Ukawa na drone camera mwanza

Ukawa na drone camera mwanza

Panazungumziwa "camera system" au "drones"? Nafikiri ni vitu viwili tofauti. Sheria ya nchii hii bado haijawa wazi kuhusu operation ya drones, hata mradi wa Anti-poaching ulishindwa ku-take off sababu ya undumilakuwili wa kisheria

Zingekuwa zinaweka ushahidi mafisadi wangeshindwa kufanya yao kwenye pembe za ndovu,wamezipiga vita ili waendelee kuuwa tembo wetu,hii serikali ya baba nanihi ni shida tupu iondoke tu hakuna namna nyingine,sawasawa?
 
Mimi nashangaa wanataka kukuza saula hili, mtu yeyote anaweza kuagiza vidrones hivi kupitia eBay au moja kwa moja kutoka Uchina kwa bei ndogo tu - ila kwa ajili ya usalama wa anga wasiruhusu viji dudu hivi kuingizwa ki holela nchini.

Acha ushamba wewe,ukitumia simu yako au computer unaweza kuona eneo lolote ukitaka kwa kutumia googlemap sasa kuna haja gani kuzuia watu wasipige picha?kawazuieni google!
 
Acha ushamba wewe,ukitumia simu yako au computer unaweza kuona eneo lolote ukitaka kwa kutumia googlemap sasa kuna haja gani kuzuia watu wasipige picha?kawazuieni google!

Waswahili wengine bwana!! Wewe unajua Google map inafanya kazi namna gani? Kwa hiyo kwa akili zako finyu unafikili googlemap unayo iona kwenye smartphone yako au Computer inaonyesha picha za satellite in realtime!!! Jaribu kuangalia sehemu yoyote ya Tanzania usiku kwa kutumia Googlemap alafu urudi hapa jamvini utupatie feedback - mnapakukia mambo bila ya kuyatafakali kwa undani, kisa UKAWA!!!

Mimi nilizungumzia kuhusu masuala ya usalama wa anga, nikasema si busara kuruhusu watu kurusha rusha vi-drone holela, vinaweza kukosea njia vikagusa nyaya za umeme mkubwa vikasababisha mlipuko mkubwa, tukumbuke kwamba vinaongozwa by remote control hivyo kuna uwezekano mkubwa wa kukosa mawasiliano ya radio kati yake na anaye virusha akiwa aridhini, vinaweza vile vile kuingingilia katika njia za International na domestic flights wakati ndege zikiwa kwenya phase ya kutua au kupaa zika-corride na vidrone au vidrone vikavutwa na injini za jets vikaharibu compressors za injini na kusababisha ajali - hayo ndio nilikuwa nazungumzia mimi sio mambo ya siasa.
 
Link itakusaidia nini! Soma The Washington Post Online ndiyo utapata hiyo story na nyingine nyingi.

Mkuu hata mimi niliwahi kuona story hiyo, jamaa alifikisha mahakamani na kudaiwa fidia lakini inalekea waliyamaliza kiutu uzima - sasa hiyo ndio baadhi ya matatizo ya kutumia vijidrone hivyo holela!
 
Bi FaizaFoxy wanachama wanakutaka kwa udi na uvumba kwenye group la wasap la jukwaa la siasa ,ama kweli nyota yako inang'aa kama lowasa
 
Last edited by a moderator:
Labda hiyo camera ila hivo vi drone mbona vipo vingi mm nilimnunulia mwanangu 68000tsh maeneo ya msimbazi anakichaji then kinaruka kwa kutumia remote
 
safari hii kama CCM watataka kuhujumu mikutano ya UKAWA kama walivyo fanya kwa chadema arusha,itabidi wajipange sana kutengeneza mazingira ya kupoteza ushahidi,maana hizo aerial shot huwa hazidanganyani,kila kitu kitajulikana.

kuhusu drone camera,kwa sasa si jambo geni hasa baada ya makampuni mengi kijihusisha kuunda drone camera za aina mbalimbali.hata bei yake si ghari sana kutegemeana na mahitaji ya mnunuzi.

hapa bongo tayari kuna wabongo ambao ninawafahamu,wanazo hizo drone camera na wanazitumia ktk ku-shoot music videos.kenya pia baadhi ya watu wanazo.

hizi ni baadhi music video za wabongo ambapo baadhi ya shots zilichukuliwa via drone camera.

 
Last edited by a moderator:
Ya bei ya chini kabisa ni $80
Japo zipo hadi za $ 700 ambazo zina technology ya 3D
Hizi kitu kisheria inatakiwa iidhinishwe na sheria za nchi coz kuna sehemu zingine ambazo kutumia hizi camera ni makosa na pia unaweza kufungwa kama sio kupigwa faini!
Hizi camera zinarushwa angani
Na pia zinakuwa controlled na remote!

Mkuu uko sahihi.

Hii camera nliitumia kwenye mambo ya utalii mwezi wa 6, lakini tulipofika eneo la Ngorongoro tulikatazwa kuitumia.

Bukyanagandi amefafanua vizuri kuhusu matumizi ya hizi camera sheria za anga.

Kuna uwezekano mkubwa zikapigwa marufuku kwenye kampeni kwa kigezo cha sheria za usalama wa anga na mbuga za wanyama.
 
Nimeona moja inaoñyesha jinsi ambavyo zinaweza kutumika kufanya uhalifu,ni hatari sana zikitumika hivyo.
 
Back
Top Bottom