UKAWA, anzeni Mapema Kumwomba Mhe. Tundu Lissu Agombee Urais Mwaka 2020 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UKAWA, anzeni Mapema Kumwomba Mhe. Tundu Lissu Agombee Urais Mwaka 2020

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mchokoo, Oct 17, 2016.

 1. M

  Mchokoo JF-Expert Member

  #1
  Oct 17, 2016
  Joined: Jul 28, 2015
  Messages: 663
  Likes Received: 561
  Trophy Points: 180
  Wadau, nimewaza sana kuhusu nani anafaa kuipeperusha bendera ya UKAWA mwaka 2020 kwenye nafasi ile nyeti.
  Kwa upande wa CCM najua kuwa bado mheshimiwa John Pombe Magufuli ataendelea kugombea kulingana na utaratibu uliozoeleka.

  Hata hivyo changamoto kubwa bado inasaria kwenye vyama vinavyounda Ukawa! Ni yupi safari ijayo; anafaa kugombea urais kupitia wa vyama hivi?
  Hili ni swali moja kubwa mno, si kwao tu bali na kwa watanzania kwa ujumla.

  Swali ambalo kulingana na unyeti wake, linahitaji uwekevu wa hekima, au tuseme utulivu wa mawazo unaoweza kupalilia njia ya kuliendea jawabu, kinyume kabisa na ule utaratibu wa kukimbilia majibu mepesi; ambayo aghalabu huwa hayawezi kukidhi haja ya jamii yenye upevu wa kifikra.

  Pengine kabla sijaanza kuitetea hoja yangu; ni vizuri watawala wetu; katika nyakati zote, wakafahamu kwamba watanzania wa leo wanahitaji maisha bora tu, na si hadithi za alfulela-ulela.

  Sasa kwenye mada, kwa nini Tundu Antipas Lissu na si mwingine?

  1) Tundu Lissu ana uwezo mkubwa wa kujenga hoja mpaka mtoto mdogo akamwelewa!
  Ukizingatia kuwa nchi yetu kwa sasa uelewa wa watu si haba, na unazidi kuongezeka kila mwaka.

  2) Tundu Lissu ni Mwanasheria mwenye akili nyingi, na mtazamo mpana mno!
  Na kwa kutumia ufahamu wake huo atasaidia sana wakati wa kampeni kuongeza ushawishi pindi atakapogusa nyanja mbalimbali na kuja na majibu muafaka kwa jamii ambayo kimsingi imekuwa kama watazamaji tu ilihali sherehe ni yao!

  3) Tundu Lissu Hana kashfa yoyote ndani ya taifa hili.

  4) Tundu Lissu ni jasiri wa asili yake, ambae wakati wote huenda mbele tuu, na kamwe harudi nyuma katika lile analolisimamia.

  5) Ndiye Mwanasheria ambaye anaweza kutupatia katiba ya wananchi ambayo wanasiasa wengi wameonesha uoga kuitetea!

  6) Ni kijana pia, ambapo katika daftari la wapiga kura; wengi wao ni vijana.

  7) Tundu Lissu ana uwezo mkubwa wa kuhoji mambo yaliyopinda hivyo anawezakutoa changamoto kubwa kwa wale walio madarakani sasa.
  Sababu ziko nyingi mnaweza kuziongeza

  Na mwisho pengine niseme hivi labda nitaeleweka zaidi.

  Ukawa, au tuseme upinzani kwa ujumla, kutokumtumia mwanasheria huyu mbobevu katika eneo hili muhimu, hiyo haina tofauti kabisa na ile hadithi ya wale wazungu wa kale waliowakuta wasukuma wa Mwadui Shinyanga; wakicheza bao kwa kutumia vipande vya almasi kama kete!!

  Je wewe unasemaje kuhusu hili?
   
 2. E

  Elimu ya hapa na pale JF-Expert Member

  #2
  Oct 17, 2016
  Joined: Aug 23, 2016
  Messages: 846
  Likes Received: 820
  Trophy Points: 180
  Mimi naona wampitishe mzee LEMBELI kwani ndiye anafaaa. Ukawa wanavifaa vingi sanaa
   
 3. Y

  Yaleyale JF-Expert Member

  #3
  Oct 17, 2016
  Joined: Aug 21, 2011
  Messages: 1,113
  Likes Received: 908
  Trophy Points: 280
  Tutamsubiri atakayekatwa ndo atagombea maana historia inaonesha wanakuwa asset kwa chama.
   
 4. Kisesa Yetu

  Kisesa Yetu JF-Expert Member

  #4
  Oct 17, 2016
  Joined: Aug 2, 2015
  Messages: 417
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 60
  Katika kila watanzania wanne, mmoja ni.....
   
 5. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #5
  Oct 17, 2016
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,996
  Likes Received: 3,320
  Trophy Points: 280
  Acha kumtaja mapema ... CCM wameshaliona hilo ndiyo maana wanampachika kesi ili apoteze sifa huko mbeleni kama watafanikiwa!!
   
 6. DEPETERO

  DEPETERO JF-Expert Member

  #6
  Oct 17, 2016
  Joined: Jul 29, 2016
  Messages: 820
  Likes Received: 560
  Trophy Points: 180
  Tuliza mshono
   
 7. elmagnifico

  elmagnifico JF-Expert Member

  #7
  Oct 17, 2016
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 7,908
  Likes Received: 7,505
  Trophy Points: 280
  Haaa hafai maana jamaa muongo sana
   
 8. Songambele

  Songambele JF-Expert Member

  #8
  Oct 17, 2016
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 3,548
  Likes Received: 1,106
  Trophy Points: 280
  Hata mwaka bado mnaanza kutafuta SUB ebu achene watu wafanye kazi, wagombea liwe swala la mwisho na tengenezeni vizazi vipya wapeni nafasi watu wenu wa excel mkianza kuweka masultan mtaendelea kuokota kwenye nyavu.
   
 9. orthogonal

  orthogonal Member

  #9
  Oct 17, 2016
  Joined: Aug 9, 2016
  Messages: 99
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 40
  Masaju na wabunge wa ccm lazima watafurahi kukosekana kwa Lissu bungeni.
   
 10. manchoso

  manchoso JF-Expert Member

  #10
  Oct 17, 2016
  Joined: Jul 27, 2011
  Messages: 907
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 180
  labda wampigie magoti kumuomba mzee
  sababu walishapiga hela sasa ujasiri wa kumkata hawana
   
 11. Upepo wa Pesa

  Upepo wa Pesa JF-Expert Member

  #11
  Oct 17, 2016
  Joined: Aug 8, 2015
  Messages: 10,242
  Likes Received: 11,811
  Trophy Points: 280
  Umeona mbali sana...nlisha pendekeza lissu angekua mwanasheria mkuu wa serikali
   
 12. H

  Hwasha JF-Expert Member

  #12
  Oct 18, 2016
  Joined: Aug 22, 2015
  Messages: 1,279
  Likes Received: 638
  Trophy Points: 280
  Mgombea aliyeleta "kula" nyingi kasema hagombei tena? msinitukane nauliza tu maana nilifundishwa kuwa aulizaye ataka kujua.
   
 13. Jitu Refu

  Jitu Refu JF-Expert Member

  #13
  Oct 18, 2016
  Joined: Sep 9, 2016
  Messages: 830
  Likes Received: 752
  Trophy Points: 180
  Wamchukue rungwe
   
 14. Mudawote

  Mudawote JF-Expert Member

  #14
  Oct 18, 2016
  Joined: Jul 10, 2013
  Messages: 5,522
  Likes Received: 4,042
  Trophy Points: 280
  Kweli injini imenokishwa na oili chafu. Poleni sana wadau. Sisi huku CCM ni hili jembe letu Dkt Magufuli usiku na mchana wala hatuwazi. Ila wasi wasi wangu Tundu Lisu hana bil 10.
   
 15. ketete

  ketete JF-Expert Member

  #15
  Oct 18, 2016
  Joined: Sep 22, 2016
  Messages: 637
  Likes Received: 557
  Trophy Points: 180
  lisu ndiye jembe la taifa
   
 16. SHIMBA YA BUYENZE

  SHIMBA YA BUYENZE JF-Expert Member

  #16
  Oct 18, 2016
  Joined: Dec 22, 2014
  Messages: 63,000
  Likes Received: 322,609
  Trophy Points: 280
  Nyeti za kuku. Thubutuuuu!
   
 17. n

  neemajames Member

  #17
  Oct 18, 2016
  Joined: Oct 13, 2016
  Messages: 25
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 5
  Tutamnunua Prof Lipumba......
   
 18. Izc

  Izc JF-Expert Member

  #18
  Oct 25, 2016
  Joined: Aug 4, 2015
  Messages: 543
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 80
  Pia itakuwa ni kumwandaa kwa ajiri ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
   
 19. l

  lipoprotein Member

  #19
  Oct 27, 2016
  Joined: Oct 4, 2016
  Messages: 51
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 25
  Acha kuchekesha wewe yaani tundu lisu apambane na jemedari magufuri, mapema sana! Mtaanza kulalama oooh kura zimeibiwa
   
 20. M

  Mgango JF-Expert Member

  #20
  Nov 14, 2016
  Joined: Oct 27, 2016
  Messages: 2,349
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  Wewe nani? Ya ngoswe mwachie mwenyewe
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...