UK-Africa Investment Summit 2020: Where is top level Tanzania representative?

Kwa hiyo kwa mpango huu mtaacha kusikia njaa sana
 
Lugha ya kitaa hiyo mzee...huko kwenu haipo au kama nimekosea nisahihishe basi.

Sasa mbona hiyo lugha ya kitaa uijue wewe tu, yaani hata Watanzania wenzio hawaifahamu, lugha za mtaani zipo kote hata huku.
 
Kwa hiyo kwa mpango huu mtaacha kusikia njaa sana
Tunakuja kwa 'lesi' moja ya ajab. Kando na dili za KES 170Billion kwenye summit ya UK-Africa Invest. kuna hii biashara nyingine ya kando. Rais Uhuru alifungua rasmi shughuli za LSE.
images
Akazindua rasmi pia float ya green bond ya kwanza kutoka Kenya, yenye thamani ya $40Million! Corporate green bond kutoka kwa kampuni ya kikenya ambayo itakuwa 'denominated' kwa KES. Tegemea kuona kampuni zingine za Kenya zikichangamkia fursa kama hiyo ya kutanua misuli hadi UK na kuvutia wawekezaji. Tena chini ya muongozo wa serikali ya Kenya.
 
Waliswagwa kwenda UCHINA, baadae URUSI na sasa ENGLAND. Hivi hawa akili zao timamu kweli?Next wataswagwa kwenda UTURUKI.
Zama zile ile tuliosema ni ukoloni mamboleo siyo tena. Ni mahaba nje nje kwa MABEBERU

UPUUZI huo! Nafurahi hatumo
 
Ni Marais 14 wa nchi za Africa ndo wamehudhulia wengine hawakuhudhulia,Kwahiyo sio Tanzania peke yake

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hakuna miradi hapo, wameenda kupewa maelekezo magumu ya mashariti hayo na mabwanyenye.
Just imagie nchi 54,marais waliohudhuria ni 16 tu.
Tanzania imewakilishwa na Balozi wa hukohuko UK.
Enzi za ujumbe wa kusombana na vimwana wenu mkidai ni watumishi wa idara husika umekwisha
Nchi 21 za Afrika zimehudhuria
 
Kama huamini Tanzania ni tajiri kwa resources ilizonazo ardhini wewe ni pumbavu mkubwa sana.
Tatizo la Tanzania sio umaskini bali namna bora ya Ku- exploit raslimali hizo toka ardhini na kuzitumia sahihi kwa maslahi ya watanzania wote ,ikiwemo na kuzichakata, pasi kujali,jinsia,dini,rangi ya mtu.

Viongozi wetu wakillitambua hili na wakaacha ubinafsi taifa litapaa sana.

Komenti za ajabu sana hizi.

Kwani ni lazima kuchagua upande?

Matokeo ya haya yanayofanywa na serikali ya awamu hii bila shaka tutayajutia hapo baadae tukishayaona matokeo yake ambayo hayapo sasa hivi, na watu wala hawajishughulishi kuzitambua athari zitakazotukabili, na hata bila kujishughulisha hata kuzichambua tu tuzijue.

Sisi tumekomalia kuwa ni matajiri, na wengine wote wanatafuta tu kuja kutuibia utajiri wetu. Na bado watu na akili zao wanaamini mambo kama haya.

Nchi haikatazwi kulinda mali zake, lakini nyakati hizi sio za kujitenga na dunia.

Hapo namwona Rwanda, Uganda, Kenya..., wote washirika wetu kwenye jumuia yetu ya Afrika Mashariki. Sisi tutakuwa soko la hawa wenzetu bila ya ubishi.

Hata tukiamua kuwa na TanzaExit yetu hatutafua dafu, tutakwenda wapi! SADC nako hapatatosha na huko AfCFTA tutauziwa tu na hawa wenzetu wanaojenga misingi ya uwekezaji imara katika wakati 'critical' kama huu.

BTW: Hivi 2019 tumepata FDI kiasi gani? Hata kutaja tu siku hizi inakuwa ni aibu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sisi tuna vipaumbele vyetu, kwanza sisi ni nchi tajiri, a donor country. Mikutano kama hii yenye kufanya maamuzi makubwa ya kibiashara si muhimu sana kwetu
 
Sio kila summit ina maslahi kwa nchi
Baadae watasainishwa mkataba utakaotaka bidhaa za uingereza ziingie bila kulipa kodi
Msimfanye mkoloni hana akili
 
Baada ya mkutano na China majaliwa alisaini mkataba wa kuingiza bidhaa za china bure nchini.Watu wenye akili finyu ndio wanaoongoza nchi how comes nchi ikadevelop?
Kabombe use your critical thinking bro.
Sio kila summit ina maslahi kwa nchi
Baadae watasainishwa mkataba utakaotaka bidhaa za uingereza ziingie bila kulipa kodi
Msimfanye mkoloni hana akili
 
Tunakuja kwa 'lesi' moja ya ajab. Kando na dili za KES 170Billion kwenye summit ya UK-Africa Invest. kuna hii biashara nyingine ya kando. Rais Uhuru alifungua rasmi shughuli za LSE.
images
Akazindua rasmi pia float ya green bond ya kwanza kutoka Kenya, yenye thamani ya $40Million! Corporate green bond kutoka kwa kampuni ya kikenya ambayo itakuwa 'denominated' kwa KES. Tegemea kuona kampuni zingine za Kenya zikichangamkia fursa kama hiyo ya kutanua misuli hadi UK na kuvutia wawekezaji. Tena chini ya muongozo wa serikali ya Kenya.
Sawa vizuri..... Nasubir hizo positive results.
 
Back
Top Bottom