UKAWA inahitaji maombi, mapambano ni makali mno

UKAWA inahitaji maombi, mapambano ni makali mno

Iwe iwavyo nabaki niliko, sitotoka kwa sababu wanatoka na sihitaji wao pia watoke kwa sababu mimi sitoki...

njia ina mawaa miba na kero nyinginezo...

Sukani situkatikie safari ingaliko mbele.

uzuri wa mateso hauchagui kuwa huyu yumo au yule hayumo. wakiweka sheria mbovu waungeni mkono ili zitubane sisi, tukiisha zitawabana wenyewe msilie.
 
Nchi hii mpinzani wa kweli ni Mchungaji Mtikila peke yake,wengine wote wananunulika
 
Nadhani waafrika tunalo tatizo haiwezekani walewale waliosema kuwa haja ya kuungana nilazima kwa ushindi leo hii ni walewale ambao hawakubaliani (Pr. na Dr.) mnajitoa wakati hakuna muda wa kupoteza mimi naziogopa akili zetu.Hata hivyo waliobaki waendeleo kwa kuwa unakuwa na dhamira kisha unatenda na kutegemea matokeo yenye heri UKAWA vikwazo vitutie nguvu wapenda mabadiliko kwa ajili ya Taifa bora
Naogopa sana kuyarudia hayo maneno mkuu, ni maneno mazima na mazito, maneno ya maaba sana.

Nashindwa kuamini na huwa siamini kwamba pesa ni kila kitu. Naamini katika uhuru wa kifikra na maamuzi sahihi. Nitakuheshimu kwa kuwa muwazi na si mwenye kuficha jambo. Watu "wana washauri wao" wakishawashikia akili wanabadilika ghafla na kuona upande ambao hawakuwa. Namheshimu sana Pro. lakini katika hili sitomuamini tena hata kwa amana ya mate. Nikikumbuka ni yeye aliyepigwa mara kadhaa, ni yeye huyohuyo aliyefunguliwa kesi mara kadhaa hata sasa, ni yeye huyohuyo aliyeshiriki wazo la UKAWA. SIAMINI KUWA YEYE NI MMOJAWAPO ANAEIBOMOA UKAWA!!

WAKATI TUNAHIMIZA UMOJA KATIKA UPINZANI WAO WANAUDHOOFISHA KWA MAKUSUDI ILI UONEKANE KUWA UPUUZI.

IKIWA WALIOPIGANIA UHURU WALIKUWA WANANCHI WA KAWAIDA, TUSUBIRI MATOKEO.
 
Nchi hii mpinzani wa kweli ni Mchungaji Mtikila peke yake,wengine wote wananunulika

mkuu tena huyo ndio wa bei ndogo kuliko wote. aliwapigisha watu miaka ya 90 maandamano ya MAGABACHOLI walipokamatwa akawakimbia!!! Ndio ukawa mwanzo wake kufilisika kisiasa. MTIKILA NI KAMA KASUKU ALIE BANDANI AKIPIGA KELELE ZA KUTOLEWA, AKISHAPEWA KARANGA NA PILIPILI ANASAHAU KUWA YU BANDANI. KESI YA MGOMBEA BINAFSI ALISHINDA HALAFU...?
 
Viongozi wa ukawa ni mnanulika kwa bei gn? ili tuwauze kabisa tubaki na watu ambao hawauziki kabisa
 
Duh kati ya wapumbavu ww MALINYIKWE2 natumai ww miongoni mwao, unauliza tuko wp? Tuko huku UKAWA,wait result 25 oct
 
Wanachama,wafuasi,mashabiki,wafurukutwa na washangiliaji wa UKAWA mnapaswa kuwa pamoja muda huu. UKAWA uko kwenye mapambano makali na aombeeni viongozi wenu;watieni nguvu na kuwafariji. Muwatetee wanapodhihakiwa kwakuwa mapambano ambayo wanayo kuelekea Uchaguzi Mkuu ni magumu mno.Wanapita kwenye tanuru la moto. Waombeeni tafadhali.

UKAWA ukifika salama uchaguzini,mshukuruni Mungu. Viongozi wenu wanapigana kufa na kupona kuulinda Umoja wenu. Viongozi wenu wanashawishiwa na kutishiwa. Wanabezwa na kutwezwa. Wanapambana kweli kweli.

Tuliopo sentimita chache ya jiko la mikakati tunajionea. Wanavutwa mashati kwa masharti lakini wanasonga mbele hata yanapochanwa. Wako nanyi wakiwatetea, wakiwaunganisha

Kila la kheri UKAWA, komaeni tukutane Oktoba 25!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Mzee tupatupa wewe ni mtanzania halisi .hongera sana .unaonaje baada ya ukawa kuwa madarakani .ukajitambulisha rasmi .ili ikiwezekana ukatunukiwa zawadi ya the best underground activist. Of our time
 
Nimemsikia Prof Lipumba akisema malengo ya UKAWA ya kutetea Rasimu ya pili ya katiba yamekiukwa kwa kuwakubali walewale walioipinga (nadhani anamaanisha hawa wanaopokelewa toka CCM)

Hapa mimi sijmuelewa kwa sababu;

1. Ina maana anataka kutuambia wote walioko CCM waliipinga Rasimu ya Katiba ya Pili ya Jaji Warioba? Kweli??

2. Ina maana wote walioko UKAWA wanaikubali Rasimu ya Pili ya Katiba ya Jaji Warioba? Kweli??

3. Ana uhakika gani malengo ya UKAWA ya kutetea upatikanaji wa Katiba mpya msingi mkuu ukiwa ni Rasimu ya Pili ya Jaji Warioba kuwa yametupwa na wenzake? Kwani Ilani ya Uchaguzi ya UKAWA imetoka na kwa hiyo haitamki chochote juu ya hili? Au EL kawagomea na juu ya hili kwamba ataendeleza palepale alipoishia JMK?

Mimi sijamuelewa profesa kabisa!!
 
Ukiona Wazungu wanakufagilia sana lazima ujue kuwa unamaslahi kwao... Kumbe Lipumba ni one of EHM?... Kazi ipo ... Hawa wasomi wetu hawana chembe ya Uzalendo, yaani yeye Madini, Gasi kukwapuliwa bure bure hakumkeri bali anachekelea kwakuwa wazungu ndo beneficiaries .... Kweli mpambano ni mkali sana ...
 
Nyie vijana acheni kujificha kivulini kwenu. Mimi ni ukawa damu lakini sikukubaliana na upuuzi uliofanywa na viongozi wa ukawa wakiongozwa na Mbowe. Mimi nilichukua dhamana ya kuwaanfikia Lisu , Dr. Slaa, Heche na Mnyika lakini wote hawakunijibu nikiwauliza kama wako serious na wanaendelea na Ngoyai. Kama kawaida Lissu akaibuka kwenye media na sauti ya ukakamavu tunamkubali na Lowasa ndo atakuwa mgombea. Kisingizio eti tafiti za poll stars nyingi hali akijua juzi take tu alipinga ujio huo. Sijui hizi poll stars zilikuwa hazijaleta majibu? Hapa namkumbuka Prof. Kabudi MTU mjinga husikiliza lakini mpumbavu hushupaa. Mmeshupaa na Dr. Slaa na matusi mengi kwa Josephine leo ni Prof. Lipumba kesho itakuwa Lema. Najiuliza nyie ndo wale wa ukawa au wazanaki?
Kwako wewe kila aandikaye humu ni kijana? Ok tuache hilo, unafahamu kuwa Chadema ya sasa inaendeshwa kwa mbinu za kisiasa tofauti na miaka ya nyuma ilipokuwa inaendeshwa kiuana harakati?
Sasa nenda jifunze kwanza siasa zinaendeshwaje nchi zingine halafu njoo utafute tofauti ya Siasa na Harakati. Wakati ulimwengu unabadilika kila siku, huwezi kusimamia kauli yako moja hiyohiyo miaka kumi.
 
Hahahaa Lolote jema kutoka kwa Fisadi Lowasa ndiyo maana mnashindwa kwa sababu ya laana ktk kwa Mungu!
​

Uzuri Mungu sio binadamu,anasamehe yyt ataemuendea na kutubu!
So usihukumu usije ukahukumuwa!

Kashawaambia km mna ushahidi mpelekeni mahakamani maneno tupu hayasaidii
 
Hela ale Mbowe na Munkya sisi kazi yetu kuomba? Ataombewa na Gwajima
 
Back
Top Bottom