UKAWA sasa IKAWA?

UKAWA sasa IKAWA?

Eti hawana sifa za kuwa viongozi...hapo walipo tayari ni viongozi tena mahiri!
Acha kukaririshwa kijana...

Sumaye alisema hawana uzoefu, lakini elimu zao pia ni tatizo, Tz ina wasomi wa kutosha. Sijui kama uko Serious Sugu, Msigwa, Lema wawe mawaziri wako. Mbowe Mbona misikiti yote itageuzwa Club za Usiku
 
UKAWA.jpg


Dubwasha hili linaundwa na vyama vinne; vitatu kati ya hivyo ni vikubwa na vina historia ndefu tu ya upinzani Tanzania. Nimeliita "dubwasha" siyo kama kejeli bali ni kitu ambacho huwezi kukielezea kikaeleweka. SIyo chama, siyo muungano, siyo umoja ni ushirikiano tu fulani hivi ambao unataka kutuaminisha kuwa unataka kuja kuongoza Taifa. Kwa muda mrefu wapo watu ambao wameushabikia sana kiasi kwamba wanafikiria UKAWA ni kama chama cha siasa fulani hivi au kina mgombea au wagombea katika Uchaguzi. Kumbe UKAWA siyo chama cha siasa na hakina wala hakiwezi kuwa na Ilani, Sera, wagombea n.k.

Lakini ambacho kimethibitika mapema sasa na wengine tumeonya tangu kuundwa kwa hili dubwasha ni kuwa UKAWA unajiandaa kutuletea matatizo; tayari mengine tumeyaona na mengine yameashiriwa tu. Baada ya uongozi wa NCCR-Mageuzi nao kuja na kulalamikia dubwasha hili nimejikuta nikisema kuwa hili sasa siyo tena UKAWA bali ni IKAWA

UKAWA sasa imekuwa ni IKAWA! Vyama vitatu vinavyounda ushirikiano huu wenye mashaka tayari vimekuwa na matatizo na viongozi wao wajuu kisa UKAWA. Imekuwa hivyo kwa CHADEMA - na kuondoka kwa Dr. Slaa - Katibu Mkuu, CUF - kwa Prof. Lipumba (Mwenyekiti) na sasa NCCR-Mageuzi na malalamiko ya Makamu Mwenyekiti na Katibu Mkuu kuhusiana na dubwasha hili.

Kimsingi sasa UKAWA imekuwa IKAWA kwani itakuwa ni shida nyingine ambayo hata hatujaifikiria sana; kwamba tayari vyama hivi vina migogoro ya ndani kuhusiana na ushiriki wao kwenye UKAWA na wengine kwa maamuzi ya kusimamisha wagombea mbalimbali. Ngoma yote itakuwa chungu pale baada ya Uchaguzi vyovyote itakavyokuwa - wakishinda CHADEMA na wagombea wake au wakishindwa kutakuwa na matokeo kwenye vyama hivi vikuu.

Fikiria kwa mbali tu ije itokee wajaribu kuunda Baraza la Mawaziri...!!!

Wanachama wa vyama hivi huko waliko nina uhakika wanaangalia kwa makini yanayoendelea kwenye vyama vyao; ukimya wao sidhani kama ni woga...

Na Itakuwa IKAWA kweli kweli...

NLD peke yao inaonekana ndio wamenufaika zaidi na dubwasha hili!

MMM
Mkuu inafahamika jinsi sheria inavyo bana vyama vya upinzani kuungana, sheria hizi zina ifeva ccm na hivyo haiko tayari kuzibadili. Naona mkono wa ccm kwa matukio kinzani ukawani. Kwakweli wana ukawa ni wa kupongezwa kwa hatua walio ifikia, wana fanya kazi ktk mazingira magumu na hila za CCM.
 
Sumaye alisema hawana uzoefu, lakini elimu zao pia ni tatizo, Tz ina wasomi wa kutosha. Sijui kama uko Serious Sugu, Msigwa, Lema wawe mawaziri wako. Mbowe Mbona misikiti yote itageuzwa Club za Usiku

Hao wasomi wako wamesaidia nini for the past 54 years?
Wasomi style ya akina Kapuya, Kawambwa, Tibaijuka and the likes?
Hao uliowataja ni viongozi tena wanajitosheleza kabisa...na kama wakihitaji technical advice, wapo wasomi wanaojielewa kama akina Prof Baregu watasaidia kama wanavyosaidia sasa.
 
Kila siku ukawa ukawa .... Nyie bhaaaaaanaaaa, wahenga walinena mti wenye matunda hauchokwi kupigwa mawe.... Acheni hizo jameni ummezidi ucomedi
 
Sio muungano wa Kilaghai tuliutarajia wengi, sio muungano wa kusigina Democrasia, kwa hali ilivyo sasa utaita muungano au "Genge" no planning, no strategy, no leadership..no reasoning, no motive, no ambitions, no mission, no vision ni uhuni na utapeli wa hali ya Juu, Chadema ikishinda uchaguzi Tz itakua ni Nchi inayoongozwa na Majuha Duniani elewa katiba iliyopp niya 1977 hebu nipangieni Baraza la Mawaziri la hawa matapeli usinitajie Mnyika,Sugu, Nyerere, Mbowe,Msigwa, Lema etc hawana sifa zote za kua viongozi.

Nani anayefaa kuwa waziri? Mulugo au mzee wa Kuwait?
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji, ulikuwa ukitetea ustawi wa demokrasia na kutaka mabadiliko ya uongozi hapa Tanzania na kwingineko. Umekuwa ukiwataka wapinzani waungane ili wawe na nguvu kwenye uchaguzi na kuweza kuiondoa Serikali iliyo madarakani kwa njia ya kura. Leo hii unaita UKAWA dubwasha!? Nini kimekupata kaka? Ndawakiki wikita naa?

Mzee Tupatupa

Mzee mwenzangu kweli huu ni Muungano wa kuushabikia kweli. Sijawahi kuona mfano kama huu popote. Wenga ne nikita nini inu? Ne nijovajova namuyako.
 
Last edited by a moderator:
Kwa bandiko hili MMM amejitangaza rasmi kuwa adui wa mabadiliko. Kumbe zile ngoja ngoja, subiri subiri na kauli zinazofanana na hizo zilikuwa ni ishara ya kutumikia kusudi lililo kinyume na shauku ya watu kupata mabadiliko
 
Teh Teh mkuu hamja onana na Slaa huko? wape i...
 
Mwanakijiji toka amepata ajira gazeti la UHURU na MZALENDO haeleweki anachokiandika... Roho inamuuma baada ya kuona EHM mwenzie amekosa Urais na sasa Mfumo mzima unang'olewa ... Billion 150 walizotenga CCM za kudhoofisha Upinzani zinayeyuka bila matokeo chanya...Mama na team yake wamevuta Mpunga bila kuathiri ari na kasi za MALOFA kuleta mabadiliko ya kweli Tanzania ...
 
Lowassa is a better man for a better Tanzania!
 
baada ya mipango ya kitengo ya dk na prof kushindwa ..mpango umebadilika badala kushutumu na kutoka nje...sasa mpango shambulieni mkiwa ndani ...tengeneza mgogoro wa ndani...mdhoofishie Mbatia ana kiherehere sana......ila naamini mpango huo nao utafail.........
 
Mwanakijiji na wenzake,walichokitaka ni kuwa vyama hivi vinabakia kuwa pressure group.lakini walipostuka wakakuta tayari Gia ishabadilishwa angani.wanachotakiwa kwa sasa ni kusubiri maumivu ya okt.25.kama ni karamu tayari imeshaliwa.
 
Sumaye alisema hawana uzoefu, lakini elimu zao pia ni tatizo, Tz ina wasomi wa kutosha. Sijui kama uko Serious Sugu, Msigwa, Lema wawe mawaziri wako. Mbowe Mbona misikiti yote itageuzwa Club za Usiku

udini usio na sababu ..kwa nini misikiti na wala si makanisa ....tumeshakuwa na mawaziri maprof na hawajafanya jipya....kuna mambo ya kawaida sana yametamalaki nchi kuyatatua uhitaji uwe na elimu kubwa
 
Huyo mzee hana jipya. Yeye anakula kiyoyozi sisi tunakula vumbi halafu analeta mdomo na insha zake muflisi kabisa.

Hawa watu waliokuwa wanajiita wapinzani baada ya kuona kweli upinzani unachukua nchi wameanza kugeuka. Hawa walikuwa puppet leaders
 
Yaani katika watu niliokuwa nawaona ni jembe humu ndani ni ww MMM ila kwa uzi huu umeharibu kila kitu, ILA ELEWA HATA MMSEMEJE VP SAHIZI NI MWAKA WA MABADILIKO NA MABADILIKO NI SASA hatukupangiwa kutawaliwa na CCM maisha ni muda muafaka sasa nayenyewe ipumzike iwapishe wengine nao watawale hiyo ni demokrasia ya kweli.
 
Sumaye alisema hawana uzoefu, lakini elimu zao pia ni tatizo, Tz ina wasomi wa kutosha. Sijui kama uko Serious Sugu, Msigwa, Lema wawe mawaziri wako. Mbowe Mbona misikiti yote itageuzwa Club za Usiku

Mkuu umeua
 
Back
Top Bottom