UKAWA kuongea na wanahabari leo saa 8 mchana

UKAWA kuongea na wanahabari leo saa 8 mchana

Status
Not open for further replies.
Ccm kwisha waziri mkuu wa pili anakiacha chama chao

Hii mbona ilishasemwa sana tu humu! Mfumo ndio huo sasa wanaunda dola ya ukaskazini, na yote hiyo nadhani shida ilee inayoongelewa sana kuhusu mgombea wa ukawa.
 
Angalau nishajua kwanini hatujaanza kampeni........
Inaitwa nipige nikupige..... UKAWA oyeeeee
 
Hii mbona ilishasemwa sana tu humu! Mfumo ndio huo sasa wanaunda dola ya ukaskazini, na yote hiyo nadhani shida ilee inayoongelewa sana kuhusu mgombea wa ukawa.
Watu wanataka mabadiliko huu ndio mwisho wa ccm ccm ikikusanya wasanii ukawa wanakusanya mawaziri wakuu wastaafu na viongozi wa chama chao
 
UKAWA Wataitisha mkutano na wanabari leo saa 8 mchana na utarushwa live na ITV.

Habari za leo, uongozi wa Ukawa utakuwa na Mkutano na Wahariri leo saa 08:00 mchana Bahari Beach Hotel, kuzungumzia masuala makubwa kuhusu uchaguzi. Tafadhali fika bila kukosa.
=========

MBOWE: Ameomba pole kwa kuwashtukiza wanahabari kwa kuwapa taarifa ya ghafla, amemualika Sumaye na anamkaribisha aje kuzumza na wanahari.

Sumaye: Nimewaita juu ya mambo mawili makubwa, moja ni kutoa ufafanuzi juu ya taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa nimejitoa CCM na kuhamia UKAWA. Ile taarifa ilikuwa uongo, niliempa aikanushe alienda mbele zaidi na kusema Sumaye hatajitoa CCM maisha yote, la pili akasema Sumaye atazunguka na Magufuli nchi nzima kumnadi, hili nalo si sahihi. Bado namshukuru ndugu Lema kukanusha taarifa japo aliongezea mambo mawili matatu.

Nina raha Magufuli ndie mgombea kupitia CCM, ninaamini ni mchapakazi japo ana mapungufu yake mengi. Mimi nina tatizo na mfumo wetu au mfumo wao katika uchaguzi, kwa sababu kile chama cha mapinduzi ni cha zamani. Mimi kwa imani yangu na naamini imani ya wengi safari hii yametokea sana katika chama cha CCM. Ni vizuri tuige kwa wenzetu waliokomaa kidemokrasia, binafsi nilitarajia sitafika mbali katika mchakato huo. Tatizo la rushwa katika CCM, hili linathibitishwa na pesa nyingi zilizotumika wakati wa mchakato, watu waliwanunua wapiga kura


Mbona nyumbu wachache sana Leo???
 
Hizi habari kuwa amekuja kuchukua nafasi ya Lowassa ni kweli? Tuambieni wakuu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom