UKAWA tuache Kuzomea Wavaa Nguo za CCM

UKAWA tuache Kuzomea Wavaa Nguo za CCM

Kwani Kuzomea Ni Kosa? Kuzomea Ni Kinyume Cha Kushangilia Je? Iweje Mtu Ufulahie Kushangiliwa Tu Inapogeuka Upande Wa Pili Uchukie?

Mungu ibariki Tz . Mungu amuru roho wa ulewa atawale akili za Watz.
 
Haya yote yalishatabiriwa ccm wasipo acha kugawana pesa za watanzania kwenye sandarusi na kuacha wizi kunasiku watashindwa kuhutubia kwenye mikutano watu wamewachoka ndani ya watu 20 unakuta mtu mmoja tu ndio ccm na ukimuliza kwanini unaipigia ccm kura anakuambia mwaka huu sitawapigia ccm.
Ccm imekuja kuwa chama cha aibu kama ugonjwa wa kipindu pindu!!
 
Kweli, mimi ni muumini wa upinzani tokea mwaka 1992,wakati huo huo wazazi wangu wote wawili walikuwa ni wanaccm,tena viongozi,ila nakumbuka mama yangu aliwahi kuninunulia kalenda niliyoipenda mwaka 2000 iliyokuwa na picha ya mgombea urais wa upinzani kwa sababu tu alijua naipenda!! Hata sasa Mama ni mwana ccm, najaribu kubadili itikadi yake taratibu bila karaha,ila sitavumilia siku nikikuta mwana ukawa mwenzangu akimzomea!!! Nitaweka itikadi pembeni!! Wengi wetu pia wana ndugu,jamaa ama marafiki walio upande mwingine wa itikadi,sidhani kama watavumilia kuona wakidhalilishwa kutokana na msimamo halali walionao,si heshima,si ustaarabu kumdhalilisha mwenzio kutokana na itikadi yake kutofautiana na yako,tuzomeane hukuhuku JF,yasifike kwenye familia zetu,kwenye jamii zetu,maana mtoto wako pia siku moja ataweza kukuzomea!utachukua hatua gani?

Waelimishe wenzio wengi wao shule ndogo.
 
My take: jambo muhimu na la msingi zaidi ya kuzomea ni kupiga kura kuondoa ccm madarakani 25/10/2015. Haya mengine ni sahihi ila si kila sahihi inafaa. Vyote ni vizuri ila si vyote vifaavyo. Tabia nzuri ni kutumia kura yako kwa uadilifu kuondoa ma ccm madarakani

Bahati mbaya hao wanaozomea hawajajiandikisha kupiga kura.
 
Kwanza anavaa nguo za kijani ili! Ccm wasitukumbushe dhuluma na umasikini waloleta.nasema wazomewe tu.
 
Wamenizomea mwenge stand hadi nikakosa amani.kumbukeni watz ccm ndiyo inayolinda amani ya nchi hii
 
Imekuwa kero sasa hususan katika miji mikubwa kuona au kusikia zomea zomea kutoka kwa wapenzi, wanachama na mashabiki wa muungano UKAWA kwa wananchi wanaopita mitaani hali wamevaa nguo za CCM. Hili la kuzomea si sahihi kwa kuwa sio lazima wote tuwe wana UKAWA. Tuwasamehe na kuendelea kuwa wastaarabu kwa kuwa tunafanya kampeni za kistaarabu.Najua ni vigumu kuendelea kuona nguo za ccm au ccm yenyewe lakini mwisho wa yote tutaishi ndani ya Tanzania yetu tukiwa tofauti kiitikadi japokuwa ccm watakuwa wachache sana ama hakuna kabisa. Tuwaache na ubaya wao na maangamizo ndani ya mioyo yao kwa kukataa ukweli wa kukataliwa na wapenda mabadiliko. Suluba ya UKAWA inawatosha tusiwaumize zaidi.
Kweli, mimi ni muumini wa upinzani tokea mwaka 1992,wakati huo huo wazazi wangu wote wawili walikuwa ni wanaccm,tena viongozi,ila nakumbuka mama yangu aliwahi kuninunulia kalenda niliyoipenda mwaka 2000 iliyokuwa na picha ya mgombea urais wa upinzani kwa sababu tu alijua naipenda!! Hata sasa Mama ni mwana ccm, najaribu kubadili itikadi yake taratibu bila karaha,ila sitavumilia siku nikikuta mwana ukawa mwenzangu akimzomea!!! Nitaweka itikadi pembeni!! Wengi wetu pia wana ndugu,jamaa ama marafiki walio upande mwingine wa itikadi,sidhani kama watavumilia kuona wakidhalilishwa kutokana na msimamo halali walionao,si heshima,si ustaarabu kumdhalilisha mwenzio kutokana na itikadi yake kutofautiana na yako,tuzomeane hukuhuku JF,yasifike kwenye familia zetu,kwenye jamii zetu,maana mtoto wako pia siku moja ataweza kukuzomea!utachukua hatua gani?
Naunga mkono hoja kwangu wazazi na wife ni CCM, ili UKAWA iweze kukabidhiwa nchi hiyo October 25 lazima kwanza ithibitishe uwezo wa managing political diversity kwa kuwastahimili hata wale ambao haikubaliani nao, kwa sababu 90 % ya watumishi wa umma ni CCM. 99.9% ya vyombo vya ulinzi na ualama ni CCM, UKAWA has to take them on board and live with them.
Pasco
 
Wachafu kuzomewa ndo suluhisho na pia leo maeneo ya steshen karibu na Central Police Dar wamezomewa hadi traffic ikabidi awaokoe.
 
Kwakweli hata mm hili jambo kwangu naona sii zuri tuvumiliane mana kuwa na itikadi yofauti sii kosa hatuwezi kuwa chama kimoja wote!japo inaonekana wazi watu wameichoka ccm tusiwazomee tutumie sanduku la kura kumalizia hasira.
 
kwa mtu mwenye staha hawezi kuzomea mwenzie,ukiona mtu anazomea mwangalie utakutana ana mapungufu mengi
 
Zaman tulikua tukiva nguo Za upinzan hadharan ccm walikua wakituona kama wahaini acha nao waonje joto bhana
 
Mtu yeyote hata kama ni baba yangu akivaa nguo ya ccm nitamzomea tuu kwa maana hakuna nyingine tumewachoka hawa majizi wa ccm mwaka huu lazima tuwaondoe madarakani.
 
Naunga mkono hoja kwangu wazazi na wife ni CCM, ili UKAWA I were kukabidhiwa nchi hiya October 25 lazima kwanza ithibitishe uwezo wa managing political diversity kwa sababu 90 % ya watumishi wa umma ni CCM. 99.9% ya vyombo vya ulinzi ni CCM we have to take them on board and live with them.
Pasco[/QUOTE Pasco mabadiliko yataletwa na watumishi wa umma na vyombo vya ulinzi vya ccm ambavyo wamechoka na huu ugumu wa maisha unaoendelea mwaka huu lazima ccm iondoke madarakani .
 
Last edited by a moderator:
Mi nadhani ktk democracy hili la zomea halina nafasi ingekuaje miaka ya 2000 km magamba wangeyafanya haya c tungesema wanafanya kwa 7bu wao ndo watawala???? Tuache siasa za chuki
 
Mbona kule bungeni maccm walikuwa wanazomea ukawa hukuanzisha mada hapa we mburula???

Yaani mimi.ndio.naongoza kwa kuwazomea na nimenunua vuvuzela nawapulizia matakon.i kabisa.shenzi.hawa
 
Back
Top Bottom