UKAWA inahitaji maombi, mapambano ni makali mno

UKAWA inahitaji maombi, mapambano ni makali mno

kijana wa ufipa katika ubora wake tena. vipi slaa kesharudi? nasikia amemuambukiza ugonwa wake le-profeseri,

Wanachama,wafuasi,mashabiki,wafurukutwa na washangiliaji wa UKAWA mnapaswa kuwa pamoja muda huu. UKAWA uko kwenye mapambano makali na aombeeni viongozi wenu;watieni nguvu na kuwafariji. Muwatetee wanapodhihakiwa kwakuwa mapambano ambayo wanayo kuelekea Uchaguzi Mkuu ni magumu mno.Wanapita kwenye tanuru la moto. Waombeeni tafadhali.

UKAWA ukifika salama uchaguzini,mshukuruni Mungu. Viongozi wenu wanapigana kufa na kupona kuulinda Umoja wenu. Viongozi wenu wanashawishiwa na kutishiwa. Wanabezwa na kutwezwa. Wanapambana kweli kweli.

Tuliopo sentimita chache ya jiko la mikakati tunajionea. Wanavutwa mashati kwa masharti lakini wanasonga mbele hata yanapochanwa. Wako nanyi wakiwatetea, wakiwaunganisha

Kila la kheri UKAWA, komaeni tukutane Oktoba 25!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
Nimekuelewa mzee VUTA-NIKUVUTE kwaio wameanza na Lipumba duu kweli Watanzania tunapenda rushwa. Mpaka dakika ya mwisho Lipumba Kaamua kupokea najua amepokea pesa ya uhakika ila ipo siku tutayapata na wananchi au watoto wetu watakaokuwepo kipindi icho watamuhukumu.

but Lipumba is a midioka...sijawahi kumpenda wala sijui kama in nthe future nitakaa nimpende
 
Umesema kweli mkuu wale wanaoishia njiani tutawaacha na wala hatutawalaumu. Ila Watz wanaelewa juu ya kinachofanyika. Ni mbinu ya kizamani kabisa. Sisi wapiga kura tupo imara na tutapigia kura mabadiliko.
 
Vita hii inaweza kuacha makovu, ni kweli lakini sisi tunasonga mbele!!!

Professa kapumzika, DR. kapumzika - sisi makamanda tuliobakia tunasonga mbele!! Mwenyezi Mungu akiwatia nguvu tutaungana nao mbele kwa mbele!!

Vita ni Kali - sisi tunasonga mbele - Alutaaaaaa...
 
Mbowe,mbatia,mzee makaidi na sefu hawa ni wapinzani haswaa na wanajua wamebeba roho za watanzania na wapenda mabadiliko hii ngoma ni ngumu ila ccm cha moto itakiona maana ukawa bado wamekaza walianza na slaa na sasa lipumba wamempata.UKAWA NI NGANGARI SANAA MCHEKI MAALIM KAKAZA BUTI LA UKAWA JUMA DUNI KASHINDILIA LIPUMBA CHALIII NA INAONEKANA ALIWASHAWISHI SANA WAKAMKATALIA
 
Kama kuna siku ya majonzi ni leo. Sikutegemea Prof. Lipumba ale n'gombe mzima lakini ashindwe kumalizia mkia!!

Huwezi jua!labda alikuwa naakula Kitimoto hajui!kuja oneshwa mkia na kwato ustadhi macho yakamtoka!Kaondoka bila kuaga Ukawa, kaja kuagia CUF.
 
UKAWA wanatakiwa kurudi mezani na kujipanga upya.
Wahakikishe Dr Slaa resumes office,vinginevyo ni ndoto.

Sio rahisi kama ulivyoiweka hapa, Ili slaa arudi kuwa katibu mkuu wa CDM, inabidi mengi yabadilike. Lowassa apewe kibuti na mgombea Uraisi ateuliwe yule waliyemchagua kabla Lowassa hajakatwa!!

Ni ngumu sana hayo kutokea.., Lowassa atazaa na mangi mbowe, kwani ameshakula vya kwake.., sasa vinamtokea puani. What mbowe did is exactly an example of dancing with the devil. Too sad his day of reckoning came earlier than he would have liked. It's all crumbling before his eyes, and there is nothing he can do since Lowassa has all the cards.., If CCM purposefuly orchestrated this Lowassa Safari ya matumaini theatrics just to get their perfect trojan horse, then they have done a masterful work.

As it goes now, Mk.we.re wa bagamoyo is getting a home run after a home run, it's becoming embarrassing.
 
Kama kuna siku ya majonzi ni leo. Sikutegemea Prof. Lipumba ale n'gombe mzima lakini ashindwe kumalizia mkia!!

Nadhani waafrika tunalo tatizo haiwezekani walewale waliosema kuwa haja ya kuungana nilazima kwa ushindi leo hii ni walewale ambao hawakubaliani (Pr. na Dr.) mnajitoa wakati hakuna muda wa kupoteza mimi naziogopa akili zetu.Hata hivyo waliobaki waendeleo kwa kuwa unakuwa na dhamira kisha unatenda na kutegemea matokeo yenye heri UKAWA vikwazo vitutie nguvu wapenda mabadiliko kwa ajili ya Taifa bora
 
Mbowe, Mbatia, Seif na Makaidi pls be strong hilo chama lina hila na hujuma nyingi
 
Mbowe lazima arudie matapishiyake...lazima ampigie magoti Dr Slaa..hakuna namna tena

Sina tatizo na DR.bali muda wa magoti haupo alikuwepo kwenye hatua zote na hakuna asilolijua hiyo uamuzi wake unaheshimiwa na lazima mambo yaende uzuri wa dunia haisimami.
 
Kama kuna siku ya majonzi ni leo. Sikutegemea Prof. Lipumba ale n'gombe mzima lakini ashindwe kumalizia mkia!!

Ktk viongoz wa upnzan binafsi nlikuwa sina iman na uyu kwan nwaka 2010 wakat slaa anagomea kusain kukubal matokeo akidai kura zimechakachuliwa uyu alimpnga slaa na kudai uchaguz ulikuwa huru na wa haki
Hata sababu aliyoitoa kwa mtu wa elimu yake haiendan kabusa
 
Siasa ni mchezo mchafu. Lakini mtu msomi anapokuwa ndumila kuwili hii sio uchafu ni kinyaa. Watanzania lazima wawajue viongozi wao na sio kuwaamini watu hao hao miaka nenda rudi bila mabadiliko yenye tija. Pesa siku zote inamtawala maskini illa huyo huyo maskini akisema sasa BASI amini kabisa ana nguvu kuliko silaha au chama chochote kile. Hadi hapo atakapomfungulia mola wake.
 
Wanachama,wafuasi,mashabiki,wafurukutwa na washangiliaji wa UKAWA mnapaswa kuwa pamoja muda huu. UKAWA uko kwenye mapambano makali na aombeeni viongozi wenu;watieni nguvu na kuwafariji. Muwatetee wanapodhihakiwa kwakuwa mapambano ambayo wanayo kuelekea Uchaguzi Mkuu ni magumu mno.Wanapita kwenye tanuru la moto. Waombeeni tafadhali.

UKAWA ukifika salama uchaguzini,mshukuruni Mungu. Viongozi wenu wanapigana kufa na kupona kuulinda Umoja wenu. Viongozi wenu wanashawishiwa na kutishiwa. Wanabezwa na kutwezwa. Wanapambana kweli kweli.

Tuliopo sentimita chache ya jiko la mikakati tunajionea. Wanavutwa mashati kwa masharti lakini wanasonga mbele hata yanapochanwa. Wako nanyi wakiwatetea, wakiwaunganisha

Kila la kheri UKAWA, komaeni tukutane Oktoba 25!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Ni kweli kabisa. Mapambano.ni makali. Awali haikutegemewa kuwa hali ingechafuka kiasi hiki. Mungu atusaidie tuvuke salama. Wakushinda washinde na wakushindwa wakubali.
 
Wametanguliza pesa na pesa hazitakaswi daima ..kwaheri Ukawa
 
Iwe iwavyo nabaki niliko, sitotoka kwa sababu wanatoka na sihitaji wao pia watoke kwa sababu mimi sitoki...

njia ina mawaa miba na kero nyinginezo...

Sukani situkatikie safari ingaliko mbele.

uzuri wa mateso hauchagui
 
Back
Top Bottom