Ukatili wa Kingono kwa Watoto, Serikali na Jamii inawajibika

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
Ukatili wa kingono dhidi ya watoto huhusisha ubakaji, ulawiti, utekaji na usafirishaji wa watoto kwa ajili ya ngono, kumshika mtoto via vya uzazi ikiwa ni pamoja na uke, uume na matiti, uoneshaji video za ngono kwa watoto

Miaka ya karibuni visa vya Ukatili wa Kingono kwa Watoto vinazidi kuongezeka kwa kasi kubwa sana mpaka inaogopesha. Kwa mujibu wa ripoti ya LHRC (2020) "Kwa kipindi cha miaka 5 matukio ya ukatili wa kingono, ubakaji na ulawiti dhidi ya watoto yamekuwa yakiongezeka. Tangu mwaka 2015 hadi 2019 jumla ya makosa 36,940 ya ubakaji na ulawiti yaliripotiwa katika Vituo vya Polisi.

Kwa kuangalia hizo takwimu tunaweza kujiridhisha kuwa vitendo hivi vya ukatili wa kingono kwa watoto vinazidi kushamiri kadri miaka inavyosonga hivyo Jamii na Serikali inawajibika kukemea na kuchukua hatua stahiki kukomesha vitendo vya Ukatili Wa Kingono

Madhara makubwa anayopata Mtoto aliyetendewa ukatili wa kingono mara nyingi hukosa amani na furaha, husononeka, kukosa kujiamini na kujithamini.

Jamii na Serikali ifanye nini?

Serikali inatakiwa Kubadilisha mitazamo ya wanajamii waone ukatili wa kingono ni kosa la Jinai na sio jambo la aibu. Mara nyingi jamii nyingi hasa vijijini zimekuwa zikichukulia kuwa unyanyasaji wa kingono kwa watoto hasa unapotokea kwenye familia fulani, hufanya juu chini kulizima kimya kimya kwa kuhisi kuwa likisambaa basi itakuwa aibu kwa familia hasa aliyetenda kosa hilo bila kujali limemuathiri vipi mtendwa ambaye ni mtoto. Tumeona katika ripoti mbalimbali kuwa asilimia kubwa ya watoto wanaofanyiwa vitendo vya ukatili wa kingono basi wanakuwa wamefanyiwa na watu wao wa karibu.

Jamii iepuke kumaliza kesi nje ya vyombo vya sheria. Hili nalo ni tatizo sugu baina ya jamii. Kesi nyingi zimekuwa zikimalizwa ndani ya familia kwa kutoa fidia au vinginevyo na hata nyingine ziliporipotiwa katika vituo vya Polisi, maafisa wasio waaminifu wamekuwa wakitengeneza mazingira ya rushwa na kupoteza/kutopeleka kesi katika ngazi ya Mahakama. Hii imekuwa ikipelekea wanaotenda ukatili huo kurudia mara kwa mara wakijua kuwa wanaweza kumaliza msala katika ngazi za familia au hata Polisi.

Teknolojia sasa inakuwa kwa kasi, maudhui mitandaoni nayo yanaongezeka kwa kasi. Sasa hapa kama mzazi unatakiwa kudhibiti maudhui ambayo mtoto anatakiwa kufuatilia kwenye Intaneti na kwenye luninga. Hakikisha maudhui mtoto anayoangalia ni ya umri wake, luninga nyingine hasa za nje zimekuwa zikiweka maudhui ya watoto yenye viashiria vya Mapenzi ya Jinsia moja hivyo kama mzazi unatakiwa kuwa makini sana kufuatilia maudhui anayaoangalia mwanao. Mfano watoto wengine wanapenda katuni na animation movies, lakini nyingine zinakuwa na utamaduni wa kizungu ambazo watoto wa nchini hawapaswi kuona wala kujifunza. Hatari ya ushoga kwa watoto wa Tanzania; Serikali itunge Sheria kuzuia vikaragosi vya Superman

Epuka mtoto kulala na mgeni au watu wengine waliomzidi umri. Ni fika familia nyingi za kiafrika tunaishi kwa mfumo wa extended family huku mazingira ya kuishi asilimia kubwa hayakidhi kutoa malazi kwa idadi ya wanafamilia hivyo kujikuta kunalazimisha ku-share vyumba kupita uwezo. Inapotokea hivi waepushe watoto kulala na watu waliowazidi umri hasa wageni. Kumbuka vitendo vingi vya ukatili wa kingono kwa watoto hufanywa na watu wa karibu, NASEMA USIMWAMINI MTU YEYOTE, dunia imekwisha

Fuatilia mwenendo wa mtoto wako na ongea naye mambo mtambuka na ikibidi kumkagua mara kwa mara.Kufuatilia mwenendo wake inajumuisha na marafiki anaocheza nao lazima kujiridhisha, kama anasoma masomo ya Dini pia unafuatilia maana walimu wa dini siku hizi hawaaminiki kabisa. Rejea Mmiliki wa Madrasa adaiwa kulawiti wanafunzi 22

Nipende kusema kuwa Wazazi, Serikali na Jamii kwa ujumla inawajibika sana kulinda haki za watoto wote, haijalishi wa kumzaa au lah ili tuweze kupunguza ukatili mkubwa kwa watoto wetu ambao unashamiri kila uchao. Mimi ukimfanyia mwanangu vitendo vya unyanyasaji wa kingono nikajiridhisha na mamlaka ikashindwa kutenda haki basi jua nikikubahatisha tutagawana majengo ya serikali mimi niende jela wewe uende mochwari
 
Wakati hatari inasogea zaidi ndiyo muda ambao ulinzi unatoweka
Hapa kinachotokea ni uwezekano wa kupata maumivu kuwa mkubwa sana. Uhuru umekuwa mkubwa sana kwa watoto wazazi wamewekeza kwenye shughuli mbalimbalii, ndiyo sababu vituo vyakutoa malezi wa watoto wadogo vimekuwa vingi
 
Wanayotenda hivi vitendo ni wakati sasa wa kumalizana nao kama VIBAKA and the likes.....
 
Back
Top Bottom