UKAWA, anzeni Mapema Kumwomba Mhe. Tundu Lissu Agombee Urais Mwaka 2020 | Page 2 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UKAWA, anzeni Mapema Kumwomba Mhe. Tundu Lissu Agombee Urais Mwaka 2020

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mchokoo, Oct 17, 2016.

 1. M

  Mchokoo JF-Expert Member

  #1
  Oct 17, 2016
  Joined: Jul 28, 2015
  Messages: 663
  Likes Received: 562
  Trophy Points: 180
  Wadau, nimewaza sana kuhusu nani anafaa kuipeperusha bendera ya UKAWA mwaka 2020 kwenye nafasi ile nyeti.
  Kwa upande wa CCM najua kuwa bado mheshimiwa John Pombe Magufuli ataendelea kugombea kulingana na utaratibu uliozoeleka.

  Hata hivyo changamoto kubwa bado inasaria kwenye vyama vinavyounda Ukawa! Ni yupi safari ijayo; anafaa kugombea urais kupitia wa vyama hivi?
  Hili ni swali moja kubwa mno, si kwao tu bali na kwa watanzania kwa ujumla.

  Swali ambalo kulingana na unyeti wake, linahitaji uwekevu wa hekima, au tuseme utulivu wa mawazo unaoweza kupalilia njia ya kuliendea jawabu, kinyume kabisa na ule utaratibu wa kukimbilia majibu mepesi; ambayo aghalabu huwa hayawezi kukidhi haja ya jamii yenye upevu wa kifikra.

  Pengine kabla sijaanza kuitetea hoja yangu; ni vizuri watawala wetu; katika nyakati zote, wakafahamu kwamba watanzania wa leo wanahitaji maisha bora tu, na si hadithi za alfulela-ulela.

  Sasa kwenye mada, kwa nini Tundu Antipas Lissu na si mwingine?

  1) Tundu Lissu ana uwezo mkubwa wa kujenga hoja mpaka mtoto mdogo akamwelewa!
  Ukizingatia kuwa nchi yetu kwa sasa uelewa wa watu si haba, na unazidi kuongezeka kila mwaka.

  2) Tundu Lissu ni Mwanasheria mwenye akili nyingi, na mtazamo mpana mno!
  Na kwa kutumia ufahamu wake huo atasaidia sana wakati wa kampeni kuongeza ushawishi pindi atakapogusa nyanja mbalimbali na kuja na majibu muafaka kwa jamii ambayo kimsingi imekuwa kama watazamaji tu ilihali sherehe ni yao!

  3) Tundu Lissu Hana kashfa yoyote ndani ya taifa hili.

  4) Tundu Lissu ni jasiri wa asili yake, ambae wakati wote huenda mbele tuu, na kamwe harudi nyuma katika lile analolisimamia.

  5) Ndiye Mwanasheria ambaye anaweza kutupatia katiba ya wananchi ambayo wanasiasa wengi wameonesha uoga kuitetea!

  6) Ni kijana pia, ambapo katika daftari la wapiga kura; wengi wao ni vijana.

  7) Tundu Lissu ana uwezo mkubwa wa kuhoji mambo yaliyopinda hivyo anawezakutoa changamoto kubwa kwa wale walio madarakani sasa.
  Sababu ziko nyingi mnaweza kuziongeza

  Na mwisho pengine niseme hivi labda nitaeleweka zaidi.

  Ukawa, au tuseme upinzani kwa ujumla, kutokumtumia mwanasheria huyu mbobevu katika eneo hili muhimu, hiyo haina tofauti kabisa na ile hadithi ya wale wazungu wa kale waliowakuta wasukuma wa Mwadui Shinyanga; wakicheza bao kwa kutumia vipande vya almasi kama kete!!

  Je wewe unasemaje kuhusu hili?
   
 2. k

  kipuyo JF-Expert Member

  #21
  Feb 17, 2017
  Joined: Jul 30, 2009
  Messages: 1,271
  Likes Received: 631
  Trophy Points: 280
  Viongozi karibu wote wanaotawala kwenye nchi karibu zote duniani(isipokuwa za kidikteta) huandaliwa na mifumo ya vyama vyao kuja kuongoza toka awali.
  Hata Tanzania,CCM ukiacha madhaifu yake ya hapa na pale wamekuwa wazuri kuwaandaa viongozi toka wakiwa wadogo mf Mkapa,Kikwete n.k
  Wapinzani bado hawajawa tayari kwa hilo.
  Wamekuwa watu wa kudaka watu wanaotemwa na waandaa viongozi.
  Imefika wakati sasa wa Upinzani kujipanga na kuweka mikakati ya muda mrefu ya ni nani atatufaa 2020,2025 ama kipindi chochote ambacho uchaguzi unaweza ukafanyika.
  Nikiangalia jinsi Tundu Lisu anavyowapa jamba jamba CCM katika uchaguzi wa TLS,basi unatambua kabisa huyu jamaa hata akigombea urais 2020 kupitia Ukawa atashinda kwa mbali sana.
  Hivyo niwape shime Chadema kumuandaa huyu jamaa ili agombee urais muda wowote uchaguzi ukitajwa.
  Kumuandaa ni pamoja na kumtengenezea personality n.k
   
 3. Gangongine

  Gangongine JF-Expert Member

  #22
  Feb 18, 2017
  Joined: Dec 31, 2015
  Messages: 3,866
  Likes Received: 1,756
  Trophy Points: 280
  Lowassa vipi mmeachana naye? Rais wa mioyo yenu!! Ahaaaaaaaaaaa!
   
 4. A

  AZUSA STREET JF-Expert Member

  #23
  Mar 18, 2017
  Joined: Oct 31, 2013
  Messages: 2,021
  Likes Received: 1,275
  Trophy Points: 280
  Kilichobaki kwa lisu sasaivi ni kugombea tu urais 2020, umeona jinsi watu walivyokupenda? unakubalika, serikali inakuogopa. tafadhali, umekabidhiwa imani kubwa na watz, fanya vyema ili 2020 upae kwenye anga zingine. Mungu ibariki TLS.
   
 5. osieee

  osieee Senior Member

  #24
  Mar 18, 2017
  Joined: Dec 16, 2015
  Messages: 148
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 45
  lissu anafaa ndio
   
 6. epigenetics

  epigenetics JF-Expert Member

  #25
  Apr 9, 2017
  Joined: May 25, 2008
  Messages: 262
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Interesting
   
 7. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #26
  Apr 9, 2017
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,331
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  He is not president type
   
 8. mop

  mop JF-Expert Member

  #27
  Apr 9, 2017
  Joined: Jul 11, 2015
  Messages: 863
  Likes Received: 605
  Trophy Points: 180
  Huyo si ni mwehu jamani,na yeye anafaa kuwa rais kweli?
   
 9. f

  future _1991 Member

  #28
  Apr 9, 2017
  Joined: Apr 7, 2017
  Messages: 7
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 5
  Lissu ni jembe
   
 10. super nova

  super nova JF-Expert Member

  #29
  Apr 9, 2017
  Joined: Aug 12, 2014
  Messages: 1,380
  Likes Received: 885
  Trophy Points: 280
  kwani antipasi ni jina la kichaga au wamasai??
   
 11. zitto junior

  zitto junior JF-Expert Member

  #30
  Apr 10, 2017
  Joined: Oct 7, 2013
  Messages: 8,924
  Likes Received: 7,954
  Trophy Points: 280
  ni lini chadema imerudia mgombea urais??
   
 12. zitto junior

  zitto junior JF-Expert Member

  #31
  Apr 10, 2017
  Joined: Oct 7, 2013
  Messages: 8,924
  Likes Received: 7,954
  Trophy Points: 280
  Hahhahhha ila magufuli ndio type ya urais?? hahhaah ccm bhana si mlisema ivo ivo urais wa TLS kilichofuata ni aibu kuu....... kiukweli mtu awe material au sio material hayamfanyi mtu kutokidhi vigezo zaidi ni kurekebishwa na kupewa mentorship za kiuiongozi basi mtu anakuwa fit coz i believe hakuna mtu aliyezaliwa akiwa kiongozi ila mazingira na mafunzo ndo yanawajenga kuwa viongozi.
   
 13. Gangongine

  Gangongine JF-Expert Member

  #32
  Apr 10, 2017
  Joined: Dec 31, 2015
  Messages: 3,866
  Likes Received: 1,756
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo 2020 hakuna kuzungusha mikono, kudeki barabara, kuigiza kunywa uji wa mama ntilie na kupanda daladala ya Gongolamboto? Kwa ubabaishaji wenu Ikulu mtaisikia kwenye Bomba miaka nenda rudi period!
   
 14. Mama Sabrina

  Mama Sabrina JF-Expert Member

  #33
  Apr 10, 2017
  Joined: Jul 30, 2016
  Messages: 12,286
  Likes Received: 17,934
  Trophy Points: 280
  Ni Kweli kabisa wamuweke Tundu lisu agombee 2020 maana ashazoea mikikimikiki ,Lowassa pumzika kabisa uwe mshaurii tu ,pia watu wengi wanamkubali Tundu Lisu,ila ingekuwa vyema vyama vya upinzani kwa uraisi wakaweka Raisi mmoja tu ili kura zisigawanyike wawe na umoja,,waweke kichwa Lissu ,hapo ntapiga kura
   
 15. Gangongine

  Gangongine JF-Expert Member

  #34
  Apr 10, 2017
  Joined: Dec 31, 2015
  Messages: 3,866
  Likes Received: 1,756
  Trophy Points: 280
  What? Lissu for Presidency? Ridiculous and ridiculousity!! A country is not a Law Society with less than 3000 members!
   
 16. Mama Sabrina

  Mama Sabrina JF-Expert Member

  #35
  Apr 10, 2017
  Joined: Jul 30, 2016
  Messages: 12,286
  Likes Received: 17,934
  Trophy Points: 280
  Mbona hadi vichaa wamekuwa raisi sembuse Lissu na akili zake timamu,wacha maneno
   
 17. nyanimzungu

  nyanimzungu JF-Expert Member

  #36
  Apr 10, 2017
  Joined: Mar 4, 2017
  Messages: 1,239
  Likes Received: 870
  Trophy Points: 280
  Lisu vs S. ally kessi 2020
   
 18. zitto junior

  zitto junior JF-Expert Member

  #37
  Apr 10, 2017
  Joined: Oct 7, 2013
  Messages: 8,924
  Likes Received: 7,954
  Trophy Points: 280
  hahhahhaah we jamaa mtu alipanda daladala kujua matatizo ya watanznaia wa chini kabida na siku anataka kurudi kuwashukuru mkamzuia mlitaka afanyeje ssa???
  kudeki barabara hayo ni mapenzi ya watu kma ambavyo juzi nape wamama walilala chini ssa kuna kosa gani watu wakikuonyesha heshima??? whether atasimama lowasa au lisu au mbatia au seif mziki ni ule ule na mtanyooshwa tu na nimnukuu humphrey polepole "UCHAGUZI UKIWA HURU NA HAKI CCM WANATOKA MADARAKANI"
   
 19. B

  Baba Kiki JF-Expert Member

  #38
  Apr 10, 2017
  Joined: May 31, 2012
  Messages: 1,425
  Likes Received: 545
  Trophy Points: 280
  Ifikie mahali tunapotaka kupata Rais wa nchi tuwe na vigezo au issues tunazotumia kumtambulisha nazo. Kuwa msemaji mzuri haipaswi kuwa mojawapo ya sifa kuu ila za ziada. Wakati mwingine tunaweza kujikuta tunaingiza watu wazuri kwa sura, au usemaji au umaarufu matokeo yake tunaugulia. Mtu yeyote anayetakiwa kugombea Urais lazima awe na;

  1. Sera nzuri na zinazotekelezeka za kiuchumi. Sera ambazo zinaweza kumwongezea kila mwananchi matumaini ya
  kufanikiwa kiuchumi. Asiyekurupuka kudandia vitu juu juu na kutuacha solemba
  2. Na hulka/silka/kipaji cha kiuongozi. Anayeweza kuliunganisha taifa bila kujali tofauti zetu na kutupatia uongozi wa
  kujivunia Utaifa wetu. Anayeweza kuhubiri umoja kwa maneno na matendo yake!
  3. Mtendaji, anayeweza kusimamia kile kilichoamuliwa na kutuonesha matokeo yake.
  4. Mnyenyekevu na mvumilivu. Hakuna kiongozi anayeweza kufanikisha matokeo makubwa na yanayodumu bila kuwa sifa za
  unyenyekevu ili ajifunze mengi na mvumilivu anapokosolewa.


  Kuwa mbishi pekee haitoshi, kuwa mbabe pia sio sifa. Kubobea katika fani yoyote iwe ni sheria, elimu, kemia, uchumi na. haitoshelezi. Tunatafuta mafanikio ya kiuchumi kwa wote, amani, demokrasia, mshikamano wa kijamii na kitaifa na mambo yanayofanana na hayo
   
 20. y

  yamungu joshua Member

  #39
  Apr 10, 2017
  Joined: Nov 17, 2016
  Messages: 29
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 5
  Kiukweli mutowa posti unabusara wazolako ni nzurisana
   
 21. honorto

  honorto Senior Member

  #40
  Apr 10, 2017
  Joined: Mar 27, 2017
  Messages: 190
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 45
  Kweli kabisa. Wanaopenda kuongozwa na marais vichaa watabisha!
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...