UKAWA sasa IKAWA?

UKAWA sasa IKAWA?

Kwa bandiko hili MMM amejitangaza rasmi kuwa adui wa mabadiliko. Kumbe zile ngoja ngoja, subiri subiri na kauli zinazofanana na hizo zilikuwa ni ishara ya kutumikia kusudi lililo kinyume na shauku ya watu kupata mabadiliko

Ni kweli..MMM ni adui wa mabadiliko yanayongozwa na vipofu
 
UKAWA sasa imekuwa ni IKAWA! Vyama vitatu vinavyounda ushirikiano huu wenye mashaka tayari vimekuwa na matatizo na viongozi wao wajuu kisa UKAWA. Imekuwa hivyo kwa CHADEMA - na kuondoka kwa Dr. Slaa - Katibu Mkuu, CUF - kwa Prof. Lipumba (Mwenyekiti) na sasa NCCR-Mageuzi na malalamiko ya Makamu Mwenyekiti na Katibu Mkuu kuhusiana na dubwasha hili.

Kuna ushirikiano wowote unaokosa misukosuko?
Tena mbaya kwenye siasa ambayo Chama Dola ina miaka 50 madarakani?
Kuna tofauti gani ya mazingira ya siasa ya sasa na za enzi ya UKoloni?
Hivi bado unaamini huku kote na mawazo huru ya mtu mmoja mmoja ?
Hivi mfano wa Kipenzi chako Dr hakujatosha kupa jibu kuwa Chama dola imeshaanza kutumia nguvu ya pesa?


Kimsingi sasa UKAWA imekuwa IKAWA kwani itakuwa ni shida nyingine ambayo hata hatujaifikiria sana; kwamba tayari vyama hivi vina migogoro ya ndani kuhusiana na ushiriki wao kwenye UKAWA na wengine kwa maamuzi ya kusimamisha wagombea mbalimbali. Ngoma yote itakuwa chungu pale baada ya Uchaguzi vyovyote itakavyokuwa - wakishinda CHADEMA na wagombea wake au wakishindwa kutakuwa na matokeo kwenye vyama hivi vikuu.


Kwa hiyo CCM ikishindwa hakuna matokeo?
Hivi kwenye mechi si kuna anayeshinda na anayeshindwa?
 
Msimshangae sana huyu MM kuwa namna hiyo. Kwani hamjui ya kuwa mtu akiwa CCM anakuwa na mawazo ya ajabu kabisa? Tumeona Ma Prof, Dr, Injinia nk, wanapohamia CCM tu utaona vituko katika kujenga hoja ... akili zote sijui huwa zinapotelea wapi. Sasa huyu naye linganisha hoja before & after kutoka upinzani ... Vioja kabisa, kama hii ndo umeandika nini?! Unahitaji maombi mkuu.
 
Mzee Mwanakijiji ungeonekana wa maana kuhamasisha mabadiliko kupitia chama mbadala na Ukawa..badala yakutumia nguvu nyingi kuuponda huku ukiacha room kwa ccm kuendelea ...

Baada ya uchaguzi heshima ya huyu Mwanakijiji hapa jamvini itakuwa imeharibika kabisa
 
huyu naye...CCM tunakuangalia tu. Hata hueleweki unachokitaka, unaenekana kwamba wewe ni mfuasi wa mke wa dr. Slaa, maana hata dr. Slaa anayakubali mabadiriko haya na ndiyo maana akamfuata na kumuomba lowasa ajiunge nao. anachofanya slaa sasa hivi ni maelekezo ya josefini ambaye hata wewe unaonekana ni mfuasi wake sugu kabisa.siku dr slaa akizinduka toka katika 'usingizi' aliolazwa kitu cha kwanza atakachofanya ni kulekea bahari bichi hotel kwa ajili ya kuendelea na shuguli za kumkalibisha lowasa, sasa sijui wewe utasimamia lipi hapo. by ze way CCM tumewawezeni sana mpaka mmechanganyikiwa
 
Sio muungano wa Kilaghai tuliutarajia wengi, sio muungano wa kusigina Democrasia, kwa hali ilivyo sasa utaita muungano au "Genge" no planning, no strategy, no leadership..no reasoning, no motive, no ambitions, no mission, no vision ni uhuni na utapeli wa hali ya Juu, Chadema ikishinda uchaguzi Tz itakua ni Nchi inayoongozwa na Majuha Duniani elewa katiba iliyopp niya 1977 hebu nipangieni Baraza la Mawaziri la hawa matapeli usinitajie Mnyika,Sugu, Nyerere, Mbowe,Msigwa, Lema etc hawana sifa zote za kua viongozi.

Hebu Tulia dawa iingie wewe. mkumbuke hata mtu au mnyama anapokata roho lazima anafurukuta. Mtatoa kila aina ya kashfa lakini haitasaidia, safari hii mnalo
 
Mwanakijiji unajidhalilisha,unaelewa kabisa katiba yetu hairuhusu vyama kuungana na kuwa chama kimoja,kwa msingi huo upinzani lazima ilikuwa utengeneze umoja husio rasmi na wewe ulikuwa unalipigia hilo chapuo. Mwanzo nilifikiri ulikatishwa tamaa kwa hatua ya Lowasa kuwa mgombea ukawa kumbe hata mgombea angekuwa mwingine haukubali umoja wa vyama kuunganisha nguvu kuiondoa CCM!!!.Wewe kumbe ni mamluki wa chama kile mkuu.Unajidhalilisha au umezeeka mnoo sasa.Rudi nyumbani Mzee si vyema kuzeekea Ughaibuni kiasi hicho Mzee.
 
Too low Mwanakijiji, kwani pilipili usioila yakuwashia nini?

Kura yangu ni mabadiliko.

Mwanakijiji is a Tanzanian and he has every right to talk about the future of his country. Why do u believe that any presidential aspirant if he wins he will be the president for only those who voted for him n thus those r the only ones who shall benefit .

Kwa hiyo pilipili iliyo shambani yatuwasha watanzania wote.
 
team lowasa na uzushi hamjambo.
nakumbuka 1995 mlimzushia sumaye ana tilioni kadhaa nje ya nchi.
Leo kawa rafiki wa kuwakomboa watz
Wanageuza watanzania kama chapati. Ila baadhi ya wanasiasa wamekimbilia UKAWA iwe sehemu ya wao kujificha.
 
UKAWA.jpg


Dubwasha hili linaundwa na vyama vinne; vitatu kati ya hivyo ni vikubwa na vina historia ndefu tu ya upinzani Tanzania. Nimeliita "dubwasha" siyo kama kejeli bali ni kitu ambacho huwezi kukielezea kikaeleweka. SIyo chama, siyo muungano, siyo umoja ni ushirikiano tu fulani hivi ambao unataka kutuaminisha kuwa unataka kuja kuongoza Taifa. Kwa muda mrefu wapo watu ambao wameushabikia sana kiasi kwamba wanafikiria UKAWA ni kama chama cha siasa fulani hivi au kina mgombea au wagombea katika Uchaguzi. Kumbe UKAWA siyo chama cha siasa na hakina wala hakiwezi kuwa na Ilani, Sera, wagombea n.k.

Lakini ambacho kimethibitika mapema sasa na wengine tumeonya tangu kuundwa kwa hili dubwasha ni kuwa UKAWA unajiandaa kutuletea matatizo; tayari mengine tumeyaona na mengine yameashiriwa tu. Baada ya uongozi wa NCCR-Mageuzi nao kuja na kulalamikia dubwasha hili nimejikuta nikisema kuwa hili sasa siyo tena UKAWA bali ni IKAWA

UKAWA sasa imekuwa ni IKAWA! Vyama vitatu vinavyounda ushirikiano huu wenye mashaka tayari vimekuwa na matatizo na viongozi wao wajuu kisa UKAWA. Imekuwa hivyo kwa CHADEMA - na kuondoka kwa Dr. Slaa - Katibu Mkuu, CUF - kwa Prof. Lipumba (Mwenyekiti) na sasa NCCR-Mageuzi na malalamiko ya Makamu Mwenyekiti na Katibu Mkuu kuhusiana na dubwasha hili.

Kimsingi sasa UKAWA imekuwa IKAWA kwani itakuwa ni shida nyingine ambayo hata hatujaifikiria sana; kwamba tayari vyama hivi vina migogoro ya ndani kuhusiana na ushiriki wao kwenye UKAWA na wengine kwa maamuzi ya kusimamisha wagombea mbalimbali. Ngoma yote itakuwa chungu pale baada ya Uchaguzi vyovyote itakavyokuwa - wakishinda CHADEMA na wagombea wake au wakishindwa kutakuwa na matokeo kwenye vyama hivi vikuu.

Fikiria kwa mbali tu ije itokee wajaribu kuunda Baraza la Mawaziri...!!!

Wanachama wa vyama hivi huko waliko nina uhakika wanaangalia kwa makini yanayoendelea kwenye vyama vyao; ukimya wao sidhani kama ni woga...

Na Itakuwa IKAWA kweli kweli...

NLD peke yao inaonekana ndio wamenufaika zaidi na dubwasha hili!

MMM

Mzee Mwanakijiji naona unaanza kuchanganyikiwa baada ya kubaini kuwa kitumbua chako kinakaribia kufika ukingoni..

Mzee ni hivi; matatizo ya watanzania chini ya ccm ni makubwa kuliko matatizo ya UKAWA..!!
 
Kiukweli hawa jamaa wamebakia wakishabikiwa na mijitu isiyo jitambua, hapo hakuna ukawa wala kitawa hovyo hovyo, na mengi nipale watakapo pigwa lauso na huyo mmewao MAMVI oktoba najua watakuja na staili ya kulia lia
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji, ulikuwa ukitetea ustawi wa demokrasia na kutaka mabadiliko ya uongozi hapa Tanzania na kwingineko. Umekuwa ukiwataka wapinzani waungane ili wawe na nguvu kwenye uchaguzi na kuweza kuiondoa Serikali iliyo madarakani kwa njia ya kura. Leo hii unaita UKAWA dubwasha!? Nini kimekupata kaka? Ndawakiki wikita naa?

Mzee Tupatupa

Mkuu Vuta Nkuvute pesa ni sabuni ya roho, waswahili wanasema, penye udhia penyeza rupia na hakika imeweza kupenya kwa huyu mzee wa ughaibuni. RIP MMM
 
Aiseee watu mnabadirika hata ww mwanakijiji? Leo hii unasema ukawa dubwasha..ni hivi mabadiriko ni lazima wala hamtuludishi nyuma
 
Baada ya uchaguzi heshima ya huyu Mwanakijiji hapa jamvini itakuwa imeharibika kabisa

Ndugu Ngorunde, nakuhakikishia ya kuwa baada ya uchaguzi wana Chadema mtakuja kumheshimu MMM, kwa mtazamo,Busara an ukweli wake, Mark my words Lowassa and team will loose the election. Baada ya uchaguzi Ndugu MMM, wana CDM Asilia wakiongozwa na Dr Slaa watakuja kuikomboa Chadema na kusafisha matita yote ya kifisadi Ndani yake. Muwe wavumilivu CDM kitarudishi kwenye misingi yake na kitakombolewa kutoka kwenye mikono ya familia ya mtei, it will truly become the People's party for the first time in its life.
 
Mkuu Vuta Nkuvute pesa ni sabuni ya roho, waswahili wanasema, penye udhia penyeza rupia na hakika imeweza kupenya kwa huyu mzee wa ughaibuni. RIP MMM

Mbona nyie hampendi ukweli hata siku moja, Hiyo Rupia imepenyezwa kwenye Uongozi wa Chadema na wakampisha Baba la Mafisadi kiti cha mgombea bila Kura ya maoni wala maelewano. Jiulizeni nani anayelipia hizi pesa za kampeni yenye gharama kubwa namna hizi.

Hakuna tofauti Kati ya CCM na CDM katika maandalizi ya mikutano , wote wanabeba watu kutoka mikoa na vitongoji mbalimbali kujaza viwanja na wanawalipa hao watu. Jee hizo pesa Lowassa anazitoa wapi, iwapo makubaliano Kati ya CDM na Lowassa ni kuwa Mgombea aje na pesa za kampeni.
 
Hata kipindi ASP na TANU zinaungana na kuunda CCM, misukosuko na migongano haikukosekana japokuwa wazee waasisi wa vyama vishiriki (TANU na ASP), walikuwa na nguvu ya ajabu.

UKAWA itahimiri misukosuko kama ilivyohimiri CCM wakati inaundwa.

Mungu ibariki UKAWA.
 
Back
Top Bottom