VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,007
Wanachama,wafuasi,mashabiki,wafurukutwa na washangiliaji wa UKAWA mnapaswa kuwa pamoja muda huu. UKAWA uko kwenye mapambano makali na aombeeni viongozi wenu;watieni nguvu na kuwafariji. Muwatetee wanapodhihakiwa kwakuwa mapambano ambayo wanayo kuelekea Uchaguzi Mkuu ni magumu mno.Wanapita kwenye tanuru la moto. Waombeeni tafadhali.
UKAWA ukifika salama uchaguzini,mshukuruni Mungu. Viongozi wenu wanapigana kufa na kupona kuulinda Umoja wenu. Viongozi wenu wanashawishiwa na kutishiwa. Wanabezwa na kutwezwa. Wanapambana kweli kweli.
Tuliopo sentimita chache ya jiko la mikakati tunajionea. Wanavutwa mashati kwa masharti lakini wanasonga mbele hata yanapochanwa. Wako nanyi wakiwatetea, wakiwaunganisha
Kila la kheri UKAWA, komaeni tukutane Oktoba 25!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam