Mimi ni mwalimu, juzi kati nikiwa nafundisha kuhusu topic ya Promoting Peace” wanafunzi walikuwa na maswali mengi sana.
Maswali yao yalikuwa ya kutaka kujua
1. kwa nini kuna nchi zipo vitani
2. kwa nini vita hutokea
3. Na ni namna gani vita uanza
Mfumo wa ufundishaji wangu ni wa kuwafanya wanafunzi wakatafute majibu ya maswali yao. Hivyo ikawa assignment kwao.
Wiki iliyofuata wakaja ku present walichokipata.
Wakati wana present kuna mwanafunzi walionyesha kuwa na wasiwasi, nikamuuliza mbona uso wako kama una wasi-wasi? Akasema anaogopa kinachoendelea nchini kwani kuna viashiria vya uvunjifu wa amani. Akasema hapendi vita na hapendi kuona watu wanauwana.
Bila shaka huu ulikuwa ujumbe kwangu kama mzazi, mwalimu na mwananchi ambaye nafurahia amani ya nchi yetu.
Ingawaje kuna changamoto au viashiria vya uvunjifu wa amani na ukiukwaji wa haki za binadamu, nilimuakikishia kuwa sisi hapa Tanzania tupo salama kutokana na uongozi imara na misingi ya upendo uliopo miongoni mwa wananchi wote.
Kwa watu wazima sasa:
“Yote tunayoyafanya katika kujiletea maendeleo au kuleta maendeleo ya nchi, basi tuilinde tunu ya Amani. Hii ikipotea tu ni ngumu kuipata.”
Na amani itaendela kuwepo
ZINGATIA: “Hakuna nchi au jamii ambayo ina kinga dhidi ya vita.” Tukikosea step tu, hao…tutapoteana na kupoteza vitu vyote tulivyonavyo.

- Tukiendelea kutoa haki
- Kuhubiri na kufundisha kuhusu Amani
- Kuhukumu kwa haki
- Kupambana na umaskini
- Mahusiano mazuri na nchi jirani na dunia kwa ujumla