Ujumbe wa wazi wa Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa kwa Askofu Methodius Kilaini

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,013
Ujumbe wa wazi wa Mkt Bavicha Taifa kwa Mhashamu baba Askofu Methodius Kilaini Askofu msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba.

Na John Pambalu

Baba Askofu salamu. Kwanza nakutakia heri ya Krismasi na mwaka mpya.

Ninakushukuru pia kwa ajili ya mahubiri/ maoni yako kuhusu mwaka 2020 kama yalivyochapishwa katika gazeti la Mwananchi.

Umesema kutokana na changamoto za uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 umetaka tusameheane kwa yote yaliyotokea.

Nafikiri unajua kabisa ni nini kilitokea kilichosababisha CCM kujitangazia ushindi bara na visiwani kwa zaidi ya 95% katika Bunge na zaidi ya 80% kwa kura za urais.

Baba Askofu ni bahati mbaya haya yote yanatokea katika kipindi ambapo kanisa limechagua kunyamaza kimya (Bila kutoa msimamo wa pamoja) na badala yake kazi hiyo imebaki kwa watumishi mmoja mmoja kama Askofu Mwamakula, Bagonza, Padri Kitima, Sheikh Ponda, Sheikh Rajabu Katimba na wengine wachache. Jamii inajiuliza kwa nini mmechagua kukaa kimya?

Nataka kusema nini? Tangu Askofu Kakobe na Niwemugizi walivyochunguzwa uraia wao. Tumeona watumishi wengi wa Mungu mmechagua kurudi nyuma na kuacha dhuruma izidi kutawala katika taifa letu.

Mhashamu baba Askofu, huku uraiani sisi ambao ni waumini wa dhehebu la Kikatoliki, wananchi wenzetu wasiokuwa waumini wa dhehebu letu wanahoji, ule msimamo wa kanisa letu kuikemea serikali kama ulivyokuwepo wakati wa serikali ya Kikwete umekwenda wapi?

Wacha tuyaache hayo. Nirejee kwenye ajenda yako ya kusameheana.

Baba Askofu kama mpatanishi wa kiroho na kijamii naamini unaifahamu misingi ya upatanishi kati ya pande mbili zinazo umizana.

Wacha nikupe picha kidogo. Mwishoni mwa mwaka jana Tume ya taifa ya Uchaguzi na Spika wa Bunge wamajitangazia wabunge wao wa viti maalumu kuwa eti ni wabunge wa Chadema na ikawaapisha. Chadema kama taasisi tukakaa tukaona tuchukue hatua za kinidhamu za kuwafuta uanachama.

Spika wa Bunge akasema piga ua garagaza watabaki bungeni. Akajitokeza Spika wa Bunge mstaafu Pius Msekwa akasema hawa wamepoteza sifa. Ndugai akajitokeza hadharani akawaambia waandishi wa habari acheni kuwahoji wastaafu njooni mnihoji mimi. Bado mlikaa kimya!

Haya ya uchaguzi, mengi yanajulikana mauaji ya wafuasi wa upinzani, polisi kubeba kura za mabegi ili kuingiza kwenye maboksi, kukamata viongozi wa upinzani na kuwapa kesi kama za ugaidi, uhujumu uchumi, uvamizi Nk. Bado mlikaa kimya tu.

Baba Askofu wakati unasema tusameheane Kuna wanachama wa Chadema zaidi ya 200 wako magereza kwa kesi nzitonzito. Jimbo la Tunduma peke yake kuna mahabusu zaidi ya 50 jimbo moja tu. Na lenyewe mmechagua kukaa kimya.

Haya na mengine mengi yanaumiza sana kiasi cha kufikirisha kuwa huenda visasi vikawa suruhu yake maana labda pande zote zikiumia mnaweza kuitana kujadiliana kwa ajili ya Amani.

Baba Askofu sisi kama Chadema tunasema "No Hate No Fear". Hatuna haja ya kulipiza visasi ila tuanataka HAKI itamalaki katika taifa.

Baba Askofu nimekueleza haya si tu kukueleza wewe peke yako juu ya hisia zangu na za vijana wenzangu ninaowaongoza, Bali kuwaeleza viongozi wote wa kiroho kuwa tunahitaji msaada wenu katika kuleta utengamano katika taifa letu.

Niseme nini tena? Nikuombe mambo 2.

1. Ielezeni serikali iachilie huru watuhumiwa na wafungwa wote wa kisiasa.

2. Ungana nasi katika VUGUVUGU la kudai KATIBA MPYA.

Nakutakia kila la Kheri katika utumishi wako.

Wasalaam.
John Pambalu
Mkt Bavicha taifa.
jpambalu@gmail.com
 
Huyu Kilaini namuona amepotoka kidogo kwenye hili, kwangu ningemuona wa maana zaidi kama kwanza angekemea ile dhuluma ya wazi iliyofanywa na CCM kwenye ule uchaguzi halafu ndio aje na habari za upatanishi.

Vinginevyo kuja na hoja ya upatanishi moja kwa moja kabla ya kukemea uovu kwangu ni dalili ya uoga (kuliogopa) kundi mojawapo kwenye huo uhasama, lakini pia tabia hii haitasaidia kumaliza tatizo kwa kundi moja kuendeleza ubabe kwa jingine kwasababu hakuna yeyote anaelikemea.
 
Tumsamehe kwa vile ni vicha. No hate no fear means tusameehane.
 
Ujumbe wa wazi wa Mkt Bavicha Taifa kwa Mhashamu baba Askofu Methodius Kilaini Askofu msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba.

Na John Pambalu

Baba Askofu salamu. Kwanza nakutakia heri ya Krismasi na mwaka mpya.

Ninakushukuru pia kwa ajili ya mahubiri/ maoni yako kuhusu mwaka 2020 kama yalivyochapishwa katika gazeti la Mwananchi.

Umesema kutokana na changamoto za uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 umetaka tusameheane kwa yote yaliyotokea.

Nafikiri unajua kabisa ni nini kilitokea kilichosababisha CCM kujitangazia ushindi bara na visiwani kwa zaidi ya 95% katika Bunge na zaidi ya 80% kwa kura za urais.

Baba Askofu ni bahati mbaya haya yote yanatokea katika kipindi ambapo kanisa limechagua kunyamaza kimya (Bila kutoa msimamo wa pamoja) na badala yake kazi hiyo imebaki kwa watumishi mmoja mmoja kama Askofu Mwamakula, Bagonza, Padri Kitima, Sheikh Ponda, Sheikh Rajabu Katimba na wengine wachache. Jamii inajiuliza kwa nini mmechagua kukaa kimya?

Nataka kusema nini? Tangu Askofu Kakobe na Niwemugizi walivyochunguzwa uraia wao. Tumeona watumishi wengi wa Mungu mmechagua kurudi nyuma na kuacha dhuruma izidi kutawala katika taifa letu.

Mhashamu baba Askofu, huku uraiani sisi ambao ni waumini wa dhehebu la Kikatoliki, wananchi wenzetu wasiokuwa waumini wa dhehebu letu wanahoji, ule msimamo wa kanisa letu kuikemea serikali kama ulivyokuwepo wakati wa serikali ya Kikwete umekwenda wapi?

Wacha tuyaache hayo. Nirejee kwenye ajenda yako ya kusameheana.

Baba Askofu kama mpatanishi wa kiroho na kijamii naamini unaifahamu misingi ya upatanishi kati ya pande mbili zinazo umizana.

Wacha nikupe picha kidogo. Mwishoni mwa mwaka jana Tume ya taifa ya Uchaguzi na Spika wa Bunge wamajitangazia wabunge wao wa viti maalumu kuwa eti ni wabunge wa Chadema na ikawaapisha. Chadema kama taasisi tukakaa tukaona tuchukue hatua za kinidhamu za kuwafuta uanachama.

Spika wa Bunge akasema piga ua garagaza watabaki bungeni. Akajitokeza Spika wa Bunge mstaafu Pius Msekwa akasema hawa wamepoteza sifa. Ndugai akajitokeza hadharani akawaambia waandishi wa habari acheni kuwahoji wastaafu njooni mnihoji mimi. Bado mlikaa kimya!

Haya ya uchaguzi, mengi yanajulikana mauaji ya wafuasi wa upinzani, polisi kubeba kura za mabegi ili kuingiza kwenye maboksi, kukamata viongozi wa upinzani na kuwapa kesi kama za ugaidi, uhujumu uchumi, uvamizi Nk. Bado mlikaa kimya tu.

Baba Askofu wakati unasema tusameheane Kuna wanachama wa Chadema zaidi ya 200 wako magereza kwa kesi nzitonzito. Jimbo la Tunduma peke yake kuna mahabusu zaidi ya 50 jimbo moja tu. Na lenyewe mmechagua kukaa kimya.

Haya na mengine mengi yanaumiza sana kiasi cha kufikirisha kuwa huenda visasi vikawa suruhu yake maana labda pande zote zikiumia mnaweza kuitana kujadiliana kwa ajili ya Amani.

Baba Askofu sisi kama Chadema tunasema "No Hate No Fear". Hatuna haja ya kulipiza visasi ila tuanataka HAKI itamalaki katika taifa.

Baba Askofu nimekueleza haya si tu kukueleza wewe peke yako juu ya hisia zangu na za vijana wenzangu ninaowaongoza, Bali kuwaeleza viongozi wote wa kiroho kuwa tunahitaji msaada wenu katika kuleta utengamano katika taifa letu.

Niseme nini tena? Nikuombe mambo 2.

1. Ielezeni serikali iachilie huru watuhumiwa na wafungwa wote wa kisiasa.

2. Ungana nasi katika VUGUVUGU la kudai KATIBA MPYA.

Nakutakia kila la Kheri katika utumishi wako.

Wasalaam.
John Pambalu
Mkt Bavicha taifa.
jpambalu@gmail.com
Ujumbe murua sana,lugha imenyooka hatari,
Huyu askofu,amekuwa muoga Kama kunguru,tangu aliposhughurikiwa kwa ushawishi wa serikali ya Kikwete na kuhamishwa Dar na kuperekwa bukoba,hajawahi kupona
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Back
Top Bottom