Ujumbe wa Jane wa Mwenge kwa mlio lala nae

Status
Not open for further replies.
Mimi ni Jane naishi mwenge Dar es
salaam naomba utalifuta jina la
baba yangu maana sitaki liwe
kwenye jf watu watanijua na
kuniangamiza maana
nimeshawaangamiza wengi sana
kwa UKIMWI ila mengine yote
usifute hata moja
ili dunia ijue tu japokua mimi
nitakufa kwa huu ukimwi nilionao.
Nilizaliwa mkoa wa Dodoma na
nilishi vizuri tu tangu utotoni na
hata
sikujihusisha na ngono hadi
nilipomaliza form 4 mwaka 2006
baada ya kumaliza nilikuja hapa
Dar kuishi kwa mama mdogo
aliyeolewa hapa Mwenge.
Nilipata marafiki wengi tu na
kuna kijana mmoja alinitongoza
kwa muda mrefu sana na siunajua
vijana wengi hutumia muda mrefu
kutongoza ili msichana unadhani
kwamba labda huyo anakupenda
kumbe anataka tu ngono na
wadada wengi sana hudhani
kufuatiliwa kwa muda mrefu na
mvulana basi huyo yuko serious
kumbe hakuna lolote.
Nilimkubalia tukawa wapenzi ila
nilikataa kuhusu kufanya mapenzi
maana anayekupenda kiukweli sio
uongo lazima asitake ngono kabla
ya ndoa.
Kwa miezi kama 5 hadi 6
aliniambia kuhusu kufanya
mapenzi nilikataa alitumia mbinu
nyingi sana kwa kunibembeleza na
hata kulia mbele yangu ili tufanye
tu mara moja ila nilikataa, alisema
atavumilia hadi siku ya ndoa yetu
ambapo tulipanga kuoana mwaka
sept 2009.
Siku moja aliniambia twende
kwenye kumbi za starehe na mimi
kwa sababu ya upagani na
kumwamini pia kwa sababu
nampenda nilikubali tulienda huko
na kulikua na bendi fulani maarufu
ya mziki wa dansi ilikua
inatumbuiza.
Tulitafuta sehemu na kukaa na
mpenzi wangu akaagiza pombe
alianza kunywa huku akinionjesha,
nilikataa kwa sababu nilikua
sijawahi kunywa pombe katika
maisha yangu yote, hata sijui
alinishawishi vipi nilijikuta
nakunywa kidogo kidogo na kwa
kuwa tulikaa pale kwa muda zaidi
ya masaa 5 nadhani nikunywa
kama bia 3 au 4 japokua nilikua
nakunywa kidogo kidogo tu tena
kwa kunywesha na mpenzi wangu
maana nikama nikua nanyweshwa
kila baada kama ya dakika 25 ndipo
nakunywa mara moja na sikujuia
kama nakunywa pombe ila niliihisi
tu naonja ili kumlizisha mpenzi
wangu.
Ilipofika saa 10 alfajiri nilihisi
usingizi na pia nilijiona wa tofauti
najua nililewa hata kama sikujua
kama nimelewa maana nakumbuka
tulitoka pale huku amenishika
mkono huyo mpenzi wangu.
Tulikodo tax na kuondoka na siku
hiyo aliniambia twende kwake
alikokua amepanga chumba maana
tulikua na usingizi sana nilikubali
huku nikidhani hatuwezi kufanya
mapenzi.
Tulifika salama na kuingia ndani
ukweli pombe ni kichocheo cha
ngono na ningekua mimi ndio Raisi
wa Tanzania ningefunga bar zote.
Nilijikuta natamani kufanya
mapenzi na huyu mpenzi wangu
hata alikua hana nia maana alijua
atanichukiza sana na uhusiano
ungekufa siku hiyo lakini kwa
sababu ya pombe nilimwambia siku
hiyo tufanye kidogo maana mwili
wangu unataka.
Ni kweli siku hiyo kwa sababu ya
pombe nilifanya mapenzi na huyo
mpenzi wangu na baadae
akanipeleka nyumbani baada ya
wiki mbili maana tulikaa wiki mbili
bila kuonana alikuja na kunieleza
habari ambayo sikuihitaji katika
maisha yangu maana nilikua nasikia
tu kwa watu wengine lakini sio
kwangu alisema ”JANE ISHI KWA
MATUMAINI KUANZIA SASA”
Nilidhani utani lakini aliniambia
kuwa yeye ana UKIMWI tangu
miaka mitano iliyopita na anapenda
tu ngono maana hawezi kuacha.
Nililia sana na baada ya wiki moja
baadae nikaenda kupima na
kukutwa nina ugojwa ambao
niliusikia tu kwa watu na chanzo
cha yote ni pombe, kupenda
starehe,disko na upagani
unaotusumbua wanadamu wengi.
Nilikua na UKIMWI na kwa hasira
maana mpenzi wangu alihamia
Arusha huku akisema neno moja la
mwisho kwamba ”shetani
amemtuma kuwaambukiza
wanadamu UKIMWI”
Sikujua, sikujua, sikujua,
sikujuaaaaaaaaa, basi tu ooh YESU
nihurumie mimi leo.Nilibebeshwa
mzigo ambao haukunistahili mimi.
Hata leo hua najiuliza kwamba
nilijitunza kwa miaka 23 yote lakini
pombe na huyu wakala wa shetani
wamenifanyia hivi. Baada ya kujua
nina UKIMWI na hali hiyo
nikaikubali na kulikua na kundi
kubwa sana la wanaume ambao
walikua wamewahi kunitongoja na
niliwakataa sana kwa sababu hii
niliwakubali ili nami nife na wengi.
Nilianza kumkubali kila mmoja na
kuna baba mmoja ambaye ana
wake 3 niliwahi kumtukana sana
kipindi cha nyuma kila
aliponitongoza
lakini wakati huu nilimkubali na
hakuamini na tukafanya ngono tena
bila kinga na akaniaachia pesa laki
6 kama zawadi ya kumkubali
kumbe naye hakujua kuwa
namwambukiza na hata leo hua
nawahurumia tu wale wake zake
ambao wana UKIMWI uliotoka
kwangu.
Kiukweli tangu may 2009 hadi 2012
nimeshatembea na wanaume zaidi
1500 maana ilifika kipindi nala na
wanaume 3 kwa siku na lengo
langu niwakomeshe kama mimi
nilivyokomeshwa na nina uhakika
kutokana na mimi
wameambukizwa UKIMWI
wanadamu zaidi ya 10,000 na hili
tangazo la ”TUKO WANGAPI” huwa
linaniliza kila siku maana hata
mimi najua kabisa nilianzisha
mtandao kama huo wa ngono kwa
idadi kubwa sana ya watu.
Nimeokoka miezi 7 iliyopita na
siku naombewa nilikutwa na
mapepo mengi sana na hata
waombeaji wakashangaa. Ningejua
ningeokoka tangu nikiwa na miaka
5 lakini ndio hivyo sina jinsi wala
uwezo wa kubadirisha hali hiyo.
Na naomba kila atakayesoma
ujumbe huu ajue kuanzia leo kuwa
pombe ni dhambi pia kwenda disko
ni dhambi,kuuza pombe ni dhambi
na kila kichochoe chochote cha
dhambi ni dhambi. Hadi sasa mtu
yeyote hawezi kujua kama nina
UKIMWI na sijui MUNGU ana
mpango gani na mimi maana
kwake yote yanawezekana.
Nauamini uponyaji wake na
sijawahi kutumia ARV hata siku
moja na afya yangu iko sawa tu na
huwezi hata wewe kujua kama
uovu huu nimefanya mimi.
Ndugu zangu kama una UKIMWI
nenda kanisani ukaombewe na
kama una akili mpe YESU maisha
yako maana pia baada ya kifo ni
hukumu. Yasalimishe
maisha yako kwa YESU na
usiambukize wengine tena.
Mimi tangu niokoke sijawahi
kufanya mapenzi tena na sitafanya
hivyo wala sitaolewa na mtu yeyote
maana yatosha kwa uovu niliofanya
na hadi sasa wapo ninaowajua zaidi
ya 15 wameshafariki na
nilihudhulia misibani huku nikijua
kabisa chanzo ni mimi.
Mwisho nawashauli wababa
kulidhika na wake zao na wamama
pia lidhikeni na waume zenu, vijana
ambao hamjaoa wala kuolewa
subiri hadi utakapooa au kuolewa
na kabla ya kuolewa au kuoa
kapimeni kwanza kwani wenye
UKIMWI ni wengi kuliko
unavyozani.
Fuata unachofundishwa kanisani na
pia soma BIBLIA na uwe
mtakatifu.
MUNGU akubariki
Ni mimi Jane, Mwenge, Dar es
salaam Tanzania

Story isiyofikirika upuuzi mtupu.
 
Kiukweli tangu may 2009 hadi 2012
nimeshatembea na wanaume zaidi
1500
maana ilifika kipindi nala na
wanaume 3 kwa siku na lengo
langu niwakomeshe kama mimi
nilivyokomeshwa

Data
Duration:3yrs 8months(maximum)=366days*(11/3)yrs=1342days
TOTAL MEN(VICTIMS-MINIMUM NO.)=1500
MEAN=1500/1342=1.111~1man/day
.:.the stats seems logical...
Ni mimi Jane, Mwenge, Dar es
salaam Tanzania

bnf=jane???!!!........with that layout...I hope its copy and paste from undisclosed source
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom