UKAWA kwenda kudai posho mahakamani

UKAWA kwenda kudai posho mahakamani

Wabunge wapewe haki inayofanana na ile haki waliopewa watumishi wa Umma ambao hawapo kazini lakini walikuwa walilipwa.Kama utaratibu umebadilika kwa Watumishi basi na Wabunge nao iwe hivyo.Kama bungeni hawapo wanalipwa kwa kazi gani?
 
ingekuwA ni mshahara wangeshinda ila posho sizani!! wanajiaibisha bure
 
Kuna wachezaji mpira wao wapo bench tokea ligi inaanza mpaka inamaliza. Na wanapata mshahara na posho pia sasa kuna kosa gani kwa wabunge wa Ukawa kuidai haki yao? Mbona kuna wabunge wanachangia kuvuliwa kibarahashia tu na posho wanapewa.
Watalipwa,Hamna sharia inayozuia kulipwa. Mkwara tu huo...
 
Nimekua nikiwaunga mkono lakini hapo wamekoseaa sanaaaaa.

Na hiyo itakuja kuwatesa sanaaaa hapo mbeleni. Wataonekana wanaeka maslahi yao mbele kuliko ya wananchi.

Zitto is the only one who is leading the way sasa hivi kwenye kuleta mapinduzi na mabadiliko ya kweli. Hawa wengine naanza kupata wasiwasi nao.
Wabunge njaa..
 
sasa kwa nini walikataa posho pindi spika alipowanyima, wakati wanajua ni haki yao? au hawakuielewa katiba inasemaje juu yaposho. AU UKATA UMEZIDI. MAGU KAFICHA PESA.

kwani bungeni mwenye jukumu la kuratibu na kuongoza bungeni ni nani si spika?

ikiwa hawamtaki naibu spika kwa nn wasilete hoja bungeni na kuipeleka mahakamani, mpk wazunguke mitaani inamaana hawajui namna ya kumuengua spika. katiba inassema spika atachaguliwa na wabunge pia kutenguliwa na wabunge kwa kufuata sheria, mbona wao hawafati sheria
Wanalala hotel za Buku 5000 na kushindia mihogo.. Mag noma sana
Ukawa njaa kali,mikopo ya magari na mikopo ya mishahara,marejesho ni lazima upate posho kwa sababu safari hakuna,lazima sasa wanalaumiana kuingizana mkenge,Tulia bado anapeta na wala hana dalili za kujiuzulu achilia mbali kung'olewa
Halafu mahakama haina mamlaka na yanayozungumzwa bungeni labda kama ni kufafanua vifungu vya katiba,alichoamua naibu spika akiwa kwenye kiti hakihojiwi na chombo chochote,hiyo kesi itaanguka siku ya kwanza tu,ukawa waache kuwadanganya wafuasi wao
 
Basi haya kama ni wa Lumumba waweke no zao apa warushiwe buku 7 zao
Mbowe anawaburuza wenzake wakati yeye ana vyanzo mbadala vya mapato ikiwemo hata access ya ruzuku,hawa wengine wenzangu na mimi ndio watakua wamelianzisha hili la kwenda mahakamani.
 
Hii nchi soon itakuwa kama Zimbabwe,,hivi huyu jamaa Mugabe anashindaje na matatizo yote haya.
 
Kwani wale waliokaa pale na kunyamaza kimya wamefanya kazi gani? Au yule wa kujenga mnara wa push up, ingekuwa watu wanalipwa kwa performance na zinatoka mfukoni mwako, ungempa ngapi yule?
Hivi wewe wakati unasoma primary ilikuwaje,wewe ukiitwa jina ukaitika nipo ata kama ulikuwa,unasinzia,itakuwa sawa na yule ambae hayupo darasani?
 
#JamboLEO Wabunge UKAWA kwenda mahakamani baada ya kunyimwa posho kutokana na kuingia bungeni kusaini kisha kutoka
View attachment 363530
Nasoma kitabu cha darasa la nne 1997 SIZITAKI MBIVU HIZI.
kama wana madai wana haki lkn ninashauri waanze kumshitaki mwajiri wao office za labour ikishindikana waende baraza la upatanishi na usuluhishi ndiyo wakikwama waende mahakamani
 
Kitabu cha Kusoma Darasa la III/73. Shairi 'Sizitaki Mbichi Hizi'. Mchoro Sungura amekodolea macho ndizi mbivu. Kitabu kina mashairi 2; shairi la kwanza ni la Sikili (mtoto mvivu).

Sikili mimi maskini uvivu wangu nyumbani, nikiwa humu njiani nakufa hapa kwa nini,
Sadiki sasa ashiba chakula kingi kwa baba, nirudi tena nyumbani nakufa hapa kwanini?

Posho: Tulia alitumia Mwongozo wa Spika wa Bunge wa 2008 (precedence) kuamua UKAWA wanyimwe posho. Mahakamani watakwenda kupoteza muda mwingine. Walaumu uongozi wao na wao wenyewe kushindwa kujiongoza vizuri. UKAWA Bungeni have lost both the battle and war, period. Tunaojua tuliwashauri tangu mwanzo kuwa they were heading and trending to fail.
 
Walisema hawana haja na hizo posho, sasa mahakamani wanafuata kitu gani? Kumbe walikuwa wanatingisha kiberiti.
 
Wabunge wa UKAWA waliositishiwa posho zao baada ya ule mchezo wa kutoka bungeni sasa kudai posho zao mahakamani.
View attachment 363532
Hiii sijui imekaaje mtu kuhangaikia pato ambalo hujalifanyia kazi.
Vipi kuhusu KITWANGA tangu alipotumbuliwa hakuwepo Bungeni je wewe mleta mada unaweza kutupatia taarifa je huyo KITWANGA alilipwa posho au hakulipwa posho? na tunajua Ndugai hakuwepo bungeni je na yeye kapewa posho za vikao vya Bunge au kanyimwa?
 
Tutapata ufafanuzi soon

Alafu wale wa Bunge wa CCM waliopewa mpaka barua na chama kwa kutohudhuria vikao nao walinyimwa posho?
Posho kupata ni mpaka uhudhurie kikao au uingie na kusaini, wale hawakuwepo kabisa
 
hivi wewe ni mlipa kodi katika nchi hii kweli.? nina wasiwasi. utakuwa under age. hivi walipwe kwa kitu gani. si bora pesa hiyo ipelekwe kununulia madawati mashuleni au madawa hospitalini. ni nani aliwatuma wagome.? kuna yeyote alienda kwenye jimbo lake na kuomba watu wake kuwa anaenda kugoma bungeni na akakubaliwa. ni lazima tujue wabunge wameomba kazi kwa wananchi majimboni. wakapewa kazi na ni lazima waende bungeni kuwafanyia kazi. na sio kwenda kugoma kula na kulala tu. nani anagharamia muda huu uliopotea. tena ningeshauri hata mishahara yao ingekatwa kwa siku zilezote ambazo hawakufanya kazi.


umewahi kumsikia abood wa morogoro toka bunge lianze hadi linaisha akitetea au kutoa hoja kuhusu watu wake wa huko moro? Kwa hiyo kod kwa wabunge wa dizain za masanamu na abood zinalipwa sahihi?
 
Mi sijawah kumsikia nyoka mwenye makengeza akitetea au kutoa hoja kuhusu jimbo lake na yupo kila cku bungeni na posho anachukua bora hata yule wa tamisemi zaman aliamka kutetea viinua mgongo vyao walipotaka kuviingilia na yule anataman kuli anasikia uchungu bunge likioneshwa live.
 
Kitabu cha Kusoma Darasa la III/73. Shairi 'Sizitaki Mbichi Hizi'. Mchoro Sungura amekodolea macho ndizi mbivu. Kitabu kina mashairi 2; shairi la kwanza ni la Sikili (mtoto mvivu).

Sikili mimi maskini uvivu wangu nyumbani, nikiwa humu njiani nakufa hapa kwa nini,
Sadiki sasa ashiba chakula kingi kwa baba, nirudi tena nyumbani nakufa hapa kwanini?

Posho: Tulia alitumia Mwongozo wa Spika wa Bunge wa 2008 (precedence) kuamua UKAWA wanyimwe posho. Mahakamani watakwenda kupoteza muda mwingine. Walaumu uongozi wao na wao wenyewe kushindwa kujiongoza vizuri. UKAWA Bungeni have lost both the battle and war, period. Tunaojua tuliwashauri tangu mwanzo kuwa they were heading and trending to fail.

Sio kweli, umesahau pia kama mnataka mali mtazipata shambani, sizitaki mbichi hizi, sadiki na chitemo
 

Attachments

  • 1467829322739.jpg
    1467829322739.jpg
    19.4 KB · Views: 123
Wako sawa kabisa! Kuna kanuni/sheria inayosema usipohudhuria vikao vya bunge unanyimwa posho. Sheria ipi aliitumia Tulia kuwanyima posho? It makes sense , ni kuwa watu hatujui haki zetu. Ni sawa kama upuuzi anaoufanya Fastjet kuahirisha safari bila kuwa na alternative air transport or accommodation to the would be passengers! Only recently one advocate has approached the court to that effect and has won the case!
Tulia alitumia sheria ya Mungu inayosema asiyefanya kazi na asile
 
Sio kweli, umesahau pia kama mnataka mali mtazipata shambani, sizitaki mbichi hizi, sadiki na chitemo
Nadhani hukunielewa ndugu. Shairi la kama mnataka mali:

Karudi Baba mmoja, toka safari ya mbali
Kavimba yote mapaja, na kutetemeka mwili
Watoto wake wakaja, ili kumtaka hali
Wakataka na kauli, iwafae maishani.

Akatamka mgonjwa, ninaumwa kweli kweli
Hata kama nikichanjwa, haitoki homa kali
Roho naona yachinjwa, kifo kimenikabili,
Kama mwataka kauli, semani niseme nini.

Yakawatoka kinywani,maneno yenye adili,
Baba yetu wa thamani,sisi tunataka mali,
Urithi tunatamani,mali yetu ya halali,
Sema iko wapi mali, itufae maishani.

Baba aliye kufani, akajibu lile swali,
Nina kufa maskini, baba yenu sina mali,
Neno moja lishikeni, kama mnataka mali,
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.

Wakazidi kumchimba, baba mwenye homa kali,
Baba yetu watufumba, hatujui fumbo hili,
Akili yetu nyembamba, haijajua methali,
Kama tunataka mali, tutapataje shambani.

Kwanza shirikianeni, nawapa hiyo kauli,
Fanyeni kazi shambani, mwisho mtapata mali,
Haya sasa buriani, kifo kimeniwasili,
Kama mnataka mali mtayapata shambani.

Alipokwisha kutaja, fumbo hili la akili,
Mauti nayo yakaja, roho ikaacha mwili,
Na watoto kwa umoja, wakakumbuka kauli,
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.

Fumbo wakatafakari, watoto wale wawili,
Wakakata na shauri, baada ya siku mbili,
Wote wakawa tayari, pori nene kukabili,
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.

Wakazipanda shambani, mbegu nyingi mbalimbali,
Tangu zile za mibuni, hata zitupazo wali,
Na mvua ikaja chini, wakona na dalili,
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.

Shamba wakapalilia, bila kupata ajali.
Mavuno yakawajia, wakafaidi ugali,
Wote wakashangilia, usemi wakakubali,
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.

Wakawanunua ngómbe, majike kwa mafahali,
Wakapata na vikombe, mavazi na baiskeli,
Hawakuitaka pombe, sababu pombe si mali,
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.

Wakaongeza mazao, na nyumba za matofali,
Pale penye shamba lao, wakaihubiri mali,
Walikiweka kibao, wakaandika kauili,
KAMA MNATAKA MALI, MTAYAPATA SHAMBANI.

..lilikuwa katika kitabu cha lugha cha darasa la nne. Mashairi mengine ni Tuipende Tanzana (Std VI) na Tausi [Ndege huyu ndege gani, hapa kwetu Tanzania] (Std. VII). darasa la tano hakuuwa na kitabu cha lugha. Sizitaki mbichi hizi ni shairi katika kitabu cha kusoma cha Std III kama nilivyosema awali. Usisahau kuwa nilikuwa kipanga enzi hizo ndio maana hata mashairi hayo husika yalibaki kichwani hata leo.
 
Back
Top Bottom