Ujumbe wa Maulid Kitenge kwa "Wanainsta"

Chaos Master

JF-Expert Member
Jul 7, 2021
636
1,304
''Kuna watu inawezekana tumejuana kwa kutuona kwa mitandao humu na ndio maana wakati mwingine wanatutukana! Muungwana anapokea kila aina ya matusi na anamshtakia Mungu tu! Safari yetu wengine ilikuwa ndefu sana kwenye tasnia hii. Tumetembea sana kwa miguu, tumekula sana mihogo ya kukaanga barabarani na hii yote katika kusaka habari na kuwahabarisha watu.

Mungu aiweke roho ya marehemu Efrahim Kibonde mahala panapostahili, lakini angekuwa leo yeye angeweza kusema kitu! Ila wale wanaotuona leo mitadaoni tunasafiri huku na kule wanadhani tumeamka tu asubuhi na kukurupuka! Safari ilikuwa ndefu sana na hakuna aliye jua kesho yake.

Mungu mkubwa baada ya miaka 20 tunaendelea kupambana! Tumesota sana, tumesaga lami sana yote kwa kupambana kufika mbele. Mafanikio hayaji kwa kuamka tu asubuhi yanahangaikiwa usiku na mchana! Tupambane. Jioni njema wana wa insta tuliojuana humu.'' @maulidkitenge
 
Asifanananishe zaman na sasa zamn kutoboa ilikua rahisi tofauti na sasa, zaman kujuana hakukuwepo mtu ukitoka chuo tyr unakazi, sahv mpaka usugue sana bench,

Zaman kama unamtaj ilikua rahis kufungua busn na ukapata faida, sahv fursa mpaka utumie akili sana. Inshort mtu anayepambana zama hv muheshim sana asee.
 
Asifanananishe zaman na sasa zamn kutoboa ilikua rahisi tofauti na sasa, zaman kujuana hakukuwepo mtu ukitoka chuo tyr unakazi, sahv mpaka usugue sana bench,

Zaman kama unamtaj ilikua rahis kufungua busn na ukapata faida, sahv fursa mpaka utumie akili sana. Inshort mtu anayepambana zama hv muheshim sana asee.
kwel tupu aseeh
 
Kila mmoja kwenye maisha alishasota kwa namna yake.Mwambieni hiyo ni kawaida tu katika maisha.Cha msingi atujibu,tangu atoboe kimaisha jamii inafaidika naye vipi?
Apart from kuwa kama roll model kwa vijana wengi wa tasnia ya habari za michezo nahisi atakua kashawahi kurudisha kwa Jamii ingawa sina rekodi za matukio yake
 
Nilishajitoaga insta na fesibuku maana hakuna chamaana zaidi ya kila mtu kujimwambafai na wanawake kuonyesha makalio yao tu.

Kwenye hiyo mitandao kila mtu ni tajiri na unaweza ukakata tamaa ya maisha kwa kujiona umechelewa sana
 
Back
Top Bottom