Dubwasha hili linaundwa na vyama vinne; vitatu kati ya hivyo ni vikubwa na vina historia ndefu tu ya upinzani Tanzania. Nimeliita "dubwasha" siyo kama kejeli bali ni kitu ambacho huwezi kukielezea kikaeleweka. SIyo chama, siyo muungano, siyo umoja ni ushirikiano tu fulani hivi ambao unataka kutuaminisha kuwa unataka kuja kuongoza Taifa. Kwa muda mrefu wapo watu ambao wameushabikia sana kiasi kwamba wanafikiria UKAWA ni kama chama cha siasa fulani hivi au kina mgombea au wagombea katika Uchaguzi. Kumbe UKAWA siyo chama cha siasa na hakina wala hakiwezi kuwa na Ilani, Sera, wagombea n.k.
Lakini ambacho kimethibitika mapema sasa na wengine tumeonya tangu kuundwa kwa hili dubwasha ni kuwa UKAWA unajiandaa kutuletea matatizo; tayari mengine tumeyaona na mengine yameashiriwa tu. Baada ya uongozi wa NCCR-Mageuzi nao kuja na kulalamikia dubwasha hili nimejikuta nikisema kuwa hili sasa siyo tena UKAWA bali ni IKAWA
UKAWA sasa imekuwa ni IKAWA! Vyama vitatu vinavyounda ushirikiano huu wenye mashaka tayari vimekuwa na matatizo na viongozi wao wajuu kisa UKAWA. Imekuwa hivyo kwa CHADEMA - na kuondoka kwa Dr. Slaa - Katibu Mkuu, CUF - kwa Prof. Lipumba (Mwenyekiti) na sasa NCCR-Mageuzi na malalamiko ya Makamu Mwenyekiti na Katibu Mkuu kuhusiana na dubwasha hili.
Kimsingi sasa UKAWA imekuwa IKAWA kwani itakuwa ni shida nyingine ambayo hata hatujaifikiria sana; kwamba tayari vyama hivi vina migogoro ya ndani kuhusiana na ushiriki wao kwenye UKAWA na wengine kwa maamuzi ya kusimamisha wagombea mbalimbali. Ngoma yote itakuwa chungu pale baada ya Uchaguzi vyovyote itakavyokuwa - wakishinda CHADEMA na wagombea wake au wakishindwa kutakuwa na matokeo kwenye vyama hivi vikuu.
Fikiria kwa mbali tu ije itokee wajaribu kuunda Baraza la Mawaziri...!!!
Wanachama wa vyama hivi huko waliko nina uhakika wanaangalia kwa makini yanayoendelea kwenye vyama vyao; ukimya wao sidhani kama ni woga...
Na Itakuwa IKAWA kweli kweli...
NLD peke yao inaonekana ndio wamenufaika zaidi na dubwasha hili!
MMM