UKAWA, anzeni Mapema Kumwomba Mhe. Tundu Lissu Agombee Urais Mwaka 2020 | Page 3 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UKAWA, anzeni Mapema Kumwomba Mhe. Tundu Lissu Agombee Urais Mwaka 2020

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mchokoo, Oct 17, 2016.

 1. M

  Mchokoo JF-Expert Member

  #1
  Oct 17, 2016
  Joined: Jul 28, 2015
  Messages: 663
  Likes Received: 561
  Trophy Points: 180
  Wadau, nimewaza sana kuhusu nani anafaa kuipeperusha bendera ya UKAWA mwaka 2020 kwenye nafasi ile nyeti.
  Kwa upande wa CCM najua kuwa bado mheshimiwa John Pombe Magufuli ataendelea kugombea kulingana na utaratibu uliozoeleka.

  Hata hivyo changamoto kubwa bado inasaria kwenye vyama vinavyounda Ukawa! Ni yupi safari ijayo; anafaa kugombea urais kupitia wa vyama hivi?
  Hili ni swali moja kubwa mno, si kwao tu bali na kwa watanzania kwa ujumla.

  Swali ambalo kulingana na unyeti wake, linahitaji uwekevu wa hekima, au tuseme utulivu wa mawazo unaoweza kupalilia njia ya kuliendea jawabu, kinyume kabisa na ule utaratibu wa kukimbilia majibu mepesi; ambayo aghalabu huwa hayawezi kukidhi haja ya jamii yenye upevu wa kifikra.

  Pengine kabla sijaanza kuitetea hoja yangu; ni vizuri watawala wetu; katika nyakati zote, wakafahamu kwamba watanzania wa leo wanahitaji maisha bora tu, na si hadithi za alfulela-ulela.

  Sasa kwenye mada, kwa nini Tundu Antipas Lissu na si mwingine?

  1) Tundu Lissu ana uwezo mkubwa wa kujenga hoja mpaka mtoto mdogo akamwelewa!
  Ukizingatia kuwa nchi yetu kwa sasa uelewa wa watu si haba, na unazidi kuongezeka kila mwaka.

  2) Tundu Lissu ni Mwanasheria mwenye akili nyingi, na mtazamo mpana mno!
  Na kwa kutumia ufahamu wake huo atasaidia sana wakati wa kampeni kuongeza ushawishi pindi atakapogusa nyanja mbalimbali na kuja na majibu muafaka kwa jamii ambayo kimsingi imekuwa kama watazamaji tu ilihali sherehe ni yao!

  3) Tundu Lissu Hana kashfa yoyote ndani ya taifa hili.

  4) Tundu Lissu ni jasiri wa asili yake, ambae wakati wote huenda mbele tuu, na kamwe harudi nyuma katika lile analolisimamia.

  5) Ndiye Mwanasheria ambaye anaweza kutupatia katiba ya wananchi ambayo wanasiasa wengi wameonesha uoga kuitetea!

  6) Ni kijana pia, ambapo katika daftari la wapiga kura; wengi wao ni vijana.

  7) Tundu Lissu ana uwezo mkubwa wa kuhoji mambo yaliyopinda hivyo anawezakutoa changamoto kubwa kwa wale walio madarakani sasa.
  Sababu ziko nyingi mnaweza kuziongeza

  Na mwisho pengine niseme hivi labda nitaeleweka zaidi.

  Ukawa, au tuseme upinzani kwa ujumla, kutokumtumia mwanasheria huyu mbobevu katika eneo hili muhimu, hiyo haina tofauti kabisa na ile hadithi ya wale wazungu wa kale waliowakuta wasukuma wa Mwadui Shinyanga; wakicheza bao kwa kutumia vipande vya almasi kama kete!!

  Je wewe unasemaje kuhusu hili?
   
 2. SHAMMA

  SHAMMA JF-Expert Member

  #41
  Apr 10, 2017
  Joined: May 23, 2015
  Messages: 25,925
  Likes Received: 75,532
  Trophy Points: 280
  Lisu asigombee urais abaki kuwa mbunge ili kuichemsha serikali, aliwahi kusema akihojiwa na salama na kukiri kuwa anapendelea ubunge zaidi
   
 3. Gangongine

  Gangongine JF-Expert Member

  #42
  Apr 10, 2017
  Joined: Dec 31, 2015
  Messages: 3,866
  Likes Received: 1,756
  Trophy Points: 280
  MWAKA 2015 UKAWA WALISAFIRIA NYOTA YA LOWASSA AMBAYE ALIJIANDAA URAIS TANGU 1995. PIA MIGOGORO YA KUKATWA KWAKE ILISABABISHA UASI NDANI YA CCM NA KUMUONGEZEA KURA. HAKUKUWA NA SERA ZILIZOWAVUTIA WAPIGA KURA KUCHAGUA UKAWA BALI MTU. MWAKA 2020 MAZINGIRA HAYO HAYATAKUWEPO NA KWA VYOYOTE VILE KURA ZA UKIWA KAMA UTAKUWEPO HAZITAZIDI 2M TU. NA CCM 13M.
   
 4. Gangongine

  Gangongine JF-Expert Member

  #43
  Apr 10, 2017
  Joined: Dec 31, 2015
  Messages: 3,866
  Likes Received: 1,756
  Trophy Points: 280
  ISSUE NI KWAMBA HATOSHI KUWA RAIS.
   
 5. zitto junior

  zitto junior JF-Expert Member

  #44
  Apr 10, 2017
  Joined: Oct 7, 2013
  Messages: 8,443
  Likes Received: 7,183
  Trophy Points: 280
  hahhahhhha mkuuu hivi uchaguzi wa serikali za mitaa na vijiji UKAWA zile 40% umezisahau??? ukitoa yale mapimgamizi 5000!!!! au lowasa naye alikuwa UKAWA hyo 2014???? kaz kwelikweli........

  kma hatuna sera huyo mwenyekiti wenu asingekuwa na ubavu wa kuzima bunge au kufuta mikutano ya kisiasa!!!! ila anaogopa anajua M4C zikiruhusiwa tutaanika madudu yote ya bajeti iliyomshinda utekelezaji na jinsi elimu bure ilivyoua elimu!!! anaogopa ukosoaji saa nashangaa nyie mnaomtetea hunu hamuoni kma kuna haja ya kuwa na sera mbadala zaidi mnatamani ukawa ipate 2 milion votes!!! dah am speechless
   
 6. zitto junior

  zitto junior JF-Expert Member

  #45
  Apr 10, 2017
  Joined: Oct 7, 2013
  Messages: 8,443
  Likes Received: 7,183
  Trophy Points: 280
  Nani anayetosha??? huyo magu wenu ndio anatosha??? kwa lipi hasa kuua uchumi na elimu ama viwanda vya kwenye briefcase
   
 7. SHAMMA

  SHAMMA JF-Expert Member

  #46
  Apr 10, 2017
  Joined: May 23, 2015
  Messages: 25,925
  Likes Received: 75,532
  Trophy Points: 280
  Hakuna aliyewahi kutosha na kwasasa aliyepo sio tu hatoshi bali hafai
   
 8. Gangongine

  Gangongine JF-Expert Member

  #47
  Apr 10, 2017
  Joined: Dec 31, 2015
  Messages: 3,866
  Likes Received: 1,756
  Trophy Points: 280
  Wewe labda kama ni Mtutsi lakini kama una uraia wa Tanzania JPM ni Rais wako. Huyo sijui nani na mafigo yenu hajashinda Urais.
   
 9. Gangongine

  Gangongine JF-Expert Member

  #48
  Apr 10, 2017
  Joined: Dec 31, 2015
  Messages: 3,866
  Likes Received: 1,756
  Trophy Points: 280
  Mwisho utasema hata baba yako hatoshi
   
 10. SHAMMA

  SHAMMA JF-Expert Member

  #49
  Apr 10, 2017
  Joined: May 23, 2015
  Messages: 25,925
  Likes Received: 75,532
  Trophy Points: 280
  Tatizo lenu mmejitoa ufahamu kwa kila jambo mmebaki kusifia wanaume wenzenu tuuuu.
  Hamtaki wakosolewa
   
 11. 0752730816

  0752730816 Member

  #50
  Apr 10, 2017
  Joined: Mar 1, 2017
  Messages: 7
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  Ili ccm wamnunue mapema kama walivyofanya kwa slaa?
   
 12. zitto junior

  zitto junior JF-Expert Member

  #51
  Apr 10, 2017
  Joined: Oct 7, 2013
  Messages: 8,443
  Likes Received: 7,183
  Trophy Points: 280
  Acha ubaguzi wwe kwani Tanzania hatuna watutsi hapa?? wamejaa huko nyarubanda na manyovu afu wwe unaendekeza ubaguzi wa kiasili mxeeeeuuuu

  Back to topic kma unataka kujua ndo ujue leo ssa kua sijawahi mchagua magu na sitokaa nimchague mpaka naingia kaburini nilichokuuliza wwe ni kuwa unadai lisu sio material ya urais je magu ni rais material???
   
 13. Gangongine

  Gangongine JF-Expert Member

  #52
  Apr 10, 2017
  Joined: Dec 31, 2015
  Messages: 3,866
  Likes Received: 1,756
  Trophy Points: 280
  Hana heshima, adabu wala stara. Hata kama Kiongozi amekosea huwezi kumuita Kiongozi wa ovyo kwa kuwa Rais siyo Malaika kama ambavyo yeye akiwa Rais atafanya makosa mengi tu. Huwezi kumdhalilisha Rais wa Nchi hadharani inaonekana huna adabu. Mtu asiye na adabu anapewaje Urais wa Nchi?
   
 14. Nichumu Nibebike

  Nichumu Nibebike JF-Expert Member

  #53
  Apr 10, 2017
  Joined: Aug 28, 2016
  Messages: 7,794
  Likes Received: 13,133
  Trophy Points: 280
  Siyo kila mahiri wa kuongea ni mahiri wa kutenda pia! Mfano mzurui ni mama Anne Kilango!
   
 15. J

  Jos-lee Member

  #54
  Apr 10, 2017
  Joined: Mar 17, 2017
  Messages: 6
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 5
  Lowasa hana ishu TUNDU LISSU NDO ANAYEWEZAAAAAA
   
 16. Waterloo

  Waterloo JF-Expert Member

  #55
  Apr 10, 2017
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 12,940
  Likes Received: 13,349
  Trophy Points: 280
  Tuko pamoja kiongozi. Tundu Lissu
   
 17. zitto junior

  zitto junior JF-Expert Member

  #56
  Apr 10, 2017
  Joined: Oct 7, 2013
  Messages: 8,443
  Likes Received: 7,183
  Trophy Points: 280
  Si ndio maana nkasema hamna mtu aliyekamili hivyo udhaifu kila mtu anao lakini zinarekebishika mfano mwigulu nchemba wa 2012 mbona ni tofauti na huyu wa sasa hta natusi kapunguza hivyo naamini kma unamuona lisu anacharacter zisizokupendeza amini kuwa zinarekebishika!!! maana ukweli ni kwamba hakuna aliyezaliwa akiwa kiongozi ila wote wanakuwa shaped either kwa mafunzo au kwa uzoefu na mapito!!!!!

  so sioni shida kwa mleta mada kupropose Tundu Lisu 2020
   
 18. Countrywide

  Countrywide JF-Expert Member

  #57
  Sep 7, 2017
  Joined: Mar 2, 2015
  Messages: 2,750
  Likes Received: 2,218
  Trophy Points: 280
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...