DOKEZO Ujumbe wa waliokuwa Wafanyakazi wa TPA kwenda kwa Rais Samia Suluhu Hassan, wasema walifukuzwa kazi hawajalipwa stahiki zao

DOKEZO Ujumbe wa waliokuwa Wafanyakazi wa TPA kwenda kwa Rais Samia Suluhu Hassan, wasema walifukuzwa kazi hawajalipwa stahiki zao

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

DodomaTZ

Senior Member
Joined
May 20, 2022
Posts
161
Reaction score
200

111.jpg

2222.jpg
TAARIFA KWA WAANDISHI WA HABARI

JINA : HAMIS MBWANA MZENGA
Awali ya yote kwa niaba ya wahanga wenzangu, Tunamshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama yetu Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri ya kuwatetea wanyonge. Tunaimani na kauli mbiu yake ya KAZI NA UTU TUNASONGA MBELE.

Sisi tuliokuwa wafanyakazi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania, tunakuomba Mama yetu mpendwa Mhe. Samia Suluhu Hassan utusaidie kupata haki yetu ambayo tumekuwa tunahangaika kwa viongozi wa Serikali ambao wamekuwa wanashindwa kutusaidia tena ni viongozi wa ngazi ya juu.

MZENGA
Mamlaka ya Bandari TPA iliomba askari kutoka JKT katika Makambi ya JKT Mgulani na JKT Mlalakuwa mwaka 2009. Maombi ambayo JKT walijibu kwa kuwaeleza Bandari kwamba wanavijana 81 ambao 28 ni darasa la 7, na 28 kidato cha nne, kutoka JKT Mgulani na vijana 25 kutoka JKT Mlalakuwa, Bandari wakajibu walete kwa barua hizi hapa.

KWA MASIKITIKO
Katika zoezi la uhakiki wa vyeti tulitakiwa kupeleka vyeti vya kidato cha nne na muajiri wetu Bandari. Tukawajibu hatuna hivyo vyeti kwani hata ajira zetu tumeajiliwa tukifahamika ni darasa la saba (7).

Hatimaye tarehe 15/09/2018 tulipewa barua ya kufukuzwa kazi kwa kosa la kujipatia ajira pasipokuwa na sifa sitahiki kwa upande wetu tunashangaa kosa la kufukuzwa kazi kwa kusema tumejipatia ajira wakati wao ndio waliotufuata kwenye makambi ya JKT tuliokuwa tunafanya kazi.

Tumeitumikia Mamlaka kwa miaka kumi (10) hadi tunafukuzwa kazi muda wote wa ajira yetu na ndani ya mikataba yetu ya ajira kulikuwa na kipengelecha cha 35% ya mishahara yetu tunalipwa kwa ajili ya kodi ya nyumba. Kwa masikitiko makubwa baada ya kufukuzwa kazi mamlaka ya Bandari imetulipa malipo madogo mfano kama mimi HAMIS MZENGA nimelipwa Tsh. 3,200/= tu ikiwa ni nauri ya mimi na familia yangu, mshahara wa mwezi mmoja (1) badala ya NOTICE na gharama za kufungasha mizigo 238,000/= jambo ambalo nimeshindwa kuelewa hii pesa niliopewa mbona haifanani na muda wangu wa utumishi? Na hata muda niliokaa kusubiri hayo malipo.

OMBI
Tunakuomba Mhe. Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania utusaidie kupata stahiki zetu pamoja na pesa za kujikimu huku tukisubiri kurudishwa maskani tulikotoka. Kwani tumefanya kazi kwa uaminifu kwa zaidi ya miaka kumi (10).

Tumekuwa tukikutana na majibu ambayo kwa upande wa Mamlaka ya Bandari wanasema wametulipa malipo hayo kutoka na maelekezo ya serikali, na malipo yenyewe ni kama hayo ya Tsh. 3,200/=. Kwa muda wote wa utumishi wangu au wetu kwa ujumla. Hivyo kupitia Mama yetu mpendwa tunaimani tutapata stahiki zetu kwa muda wote tuliofanya kazi kwani sisi tuliombwa kuja kufanya kazi ambayo tulifanya kwa uaminifu mkubwa lakini ndio tulipwe Tsh. 3,200/=. Mama yetu wewe ndio tumaini letu kwasasa

Mwisho MWENYEZI MUNGU amlinde na kila jambo Amiin
KAZI NA UTU TUNASONGA MBELE


MSEMAJI
Awali ya yote kwa niaba ya wahanga wenzangu, Tunamshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama yetu Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri ya kuwatetea wanyonge. Tunaimani na kauli mbiyu yake ya KAZI NA UTU TUNASONGA MBELE

Tumelazimika kuwaita Waandishi wa Habari ili muweze kutufikishia malalamiko yetu kwa Mama yetu na Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Tunaamini Mhe. Rais mama yetu mpendwa aufahamu hiki kilio chetu cha muda mrefu zaidi ya miaka sita 6 ambacho tumekosa haki zetu tulizostahili kulipwa kutoka kwa aliekuwa muajiri wetu.

Ikiwemo haki ya malipo ya kujikim wakati tukisubiri kurudishwa maskani kwetu tulikotoka kwa muda miaka minne 4 pamoja na haki ya malipo utumishi kwa kipindi chote cha utumishi wetu.

Mhe rais mama yetu tumelazimika kutumia waandishi wa habari ili waweze kutufikishia kilio chetu kwako tukiamini wewe ndio mkombozi wetu wa kutuokoa na mateso tunayoyapia kwa muda mrefu wa kuhangaika kwenye ofisi mbalimbali za Wasaidizi wake bila kupata msaada zaidi ya kutupa majibu ambayo tunakosa haki zetu tuliozostahili kupata. Kimsingi tulistahili kulipwa posho ya kujikimu huku tukisubiri kurudishwa makwetu pamoja na malipo ya utumishi wetu.

JITIHADA TULIZOZIFANYA
Baada ya kulipwa nje ya muda tena kwa malipo pungufu tulimuandikia mwajiri wetu ambae ni Mamlaka ya Bandari kuomba stahiki ya Posho ya kujikimu muda tukisubiri malipo ya kurudishwa makwetu. Mwajiri alijibu na kukiri kuchelewesha kufanya malipo akisubiri maelekezo kutoka Serikalini Ofisi ya Utumishi wa Umma. Kwa barua yenye Kumb namba BA. 534/583/01-A/74 ya tarehe 20/OCT/2022 tunaambatanisha.

Baada ya majibu hayo kwa makundi tofauti tofauti tuliiandikia barua tume ya Utumishi wa Umma tukiomba haki zetu ambako nako tulipata majibu ya tume ikituelekeza kupeleka malalamiko yetu kwa Katibu Mkuu Utumishi wa Umma kwa barua yenye kumbu Na. CAD. 26/55/012/31-17/JAN/2023 tunaambanisha. Tulifanya hivyo kama tulivyoelekezwa na Tume.

Kumuandikia Katibu Mkuu utumishi wa Umma tunasikitishwa na majibu ya Katibu Mkuu kwa kusema hatulistahili kulipwa kwa sababu tulifukuzwa kazi kwa kosa la kujipatia ajira pasipokuwa na sifa stahik hali akijua sisi tuliombwa kuja kufanya kazi kutoka JKT na baadhi yetu tuliokuwa vibarua wa muda mrefu kuanzia miaka ya 1993 na kuendelia na baadae kupewa ajira.

Bila kuangalia madai ya msingi au kisheria katibu mkuu utumishi alitujibu kwa barua yenye kumbukumbu namba CA.271/313/01/A/36 ya 10/01/2025 tunaambanisha Katika jitihada za kuomba msaada wa kuomba haki yetu, tuliandika barua kwenda kwa Mhe. Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mama yetu mpendwa, kuomba msaada wa utatuzi wa swala letu.

Majibu ya awali kutoka kwa katibu mkuu kiongozi ambayo kwa barua yake hiyo alikiri kwa tunastahili kulipwa na alita vilelezo kutoka kwa muajiri wetu barua yenye kumbukumbu namba SBA.91/558/04B/33 ya 05/07/2024 naambatanisha.

Kwa masikitiko makubwa mara baada ya kupeleka vilelezo tulipata majibu yakwamba hatustahili kulipwa kwani tayari tumeshalipwa jambo ambalo tunaamini kwamba taarifa aliyopewa kutoka kwa muajiri wetu sio sahihi ya kwa tumelipwa stahiki zetu zote. Tunalazika kusema wasaidizi wako wanakuangusha au hawakusaidii kutenda haki kama vile wewe unavyotutendea wananchi wako.

Mama tunakupongeza kwa kazi iliyotukuka kwa watanzania, tunaamini kupitia wewe mama yetu mpendwa utatusaidia kupata haki yetu. Mama tumekuwa kunasikitishwa na hiki kinachofanywa na wasaidizi wako IKIWA TAASISI IMEOMBA WAFANYAKAZI KUTOKA TAASISI NYINGINE KABLA YA KUPEWA WALISHAPEWA SIFA ZAO NA WAO WAKASEMA WALETE TUNAWAHITAJI inakuwaje unakuja kumfukuza kazi kwa kumdharirisha? Tena unamnyima haki zake kwa madai alijipatia ajira huku ukijua wakati wa ajira yake hakufanya udanganyifu wowote.

Mhe. Rais tumekuwa tunapitia kipindi kigumu sana, kwani hadi hivi sasa bado tuko kwenye vituo vyetu vya kazi kwani nauli tuliopata ni ndogo kutokana na madeni ya kodi ya nyumba tulikuwa tumepangishiwa na bandari tulio wengi vitu vyetu vimezuiwa na wenye nyumba baada ya bandari kutolipa kodi huku tukisuburia kurudishwa makwetu.

Mhe. Rais kwa waliotokea JKT wamefanyakazi miaka kumi 10 na waliokuwa vibarua wa muda mrefu na kupewa ajira ni zaidi ya miaka hiyo unakuja kumfukuza kazi na kumlipa Tsh. 3,200/= kama stahiki zake hii kwetu imekuwa ni zaidi ya maumivu. Tunaamini kupia wewe mama yetu kipenzi cha watanzania tutapata msada wa kupata tumaini jipya kwenye maisha

Mhe Rais tunalazimika kusema wasaidizi wako wanakuangusha kwani baada ya kufukuzwa kazi aliekuwa muajiri wetu aliandika barua mara nyingi kwenda WIZARA YA UTUMISHI akiomba nafuu ya kurudishwa kazini kwa watumishi wa aina yetu darasa la saba, pamoja na watu wengine tisa 9 ambao walitoka kwa swala la vyeti. Kwa masikitiko makubwa kwa upande wetu WIZARA ilikataa kuturudisha kazini badala yake wakarudishwa kazini wale watu 9 ambao walitolewa kwa kosa la vyeti vya kugushi. Tumejaribu kufuatilia sehemu mbali mbali bila mafanikio

Ahsanteni Sana,

Imeandaliwa na

…………………………
MWENYEKITI WA KAMATI

photo_2025-03-26_16-54-36.jpg

photo_2025-03-26_16-54-57.jpg

photo_2025-03-26_16-55-02.jpg

photo_2025-03-26_16-55-14.jpg

photo_2025-03-26_16-55-21.jpg

photo_2025-03-26_16-55-31.jpg

Pia soma ~ Askari wa JKT tulioishia Darasa la 7 hatujalipwa stahiki zetu na TPA tangu tulipoachishwa kazi Mwaka 2018
 
OMBI
Tunakuomba Mhe. Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania utusaidie kupata stahiki zetu pamoja na pesa za kujikimu huku tukisubiri kurudishwa maskani tulikotoka. Kwani tumefanya kazi kwa uaminifu kwa zaidi ya miaka kumi (10).
Atawaelewa?
 
Watajijua,
Tukiwaambia hii nchi CCM haitakiwi hamuelewi
Hamlipwi hela wakati bongo muvi na bongo fleva wanapelekwa Korea kula maisha na wanaishi kwenye mahoteli ya nyota tano

Mtakoma
 
Mama yetu mpendwa, mama yetu mpendwa.... Mwiteni Rais acheni uchawa wa mama mama mpendwa. Yule ni Rais hivyo mwiteni Mheshimiwa Rais...
Any way poleni ila msisahau kuendela kumpgia kura mpendwa.
 
  • Thanks
Reactions: vnn
Kuna taarifa haijawekwa wazi hapo.
Tupe mchanganuo wa kulipwa hiyo 3,200/= yaweza kuwa stahili yako ilikuwa may be 52,000,000/= lakini hapo hapo una mikopo;
Mkopo wa Nyumba 32M
Mkopo wa gari 15M
Cash Advance 3M nk nk
Wakiitoa yote hicho ulicholipwa ndio stahili yako. Madai haya yamekuwa ya upande mmoja kitaalamu ni ngumu kutoa utetezi wa moja kwa moja.
All in all pambanieni haki yenu
 
Kwa Jina naitwa Godfrey Mwakasendo, Mama yangu Mzazi ni muhanga mmoja wapo wa hili suala la kufukuzwa kazi katika Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Jina lake ni Happyness Arthur Mwaitenda aliajiriwa Mnamo mwaka 2006 kwa sheria ya ajira ya mwaka 2004 akipeleka vyeti vya darasa la saba yani elimu ya msingi akiwa na ujuzi wa ulinzi na cheti cha mgambo na kitambulisho.

Sanjali na hayo alipata uzoefu wa masuala ya ulinzi katika Kampuni ya ulinzi iitwayo GENERAL GUARD TANZANIA amabayo kwa mwaka 2000 mpaka 2006 ilikuwa Ina mkataba na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).

Happiness Arthur Mwaitenda-Security Guard alifanya alipangiwa kazi katika Lindo la Bandari College mwaka 2003 na baada ya mwezi mmoja kuamishiwa zahanati ya bandari iliyopo Kurasini, alifanya kazi yake kwa uadilifu na uaminifu huku akimuheshimu mkubwa na mdogo.

Mnamo mwaka 2004, Mama yangu Mzazi yani Happyness Arthur Mwaitenda alipata taarifa kwamba Kuna nafasi za ajira mamlaka ya bandari imentangaza na katika nafasi hizo zilikuwepo nafasi za Askari au kwa kipindi hicho zilikuwa zinajulikana kana Auxiliary Police (Polisi wasaidizi) waliokuwa wanafanya kazi TPA.

Happyness Arthur Mwaitenda Aliomba nafasi za kazi kwa kutumia utaratibu wa kipindi hicho na kuwasilisha nyaraka zote zilizokuwa zinahitajika, baadae alifanikiwa kupata ajira ya mkataba ndani ya Mamlaka ya Bandari Tanzania.

Alipangiwa kituo cha kazi Mkoani Mtwara mwaka huo 2006 mwezi wa 6, mimi nikiwa darasa la 6 nasoma shule ya msingi kurasini B kwa Sasa ni Mivinjeni Shule ya msingi ambayo inabomolewa hivi karibuni kwasababu ya muwekezaji uchwara GS* akipigiwa shavu na mzee wa msog* huku wakisema ni DP WORLD Shame on this Government.

Tuendelee katika Mada return, Happyness Arthur Mwaitenda Alifanya kazi kwa uadilifu, uaminifu na uhajibikaji wa Hali ya juu akiwa chini ya viongozi mabli mbali wa idara yake na utumishi wake ulitukuka japo kuwa ya kuwa wengi ya wakubwa wake walitokea idara nyeti za serikali kama TISS, TANPOL, na JWTZ na pia viongozi wake walifahumu yakuwa Happyness Arthur Mwaitenda alitokea katika familia ya kiongozi wa TANPOL, alikuwa RC MTWARA, TABORA, DSM KANDA MAALUMU huyo ni Aloyce Arthur Bulinda Mwaitenda.

Pia Baba Mzazi wa Happyness Arthur Mwaitenda alikuwa bado yupo mpaka 2016 alipostaafu kama Kachero mwandamizi kutokea TISS na DCI ( Mkurugenzi wa Mashitaka Tanzania).

Chloe na wadhifa wa mzazi wa Happyness Arthur Mwaitenda hakikumpatia kiburi na majivuno kwa viongozi wake akiwa katika utumishi wake katika Mamlaka ya Bandari Tanzania mpaka mwaka 2018.

Happyness Arthur Mwaitenda (Mama Yangu Mzazi) alifukuzwa kazi mnamo mwaka 2018/September/29 nakumbuka kwakuwa nilikuwa nimemaliza kusoma chuo cha kilimo sokoine (SUA).

Nikiwa nyumbani kwa Mama yangu mzazi (Happyness Arthur Mwaitenda) siku hiyo nilikuwa nimeshakula vizuri mchana mzazi wangu alirudi nyumbani akiwa na uso wake wa furaha bila wasi kabisa alikuwa ameshika Barca yake ya kufukuzwa kazi na alinikabidhi niliisoma na nilikuwa nishikwa na mshangao ghafla ila sikutaka kumpatia hofu sana.

Kwakuwa Mama yangu alikuwa Hana kosa lolote na alipatiwa ajira ya mkataba na baadae alithibitishwa na kupewa mkataba wa kutumudu mpaka atakapo maliza miaka yake ya utumishi wake yani miaka 60.

Nilimpatia maneno ya kumuondolea mawazo na maisha yaliendelea .


Tutaendelea.....
 
Hawa si ndio walikuwa wanasema suala la uwekezaji bandarini ni wakirisitu wanaona wivu na ni suala la kidini? 😂 😂 😂 😂 😂
 
Kuna taarifa haijawekwa wazi hapo.
Tupe mchanganuo wa kulipwa hiyo 3,200/= yaweza kuwa stahili yako ilikuwa may be 52,000,000/= lakini hapo hapo una mikopo;
Mkopo wa Nyumba 32M
Mkopo wa gari 15M
Cash Advance 3M nk nk
Wakiitoa yote hicho ulicholipwa ndio stahili yako. Madai haya yamekuwa ya upande mmoja kitaalamu ni ngumu kutoa utetezi wa moja kwa moja.
All in all pambanieni haki yenu
Mlinzi alipwe million 52🤣🤣🤣
 
Kama ni kweli hamfahamu pa kupeleka malalamiko yenu basi tunasafari ndefu km taifa..

Nyerere alikosea sana kuomba uhuru kwa watu ambao hawajajitambua
 
Ila sauti zimepazwa na jambo linaenda sawa, samia mitano tena deni linalipwa
Una UPUMBAVU sana,sasa kumuanika Mama yako HAPPINESS MWAITENDA na porojo nyiiingi sijui mtoto wa nani kulikusaidia nini??angekuwa mtoto au ndugu wa hao wakubwa uliowataja angeishia standard seven??
 
Back
Top Bottom