Kama si Lowassa ni Dr. Magufuli. Mmoja kati ya wagombea hawa wa CHADEMA na CCM ataibuka kidedea kwenye uchaguzi utakaofanyika Oktoba 25. Kulingana na kampeni zao na za wengine, ni wazi kuwa hawa wawili ndiyo wagombea wenye nguvu kubwa ba ushawishi kwenye uchaguzi wa mwaka huu. Wakati Lowassa akibebwa na mkusanyiko wa vyama na watu, Magufuli anabebwa na uimara wa CCM.
Watanzania wamegaanyika pande mbili. Wapo wa Lowassa na wale wa Dr. Magufuli. Ni kama vile Simba na Yanga. Kama mtu si mshabiki wa Simba basi atakuwa wa Yanga. Lowassa anachanja mbuga, Dr. Magufuli anachanja mbuga pia. Mpambano wa kukata na shoka unaendelea. Dr. Magufuli anasaidiwa kujibu mapigo,hasa ahadi za UKAWA na Serikali. Mfano ni majibu ya Waziri Sitta kuhusu mabehewa na ATC.
Lowassa naye hajabaki bila wasaidizi. Wapo akina Sumaye, Mgeja, Masha na Tambwe ambao ni specialists wa kujibu shutuma na vijembe vya wapinzani wao juu ya Lowassa. Wao wakimwachia Lowassa akijinadi na kumwaga ahadi, wanajibu mapigo ya kikampeni hadi basi. Dr. Magufuli na Lowassa ndiyo wagombea waliopaswa kuwa pekee mwaka huu. Wengine wanasindikiza tu.
Ni jino kwa jino;bega kwa bega. Ni mechi ya karne!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam