa

UKAWA VS CCM KATIKA URAIS

  • UKAWA

    Votes: 757 85.2%
  • CCM

    Votes: 118 13.3%
  • NONE OF THE ABOVE

    Votes: 13 1.5%

  • Total voters
    888
Status
Not open for further replies.
Maendeleo ya nchi hayaendi kwa kasi inayotarajiwa, sambamba na utajiri wa nchi hii, kwa kuwa viongozi wanashiriki na kuhujumu uchumi. Kiongozi anayefaa ni yule mwenye mikakati dhahiri na tekelezeki ya kupambana na ufisadi bila woga na kwa nguvu zote. Kati ya hao ni nani? Kauli na matendo yao wakati huu wa kampeni yatawapambanua.
 

Attachments

  • 1441018196354.jpg
    1441018196354.jpg
    40.9 KB · Views: 110
Tangu juzi kaibiwa sauti, kawa mpole balaa...

Hajielewi huyu anafananisha mageuzi ya LIBYA na TANZANIA. Huo upuuzi akawaeleze wazee wa kijijini. GADAFI alitolewa madarakani kwa nguvu za WAMERAKANI kwa sababu ya maslahi yao. CCM inatolewa madarakani kwa nguvu ya umma kwa maslahi ya umma. Kwa taarifa yake tutakichoma kitanda CCM ili tukiangamize pamoja na kunguni wake wote hakuna kitanda chenye kunguni mmoja.
 
Hahahaaa
 

Attachments

  • 1441018345921.jpg
    1441018345921.jpg
    19.6 KB · Views: 165
Wanachojivunia wanasiasa wa hapa TANZANIA ni kwamba wananchi wana uwezo mdogo wa kuchanganua mambo na hawabebi historia....ndio maana leo mgombea anaweza akasema hili huku akisema ana ushahidi wa jambo na watu wakamshangilia na pia kesho tena akalikana jambo na kusema ana ushahidi na watu hao hao wakamshangilia.........
 
Magufuli anastahili hilo halina ubishi

Anastahili kwa lipi? Kukanusha kuwa sera ya elimu ya lowasa haina maana. Hivi kuna jambo lolote lisilohitaji elimu hapa ulimwenguni. Hivyo viwanda, mahakama ya mafisadi, hospitali, mashule na vyuo, na vinginevyo atakavyoanzisha vitasimamiwa na watanzania wasio na elimu au tutaletewa wataalamu kutoka nje? Ukiletewa kifaa kipya tu unahitaji kupata elimu ya jinsi ya kukitumia. Ongeeni kama watu mnaofikiri kwanza sio kukurupuka kama nyati.
 
Anastahili kwa lipi? Kukanusha kuwa sera ya elimu ya lowasa haina maana. Hivi kuna jambo lolote lisilohitaji elimu hapa ulimwenguni. Hivyo viwanda, mahakama ya mafisadi, hospitali, mashule na vyuo, na vinginevyo atakavyoanzisha vitasimamiwa na watanzania wasio na elimu au tutaletewa wataalamu kutoka nje? Ukiletewa kifaa kipya tu unahitaji kupata elimu ya jinsi ya kukitumia. Ongeeni kama watu mnaofikiri kwanza sio kukurupuka kama nyati.

Nafikiri wewe ndo umekurupuka kama nyumbu kwani kwenye ilani ya magufuli hakuna elimu?
 
Uko sahihi..swali la kujiuliza...mbadala wa ccm ni chama kipi? Dr Slaa angeongoza jahazi wengi tungesupport....lakini hatuwezi kuondoa vibaka tukaweka majambazi

Usipende kuongozwa na hisia unatakiwa uwe na uhakika na jambo unaloliongea, nikikuuliza hayo majambazi ni akina nani na wameiba nini katika nchi natumai utanipa majibu yenye facts kuliko porojo. Nadhani unaujua mfumo wa serikali na chama chake cha ccm ulivyo sema unataka kujitoa ufahamu, Lowasa anaitumia chadema na ukawa kuingia ikulu ili kuvunja mfumo wa utawala wa chama kimoja hivyo hivyo ukawa wanamtumia Lowasa kwenye kushika madaraka ya nchi. Achana na propaganda amabazo hazitakusaidia kwa sasa watu hawaambiliki hata uwaambie vipi kuwa Lowasa ni fisadi bado watamchagua
 
Nafikiri wewe ndo umekurupuka kama nyumbu kwani kwenye ilani ya magufuli hakuna elimu?

ukusikiliza vizuri wewe alidai Lowasa kashikilia elimu tuu kasahau viwanda mashule na vinginevyo hivyo vyote vitaletwa na watu wasio na elimu ujenzi nao unahitaji elimu haijalishi ni formal au informal
 
Katika thread mbalimbali nimewahi kupost haya:

Kumpokea na kumfanya(Lowassa) mgombea urais, hilo litahalalisha kura yangu na zawengine wanaoniamini tutazipeleka kwingine.

EL hajasimama mwenyewe kwenye maamuzi haya. EL kasimamishwa na KITENGO kwa kazi maalum kuua Ukawa. Anaelekea kutekeleza kazi aliyotumwa.

Natangaza rasmi akitangazwa kuwa Mgombea urais kura yangu na wengine ambao wako nami mtakuwa mmezikosa.

El imara ni yule atakaye jitengenezea historia yake kwa kujivua nyadhifa zote ndani ya CCM, atakaye Achana na masulufu ya uwaziri mkuu aliousema ndilo lilikuwa tatizo na si Richmond kama watanzania walivyo aminishwa lakini akubali kubaki kama mwanaCCM wa kawaida.
Kama amegoma kufuata ushauri wangu awe tayari kukabiliana na vitendo vya viitengo.
Unajua El anaweza kuwa ndani ya Kitengo cha Tawala. Na sasa ndiye anatumika na kitengo hicho kuua Ukawa na Chadema...! hapa yanahitaji macho ya ziada kufanya uchunguzi makini katika 'move' hii.

Ili Edward ... kuwa ana maamuzi maamuzi magumu afanye yafuatayo:

1. Ajudhuru/ajiuzuru nyazifa zote ndani ya chama (ulezi wa vijana nakadhalika) abaki mwanachama wa kawaida.
2. Atangaze adharani kuwa kuanzia sasa hatachuku masurufu ya uwaziri mkuu wa kustaafu.
3. Atangaze kuwa anaachia ngazi ya uwenyekiti wa kamati ya 'usalama' ya bunge, maana bunge halijavunjwa rasmi
mpaka tarehe ishirini kama mkulukulu alivyosema.
4. Atangaze rasmi kwa wafuasi wake (kama wapo), kuwa sasa wafanye maamuzi wanayoyataka bila kuathiri sheria za
nchi na watumie haki yao ya kikatiba kuamua kuchagua yeyote wanayeona anafaa kutuongoza katika nchi yetu bila
kujali yeye ameamua kumuunga mkono nani.
5. Awaombe wanaCCM wamsamehe kwa kukaa kimya juu ya mchakato wakuteua mgombea, ila sasa wamruhusu kuwa
mwanachama wa CCM aisiye na cheo cochote ndani ya chama.
6. Atangaze rasmi kuwa atakuwa tayari kushirikiana na rais YEYOTE ambaye atachaguliwa na watanzania wote na yeye
akiwemo kama raia wa kawaida na si mgombea.
7.....

MwanaJF unaweza kuongeza mengine ambayo unadhani kwa hekima,busara, na tahadhari kubwa Edward anatakiwa kuyafanya.

Nadhani bado niko sahihi....!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom