UK-Africa Investment Summit 2020: Where is top level Tanzania representative?

Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
11,069
2,000
Sisi hatutajuta kwa kuwa tunajua serikali inafanya nini.UK wanatuhitaji kuliko tunavyowahitaji. Kaa kimya

Eleza "unachojua serikali inafanya nini".

Hukuandika chochote cha kunifanya 'nikae kimya' katika mstari huo ulioweka hapo. Kwa hiyo nachukulia kuwa wewe ni kati ya wajinga na wapumbavu niliowazoea hapa JF.

UK haina haja ya "kuwahitahi" nyinyi kwa lolote inalolitaka kutoka kwenu na isilipate. Koloni lake lipo hapo mnashirikiana nalo. Kuna ugumu gani wa kulitumia koloni hilo ili ipate inachokitaka kutoka kwenu.

Kwanza kuonyesha ulivyo mjinga, hata huelewi yanayoendelea kwenye mkutano huo.

Bure kabisa.
 

Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
11,069
2,000
Rwanda inaishinda URT maeneo yapi haswa au ndiyo kazi zenu za kutumika kama toilet paper
Wewe kweli ni kiazi.

Unataka uelezwe Rwanda inaishinda kitu gani Tanzania leo; huna habari kwamba Rwanda anajenga leo kuishinda Tanzania kesho na keshokutwa?
Haya, ngoja nikupe mfano mmoja: uchumi wa Rwanda unakua kwa kasi zaidi ya huo wa Tanzania kwa sasa, na ndio maana Kagame yupo huko kutafuta fursa zaidi ili uchumi wake uzidi kukua kwa kasi.
Au unasubiri mpaka uambiwe kwamba GDP ya Rwanda ni kubwa zaidi ya Tanzania, jambo ambalo haliwezekani kwa sasa katika mlinganisho? Rwanda pamoja na GDP yake ikiwa ndogo, maisha ya wananchi wake yatakuwa mazuri zaidi ya yako; bado hujui maana yake ni nini?
 

MkamaP

JF-Expert Member
Jan 27, 2007
7,989
2,000
Kwanini uwe huna cha ku export?
Kukosa cha ku export maana yake ni:-

1. Huna maliasili (malighafi)
2. Huna akili
3. Huna vyote viwili hapo juu.

Maliasili ni ya hadi ikupleke huko? watakuja tu wenyewe kuitafuta.
 

Mackanackyyy

JF-Expert Member
Mar 26, 2019
2,348
2,000
Nchi 21 za Afrika zimehudhuria

Wawakilishi zaid ya 1500

Miradi ya jumla ya Pauni Bil 6.5 imetangazwa.

Je hatutaki fursa hii na sisi wanachama wa jumuia ya madola? Baada ya Brexit mwezi huu kuna fursa kubwa za biashara na waingereza. Au ni bora inatosha kufanya biashara na wachina tu? Deal kama hizi rais wa nchi anatakiwa awepo kwenye meza ili na Tanzania ipate mgao wa keki yake.


21 African nations

🔹

1500+ attendees

🔹

£6.5bn of commercial deals announced

View attachment 1328928
Kwa taarifa za Uhakika ni kuwa mwakilishi wa Tanzania alihitaji kwenda lakini Kiingereza kikawa kikwazo!
 

Bambushka

JF-Expert Member
Jan 9, 2020
2,743
2,000
😂😂😂jamani comment zenu hasa za lugha gani itakayotumika, they have made my day...khaa thanks jf...


Everyday is Saturday........:cool:
 

Ndahani

Platinum Member
Jun 3, 2008
17,598
2,000
Nchi zote za common wealth afrika zimehudhuria?

Ukiona unatumia njia ile ile iliyoshindwa kukupa majawabu kila wakati, na kutegemea kuona kitu tofauti, lazima utakuwa na shida.
Uingereza na hiyo commonwealth wametusaidia cha zaidi? Ni maslahi yao tu ndio wanayojari
 

Freddie Matuja

JF-Expert Member
Jul 21, 2018
1,162
2,000
Africa ina nchi kama 60. Deals ya kibiashara na msaada kwa nchi zote ni sawa na GBP 9bil sawa na takribani Tril 27

Kama nchi 50 zitapata mgao sawia wa cashflow kibiashara na msaada ni sawa na kama bil 540.

Mabeberu sometimes huwa sijui wanatuonaje Africa. Bora JPM hakwenda

Russia-Africa
Japan-Africa
China-Africa
Mabeberu #1 sote twajua-Africa.
Ufaransa-Afrika
Germany-Afrika

Kwanini kama wanatuheshimu sana basi walau waje Addis; yaaani sisi ni kuwafuata tu. Tunawasikiza; then tunapiga picha. Imetosha.
It's high time Afrika ijue wanatuhitaji kama ilivyokuwa huko nyuma;
Tukikaa kilofa; wataendeleza masuala ya kipuuuzi kama haya ya kila nchi kuwa na plan for Africa

Sent using Jamii Forums mobile app
 

sweettablet

JF-Expert Member
Nov 16, 2014
7,489
2,000
Kulikuwa na Russia - Africa Summit tupeni mrishonyuma. Kulikuwa na Japan - Africa Summit, tupeni mrishonyuma. Kulikuwa na China - Africa Summit, tupeni mrishonyuma.
Kulikuwa na Germany - Africa Summit, tupeni mrishonyuma.
 

Mbase1970

JF-Expert Member
Jun 11, 2015
6,054
2,000
Hapa kuna fursa nzuri lakin Tanzania hawataweza kuzifuatilia,bado sana.
Kama wangekuwa na nia pale brexit inaongelewa wangekuwa washaanza kunusanusa na kujipanga kama wanavyofanya wakenya au walivyofanya Canada na Australia kwa kuwaalika kwao.
Cha ajabu kitakachotokea ni kuwa wazungu watakuja kulima alafu wataondoka na mazao yao,sababu hii ndo inatokea mara nyingi kama wenyeji sio wachang'amkaji.Nakumbuka siku nilliona Tangazo kwenye la ice cream kwenye duka linaitwa waitrose (supermarket ya bei kidogo),"ice cream made with Tanzanian bloody oranges", sijui wangapi wanayajua haya machungwa,huo ni mfano mmoja tu bado hujaingiza green beans,aubergine vyote toka bongo vinauzwa uk na watu ambao sio watanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
Unajuaje kama ni vya Tanzania kama havina Label ama ni yale ya vijiweni ya wala unga na wavuta bhange?
 

Mbase1970

JF-Expert Member
Jun 11, 2015
6,054
2,000
Berlin Conference 1884.Sasa naona wameamua kuja mmoja mmoja. France-Africa. Uk-Africa,Russia-Africa,China-Africa,Japan-Africa. Hapa naweka conclusion Africa is potentiel. Thomas Sankara,Patrice Lumumba i wish mngekuwa hai.
Unajua hili jamvi limekimbiwa na Ma GT wote tuliobaki ni wabwabwajaji wengi wetu. Watu wamesahau kua Tanzania tulikataa ku sign EPA kwa wale wasiojua kutoka Afrika Mashariki Kenya na Rwanda peke yao walisaini hii Agreement. Sasa unadhani Tanzania wataalikwa? Kwasiojua EPA ni Economic Partnership Agreement.
 

Buyengwa

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
14,050
2,000
Haya ni mapambano ya kisiasa na kiuchumi kati ya Umoja wa nchi za Ulaya na Uingereza baada ya kujitoa kwenye Jumuiya ya nchi za Ulaya.

Hoja ya msingi sio kuhudhuria summit bali kuchagua upande wa vita ya kiuchumi kati ya Umoja wa Nchi za Ulaya na Uingereza!
UK ni moja wa nchi yenye FDIs nyingi na inayotoa misaada mingi Tanzania. Kuikwepa ni sawa na kuingiza kichwa chini ya mchanga huku kiwiliwili chote kipo nje.
 

Mzalendo2015

JF-Expert Member
Aug 14, 2012
6,614
2,000
UK ni moja wa nchi yenye FDIs nyingi na inayotoa misaada mingi Tanzania. Kuikwepa ni sawa na kuingiza kichwa chini ya mchanga huku kiwiliwili chote kipo nje.

FDI(Foreign Direct Investment) ni uwekezaji wa nchi husika kwenye nchi iliyo na mahusiano ya Kidiplomasia. Uingereza ni nchi iliyoendelea kiuchumi na kiviwanda.
Hakuna sababu za kimsingi kwa Tanzania kutoshiriki kwenye Summit hiyo zaidi ya upuuzi na viongozi kuhofia kuongea lugha ya Malkia…!
 

Mfiaukweli

JF-Expert Member
Aug 30, 2018
5,630
2,000
Unajua hili jamvi limekimbiwa na Ma GT wote tuliobaki ni wabwabwajaji wengi wetu. Watu wamesahau kua Tanzania tulikataa ku sign EPA kwa wale wasiojua kutoka Afrika Mashariki Kenya na Rwanda peke yao walisaini hii Agreement. Sasa unadhani Tanzania wataalikwa? Kwasiojua EPA ni Economic Partnership Agreement.

Agreed. Wewe ni mbwabwaji.
 

Mbase1970

JF-Expert Member
Jun 11, 2015
6,054
2,000
FDI(Foreign Direct Investment) ni uwekezaji wa nchi husika kwenye nchi iliyo na mahusiano ya Kidiplomasia. Uingereza ni nchi iliyoendelea kiuchumi na kiviwanda.
Hakuna sababu za kimsingi kwa Tanzania kutoshiriki kwenye Summit hiyo zaidi ya upuuzi na viongozi kuhofia kuongea lugha ya Malkia…!
Una uhakika kama tulialikwa?
 

samurai

JF-Expert Member
Oct 16, 2010
8,650
2,000
Kama huamini Tanzania ni tajiri kwa resources ilizonazo ardhini wewe ni pumbavu mkubwa sana.
Tatizo la Tanzania sio umaskini bali namna bora ya Ku- exploit raslimali hizo toka ardhini na kuzitumia sahihi kwa maslahi ya watanzania wote ,ikiwemo na kuzichakata, pasi kujali,jinsia,dini,rangi ya mtu.

Viongozi wetu wakillitambua hili na wakaacha ubinafsi taifa litapaa sana.Sent using Jamii Forums mobile app

Hilo sio tatizo la Tanzania pekee ni tatizo la Africa nzima na waarabu, na akili hiyo haiji hivi hivi kibwege bwege... Ulishajiuliza kwanini akili hiyo hatuna na baadala yake ni Wazungu tu ndio wenye akili hiyo...
 

mng'ato

JF-Expert Member
Oct 27, 2014
29,281
2,000
'Watu wamesahau kua Tanzania tulikataa ku sign EPA kwa wale wasiojua kutoka Afrika Mashariki Kenya na Rwanda peke yao walisaini hii Agreement. Sasa unadhani Tanzania wataalikwa?'

Then ikawaje Uganda ikaalikwa wkt na yenyewe haikusaini hio EPA?

Unajua hili jamvi limekimbiwa na Ma GT wote tuliobaki ni wabwabwajaji wengi wetu. Watu wamesahau kua Tanzania tulikataa ku sign EPA kwa wale wasiojua kutoka Afrika Mashariki Kenya na Rwanda peke yao walisaini hii Agreement. Sasa unadhani Tanzania wataalikwa? Kwasiojua EPA ni Economic Partnership Agreement.dodge
 

Kilatha

JF-Expert Member
Nov 28, 2018
3,958
2,000
Biashara ni kuchangamkia fursa na mipango, ndio waingereza wanachofanya.

Hawa wenzetu awachezi kamali na maswala uchumi siku zote ufanya risk assessment na kujikinga.

Kwa ivyo haya ni maandalizi ya life after BREXIT.

Ukiwa member ndani ya jumuiya ‘EU’ trade negotiations zilikuwa chini ya block control kwa lugha nyingine wana negotiate kwa pamoja hakuna kufanya mambo individually as a nation, ndio maana wakaja na EPA.

UK wanatoka EU, inatarajiwa by next year watakuwa full independent and responsible na uchumi wao ivyo inabidi wawe na trade zao kote duniani sio Africa tu hata EU itabidi wanegotiate nao upya jinsi yakufanya nao biashara. Ndio maandalizi yenyewe.

Kuna faida gani kwa Africa, kwa utaratibu wa sasa EU member state (wana custom union) hakuna ushuru wa kuagiza bidhaa kutoka nchi moja kwenda nyingine ndani ya jumuiya. Maana yake nini mfano muuzaji mkubwa wa maua EU ni Kenya na kwa sasa yanaingia kupitia Holland; retailers wa nchi nyingine ndani ya EU wana nunua Holland ndio na kupelekewa gharama ni usafiri tu.

UK wakitoka EU either inabidi wawe na deal nzuri na block kwenye hizi movement za bidhaa hili kusiwe na madhara ya bei au sasa waagize wenyewe maua kutoka Kenya.

Sasa imagine kuna bidhaa ngapi zinatoka nchi za Africa ambazo main supplier yupo nje ya UK na kutakuwa na impact gani wasipopata trade deal nzuri na EU?

Kuondoa hayo madhara baada ya BREXIT ndio sasa wanatafuta trade zao wenyewe; UK kuna waafrica wengi pia na asilimia kubwa ya vyakula vyao main supplier wapo Holland (wao ndio wananunua Africa au nchi zingine) na kuuzia UK retailers. Kwa ivyo fursa luluki zipo.

Sie tuendelee kujifungia tu, fursa zitatufuata because we are very special breed in planet earth.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom