UKAWA kwenda kudai posho mahakamani

gimmy's

JF-Expert Member
Sep 22, 2011
3,305
3,327
Wabunge wa UKAWA waliositishiwa posho zao baada ya ule mchezo wa kutoka bungeni sasa kudai posho zao mahakamani.
image.jpeg

Hiii sijui imekaaje mtu kuhangaikia pato ambalo hujalifanyia kazi.
 
#JamboLEO Wabunge UKAWA kwenda mahakamani baada ya kunyimwa posho kutokana na kuingia bungeni kusaini kisha kutoka
image.jpeg

Nasoma kitabu cha darasa la nne 1997 SIZITAKI MBIVU HIZI.
 
Tutapata ufafanuzi soon

Alafu wale wa Bunge wa CCM waliopewa mpaka barua na chama kwa kutohudhuria vikao nao walinyimwa posho?
 
#JamboLEO Wabunge UKAWA kwenda mahakamani baada ya kunyimwa posho kutokana na kuingia bungeni kusaini kisha kutoka millard ayo on Twitter

Nasoma kitabu cha darasa la nne 1997 SIZITAKI MBIVU HIZI.
Darasa la NNE nchi gani mkuu hicho kitabu mwaka huo wa 1997?
Maana
Sizitaki mbivu hizi????;!!!!!!!
Kwanini ccm ni watupu sana kichwani jamani?
Ebu nisaidieni
Au edity fasta kabla magret thinkers hawajaja hapa
 
Wabunge wa UKAWA waliositishiwa posho zao baada ya ule mchezo wa kutoka bungeni sasa kudai posho zao mahakamani.
Hiii sijui imekaaje mtu kuhangaikia pato ambalo hujalifanyia kazi.
Source Star tv face book.
Wako sawa kabisa! Kuna kanuni/sheria inayosema usipohudhuria vikao vya bunge unanyimwa posho. Sheria ipi aliitumia Tulia kuwanyima posho? It makes sense , ni kuwa watu hatujui haki zetu. Ni sawa kama upuuzi anaoufanya Fastjet kuahirisha safari bila kuwa na alternative air transport or accommodation to the would be passengers! Only recently one advocate has approached the court to that effect and has won the case!
 
Kuna wachezaji mpira wao wapo bench tokea ligi inaanza mpaka inamaliza. Na wanapata mshahara na posho pia sasa kuna kosa gani kwa wabunge wa Ukawa kuidai haki yao? Mbona kuna wabunge wanachangia kuvuliwa kibarahashia tu na posho wanapewa.
 
inaelekea maamuzi ya kususia bunge walikuwa wanafata mkumbo, bunge limeisha na posho hakuna hii ni hatari kwani CCM wamshagundua madhaifu yao
 
Nilimsikia Mbowe kwenye habari akidai wao hawana shida na posho.

Au hii habari ni uzushi tu?
 
Ukawa
Wana haki ya kwenda mahakamani
Kwa kuwa walikuwa wanasaini mahudhurio
Kisha wanatoka
Malalamiko yao waliyafikisha kwenye kamati ya bunge kuwa hawana imani na naibu spika
Kwaio wanavigezo vyote vya kushinda kesi
hivi wewe ni mlipa kodi katika nchi hii kweli.? nina wasiwasi. utakuwa under age. hivi walipwe kwa kitu gani. si bora pesa hiyo ipelekwe kununulia madawati mashuleni au madawa hospitalini. ni nani aliwatuma wagome.? kuna yeyote alienda kwenye jimbo lake na kuomba watu wake kuwa anaenda kugoma bungeni na akakubaliwa. ni lazima tujue wabunge wameomba kazi kwa wananchi majimboni. wakapewa kazi na ni lazima waende bungeni kuwafanyia kazi. na sio kwenda kugoma kula na kulala tu. nani anagharamia muda huu uliopotea. tena ningeshauri hata mishahara yao ingekatwa kwa siku zilezote ambazo hawakufanya kazi.
 
Wabunge wa UKAWA waliositishiwa posho zao baada ya ule mchezo wa kutoka bungeni sasa kudai posho zao mahakamani.
Hiii sijui imekaaje mtu kuhangaikia pato ambalo hujalifanyia kazi.
Source Star tv face book.
HahHahaha kweli njaa haina baunsa! Hahaha kumbe hawa walikuwa wanapigania posho
 
Back
Top Bottom