'Ukabila' nilioahidi kuuanza baada ya 9 Disemba 2011: Naanza kubeep!

ndyoko

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,971
1,650
Sijui ni makusudi au bahati mbaya au coincidence. Ufukunyuku wa muda mfupi niloufanya nimegundua jambo hili limeanza kufanyika kwa kasi ya ajabu sana na baada ya muda kuna uwezekano yale majina ya familia yenye asili ya kibantu yatapotea kabisa na kubaki na yale ya kimagharibi mfano Stephen, McDonald, Clinton, Wycliff n.k.

Jamii na koo nyingi sasa zimeanza kuachana kabisa na majina yao ya kiasili kama Jilala, Kifurugobe, Matata, Kasenene, Mkude. Mfutakamba. Bado sijajua sababu hasa ni nini watu wanaona kuendelea kutumia majina yao ya ukoo ya kiafrika na ya asili. Najua mko mtakao bisha lakini ukweli unabaki pale pale kwamba hili linatokea kwa kasi ktk jamii ya baadhi ya makabila hapa TZ.

Majina ya watu tuliyoyazoea kama Janeth Kamugisha, Catherine Massawe, Juieth Munisi, James Hawala, Edson Karumekenge, Kelvin Limbwata yameanza kupotea na tunaanza kuona yanapotea kwa kasi sana, sasa watu wanajiita Janeth Clinton, Catherine McDonald, Eveline Stephen, Juieth Williams, yaani ki westeni zaidi kuliko kiafrika. Mbaya zaidi linapokuja suala la kuomba kazi maofisini hapo ndo utashangaa majina ya ukoo ya kibantu ndo hutayaona kabisaaaaaaa, ila mtu akipata kazi tu, ndo anaanza kulazimisha sasa ofisi ilitambue rasmi jina lake la ukoo lenye lafudhi ya kiafrika.

Kama haujui basi nakupa 'hint' kwamba kwa sasa bogo kuna makabila mawili hapa Bongo ambayo kwayo tabia hii miongoni mwa watu wake yanaongoza kwa kuficha majina yao ya ukoo ya kiafrika, lakini huyafufua na kutaka yatumike rasmi pindi wanapopata ajira.

Nakaribisha critics na maoni yenu!

'Buriani'!
 
dunia imebadilika watu wamehamia mijini, watoto wanasoma shule za academy hatakubali kuitwa joseph mkosamali stanford atapenda kuitwa joseph m. Stanford, wanawake wanaolewa wanaitwa mrs john hataitwa tena kokushubirwa. Nashut down
 
kitu gani kinamfanya awe na hizo hisia za 'hatokubali' ndo shida yangu mie, what is the motivation behind such a behaviour? nielimishe please!
 
Ukabila unarudi kwa nguvu kubwa nchini. ni afadhali usiegemeze kwa jina la kabila yoyote ili hata kwenye interview huweze kupita. kama DG ni Mbonde Kamugisha hawezi kupata kazi. Ndio maana wapenda majina ambayo ni neutral kukwepa ubaguzi huo.
 
Nalipenda jina langu Kadakabikile ambalo ni la asili sio la kipumbavu kutoka ulaya.
 
Ukabila unarudi kwa nguvu kubwa nchini. ni afadhali usiegemeze kwa jina la kabila yoyote ili hata kwenye interview huweze kupita. kama DG ni Mbonde Kamugisha hawezi kupata kazi. Ndio maana wapenda majina ambayo ni neutral kukwepa ubaguzi huo.

so unaniambia kuwa moja ya sababu watu kuficha majina ya asili ni ukabila. tuanenda wapi wabongo?
 
Pana ukweli humo, lakini hata hivyo nani anaweza kujua asili ya jina langu Aweda?
 
Bora na mtu kuwa na jina la kigeni kabisa kuliko yule anayelibadilisha la kwake kwa kulitia nakshi za kipuuzi. Hawa ndio vichefuchefu kabisa wasiojiamini na wamejidharau kwa kuwa sio wazungu:
Moshi = Moshy (chaga)
Kesi = Kessy (chaga)
Urio = Urioh
Kassim = Cassim
Khamisi = Khammisy
Amina = Amyna
Mohammed = Mohamedy
Khadija = Haddijah

x*y.!,.*zq' zenu. Kama jina lako ni Mangesho andika tu Mangesho na sio Mangeshow, pambaf

Siku moja nilikutana na mpambaf mmoja pale TTCL kapaka lip-stick ya silver kwenye mamidomo yake myeusi kama kunguru, basi kawa kama kituko. Namwambia jina langu Noremi, mwenyewe kwa ujuha wake akaandika Noremy, nikamwambia FUTA HARAKA!
 
mkuu ban inakunyemelea and very soon you will add to the list.
 
Cheki watu wanavyopenda kubadilisha majina kufuata uzungu
Chausiku-Chanight
Jumanne-Tuesday
Tumaini-Hope
Furaha-Happyness
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom