UKAWA sasa IKAWA?

UKAWA sasa IKAWA?

Tunaipenda sana Tanzania kuliko unavyofikiria, Tuache na UKAWA yetu, Tunahitaji mabadiliko ya utawala, Tunahitaji

rasmu ya Jaji Warioba irejeshwe ili tupate katiba mpya; haya yote yanawezekana ikiwa watanzania tutazidi kujitambua

kuwafahamisha wale ambao hawajui umaskini tulio nao umetokana na usimamizi mbovu wa resources na utawala wa

kupeena vyeo.

MMM jiulize kwanini nchi kama Kenya inapaa kiuchumi kuliko sisi,? Rwanda wametoka kwenye vita miaka ya 1990s

leo ina ndege zinazopishana kwenda nje ya mipaka ya Rwanda, kwanini ss tumeshindwa?Jiunge nasi kuing'oa ccm
 
Sio muungano wa Kilaghai tuliutarajia wengi, sio muungano wa kusigina Democrasia, kwa hali ilivyo sasa utaita muungano au "Genge" no planning, no strategy, no leadership..no reasoning, no motive, no ambitions, no mission, no vision ni uhuni na utapeli wa hali ya Juu, Chadema ikishinda uchaguzi Tz itakua ni Nchi inayoongozwa na Majuha Duniani elewa katiba iliyopp niya 1977 hebu nipangieni Baraza la Mawaziri la hawa matapeli usinitajie Mnyika,Sugu, Nyerere, Mbowe,Msigwa, Lema etc hawana sifa zote za kua viongozi.

Kama Kikwete aliweza kuwa raisi wa nchi hii, hao uliowataja hapo juu wana uwezo mara dufu (kuliko huyo boss wa wacheza kigodoro) wa kuwa raisi wa Tanzania, achilia mbali uwaziri.
 
Sio muungano wa Kilaghai tuliutarajia wengi, sio muungano wa kusigina Democrasia, kwa hali ilivyo sasa utaita muungano au "Genge" no planning, no strategy, no leadership..no reasoning, no motive, no ambitions, no mission, no vision ni uhuni na utapeli wa hali ya Juu, Chadema ikishinda uchaguzi Tz itakua ni Nchi inayoongozwa na Majuha Duniani elewa katiba iliyopp niya 1977 hebu nipangieni Baraza la Mawaziri la hawa matapeli usinitajie Mnyika,Sugu, Nyerere, Mbowe,Msigwa, Lema etc hawana sifa zote za kua viongozi.

Hapo hakuna cha UKAWA wala UPAWA ni uhuni kwa kwenda mbele. Mie nawashangaa CCM kwa kuwafumbia macho na kuwakuza kwa kuwaita ukawa. Hao ni Umoja wa Kaskazini na Wachaga.
 
Awali waliunda genge la kutaka kusikikika wakati wa Bunge la Katiba. Baada ya shughuli hiyo walishindwa kujipanga ili kutengeneza muungano makini na wenye tija hali inayopelekea Chadema kutumia mwanya huo kujinufaisha.
 
Imekula kwao
 
UKAWA.jpg

Dubwasha hili linaundwa na vyama vinne; vitatu kati ya hivyo ni vikubwa na vina historia ndefu tu ya upinzani Tanzania. Nimeliita "dubwasha" siyo kama kejeli bali ni kitu ambacho huwezi kukielezea kikaeleweka. SIyo chama, siyo muungano, siyo umoja ni ushirikiano tu fulani hivi ambao unataka kutuaminisha kuwa unataka kuja kuongoza Taifa. Kwa muda mrefu wapo watu ambao wameushabikia sana kiasi kwamba wanafikiria UKAWA ni kama chama cha siasa fulani hivi au kina mgombea au wagombea katika Uchaguzi. Kumbe UKAWA siyo chama cha siasa na hakina wala hakiwezi kuwa na Ilani, Sera, wagombea n.k.

Lakini ambacho kimethibitika mapema sasa na wengine tumeonya tangu kuundwa kwa hili dubwasha ni kuwa UKAWA unajiandaa kutuletea matatizo; tayari mengine tumeyaona na mengine yameashiriwa tu. Baada ya uongozi wa NCCR-Mageuzi nao kuja na kulalamikia dubwasha hili nimejikuta nikisema kuwa hili sasa siyo tena UKAWA bali ni IKAWA

UKAWA sasa imekuwa ni IKAWA! Vyama vitatu vinavyounda ushirikiano huu wenye mashaka tayari vimekuwa na matatizo na viongozi wao wajuu kisa UKAWA. Imekuwa hivyo kwa CHADEMA - na kuondoka kwa Dr. Slaa - Katibu Mkuu, CUF - kwa Prof. Lipumba (Mwenyekiti) na sasa NCCR-Mageuzi na malalamiko ya Makamu Mwenyekiti na Katibu Mkuu kuhusiana na dubwasha hili.

Kimsingi sasa UKAWA imekuwa IKAWA kwani itakuwa ni shida nyingine ambayo hata hatujaifikiria sana; kwamba tayari vyama hivi vina migogoro ya ndani kuhusiana na ushiriki wao kwenye UKAWA na wengine kwa maamuzi ya kusimamisha wagombea mbalimbali. Ngoma yote itakuwa chungu pale baada ya Uchaguzi vyovyote itakavyokuwa - wakishinda CHADEMA na wagombea wake au wakishindwa kutakuwa na matokeo kwenye vyama hivi vikuu.

Fikiria kwa mbali tu ije itokee wajaribu kuunda Baraza la Mawaziri...!!!

Wanachama wa vyama hivi huko waliko nina uhakika wanaangalia kwa makini yanayoendelea kwenye vyama vyao; ukimya wao sidhani kama ni woga...

Na Itakuwa IKAWA kweli kweli...

NLD peke yao inaonekana ndio wamenufaika zaidi na dubwasha hili!

MMM

Ushauri kwako.Mimi nadhani ungetumia nguvu kama hii katika kuwalaghai watu waishio vijijini.maana huko ndiko ambako watu wengi hawana elimu ya uraia.ila nguvu unayoitumia ktk mitandao ya Jamii ambamo watu wengi wanauelewa wa kutosha sidhani kama inakusaidia.binafsi naamini kuwa unapoteza sana muda maana watu wameshaamua kufanya mabadiliko.hata uandike nini bado huwezi badilisha upepo.hivi unajisikiaje tangu umeanza harakati za kuwaponda ukawa bado watu wanazidi kumiminika ktk kampeni.la mwisho unahisi wewe ni zaidi ya slaa na lipumba?.kama hawa wameshindwa kubadili upepo utaweza wewe?.huo muda unaoutumia kuwaponda ukawa ungekuwa unatunga mashairi kuhusu umaskini wa watanzania na ungeuza sana
 
Ww sio mpiga kura wa nchi hii
Siasa za kwenye mtandao zitakupa presha bure

Viva ukawa!!!!!
 
ndumila kuwili ukiendelea kugeukageuka nyuma mwishowe utageuka kuwa jiwe la chumvi........
wew unajua nini kwanza umeishia darasa la pili na unawazo gan au hoja ipi ya maana au nitaarabu unatuandikia ?hii ni nchi ya vyama vingi bana usiongee upumbavu wako kama vile ccm imetoka mbinguni chizii nin?😕
 
ndumila kuwili ukiendelea kugeukageuka nyuma mwishowe utageuka kuwa jiwe la chumvi........

Hujui kitu demokrasia haipo unavyodhania rudi shule kasome tenaaaaa😯😯😯
 
Sio muungano wa Kilaghai tuliutarajia wengi, sio muungano wa kusigina Democrasia, kwa hali ilivyo sasa utaita muungano au "Genge" no planning, no strategy, no leadership..no reasoning, no motive, no ambitions, no mission, no vision ni uhuni na utapeli wa hali ya Juu, Chadema ikishinda uchaguzi Tz itakua ni Nchi inayoongozwa na Majuha Duniani elewa katiba iliyopp niya 1977 hebu nipangieni Baraza la Mawaziri la hawa matapeli usinitajie Mnyika,Sugu, Nyerere, Mbowe,Msigwa, Lema etc hawana sifa zote za kua viongozi.
Wenye sifa za Kuwa viongozi ni ccm peke yake kwenye hii nchi.
There comes a time in life you have to swallow that pill. Bitter, bitter pill. It is called pill "Mabadiliko".
It is the only pill in town that can cure you.
The rest of the pills are from madabida's laboratories.
 
Back
Top Bottom