Ukaguzi wa vyeti feki Serikalini umeanza rasmi, waanza na Walimu

Hivi JK ana degree ngapi vile... nauliza tu najua kastaafu..

Muhongo anarudia std 7 mara 3...

Kigwangala aliiba eti jina la Mtoto wa mtu akiwa std 7 kuingia Sec, sio jina lake kamili...

Vipi, Dr. Mwaka...!!?
 
Walimu hukaguliwa vyeti kabla ya kufanya mtihani wa taifa wa ualimu,na zoezi hili hufanyika mara kwa mara wawapo kazini,sasa huu ukaguzi unahusu kina nani?
 
Wangeambiwa wapeleke vyeti vya chuoni na vya kuzaliwa wafananishe hatari cha kuzaliwa kimeandikwa zubeda cha chuon kimeandikwa mwafilombe kwikwi
 
Hilo nalo jipu. Mamluki kibao wameajiria bila sifa na ndio maana madudu na utendaji chini ya kiwango vimetawala
 
tunae mwalimu jipu hapa shule ya msingi msanga wilaya ya chamwino karibu kabisa na ikulu ndogo ya chamwino dodoma jina lake halisi ni prisca nyonyo alikuwa nyuma yangu kimadarasa anatumia cheti cha dada yake anaitwa stella nyonyo kwahiyo kwa sasa anaitwa stella nyonyo, stella nyonyo origino ni mtumishi pale manisipaa dodoma ni nesi. kazi kwako mr kaponda afisa elimu mkoa wa dodoma.

haaaaaaaaaaaaa,huogopi juju mkuu?,majipu mengine hayajaivaaaaaaaa
 
JwTZ kitakachowasaidia ni ile sheria yao kuwa ukimaliza tu depo regardless education level ndo umesha win na kama unakumbuka vizuri nafasi nyingi za TPDF miaka ya nyuma ni darasa la saba na form four mostly failures

Ikiwa issue ni forgery katika vyeti, sidhanii kama TPDF watakuwa exceptional, kwani hata huyo darasa la saba anaweza vile vile akawa ame-forge cheti, na hata form aliofeli nae anaweza akawa ali-forge cheti vile vile.
Otherwise kuwe na some sort of substandards.
 
kuna majipu yapo idara ya AFYA Daaaaaa ninaofahamu tu ni zaidi ya kumi shidaaaaa
 
Katika kuhakikisha wafanyakazi wa Serikali ni wale wenye sifa stahiki, Serikali imeanza ukaguzi wa vyeti ili kuhakiki kama ni vyeti ambavyo sio feki.

Baadhi ya mikoa walimu wametakiwa kuwasilisha vyeti vyao kwa uhakiki.

Baada ya walimu wataofuata ni Halmashauri zote nchini kwa kuwa fedha nyingi za maendeleo hupelekwa huko.

Connect Dots fedha za Elimu kupelekwa moja kwa moja kwa wakuu wa shule.

Acha kuongopea watu..mkoa gani wameambiwa ivo??wakati unapoajiriwa unapeleka vyeti original vinaskaniwa.....mlidanganya jeshi la polis limefukuza watu kutokana na vyeti feki kumbe waongo..mkatoa na majina sasa wanawatafuta
 
Tegemeeni watu wengi kupoteza uhai kwa kiharusi. Tena nawashauri wahakiki vyeti vyote kuanzia sekondari yaani form four hadi vyuo. Tunaweza kushangaa asilimia 75 wana vya magumashi.

Inatakiwa zoezi lianze na ukaguzi wa kadi za clinic, vyeti vya kuzaliwa, sambamba na vyeti vya kitaaluma, hii itasaidia pia kukamata mamluki na raia wa kigenj waliojiingiza serikalini.
 
Ukweli ni kuwa taasisi zilizojaa watu wenye vyeti feki au kutumia vyeti vya ndigu, marafiki au vya kununua ni polisi na ualimu. Msako mkali ufanyike kuhakiki vyeti na uhalisia wa mmiliki. Kuwagundua ni rahisi sana. Ukimuuliza hiyo shule aliyuomaliza kidato cha nne mfano iko wapi, mkuu wa shule alikuwa nani, mwalimu wake wa kiingereza alikuwa nani na maswali ya jumla kuhusu uelewa wake wa kile kilichoandikwa, wengi watagundulika.
 
Back
Top Bottom