Ujumbe wa Jane wa Mwenge kwa mlio lala nae

Ujumbe wa Jane wa Mwenge kwa mlio lala nae

Status
Not open for further replies.
ukimwi kwa vpimo vya kawaida ni miezi 3 baada ya kuambukizwa si chini ya apo

acha kujipa moyo its with in three months for window piriod ata just a week its possible.kapime acha uoga mkiambiwa ukwel mnaleta zenu
 
pole jane na hongera kumpokea yesu,kama kwel unamuamin yesu ata UKIMWI utapona yesu ajasema ukimwi siuwez nijust ugumu wa mioyo yetu nikiwa mzumbe kuna dada aliombewa alishalazwa kwa ukimwi na baadae akawa negative just soma yeremia32:27
 
hadithi zingine ! uambukizwe ukimwi leo baada ya wiki 2 kwenye damu uonekane dah... haya ma doctor waje watuchambulie vizuri ukimwi unavyoambukiza. ingekua hivi, si ingekua kiama tayari.

inategemea na aina ya kipimo alichotumia
 
Karibu tena Dada Jane maana umekumbuka shuka kumekucha....umeokoka baada yakuona umeungua ...weka picha yako tukuone maana mna majina mengi nyie usije ukawa ndo yule uliyenidanganya unaitwa ashurA pale mwenge.....kama kweli umeokoka na umetubu tupia picha yako tuthibitishe maana 5% ya jf member wata kuwa wamehucka na hili
 
Mimi ni Jane naishi mwenge Dar es salaam naomba utalifuta jina la baba yangu maana sitaki liwe kwenye jf watu watanijua na kuniangamiza maana nimeshawaangamiza wengi sana kwa UKIMWI ila mengine yote usifute hata moja ili dunia ijue tu japokua mimi nitakufa kwa huu ukimwi nilionao.

Nilizaliwa mkoa wa Dodoma na nilishi vizuri tu tangu utotoni na hata sikujihusisha na ngono hadi nilipomaliza form 4 mwaka 2006 baada ya kumaliza nilikuja hapa Dar kuishi kwa mama mdogo aliyeolewa hapa Mwenge.

Nilipata marafiki wengi tu na kuna kijana mmoja alinitongoza kwa muda mrefu sana na siunajua vijana wengi hutumia muda mrefu kutongoza ili msichana unadhani kwamba labda huyo anakupenda kumbe anataka tu ngono na wadada wengi sana hudhani kufuatiliwa kwa muda mrefu na mvulana basi huyo yuko serious kumbe hakuna lolote.Nilimkubalia tukawa wapenzi ila nilikataa kuhusu kufanya mapenzi maana anayekupenda kiukweli sio uongo lazima asitake ngono kabla ya ndoa.

Kwa miezi kama 5 hadi 6 aliniambia kuhusu kufanya mapenzi nilikataa alitumia mbinu nyingi sana kwa kunibembeleza na hata kulia mbele yangu ili tufanye tu mara moja ila nilikataa, alisema atavumilia hadi siku ya ndoa yetu ambapo tulipanga kuoana mwaka sept 2009.

Siku moja aliniambia twende kwenye kumbi za starehe na mimi kwa sababu ya upagani na kumwamini pia kwa sababu nampenda nilikubali tulienda huko na kulikua na bendi fulani maarufu ya mziki wa dansi ilikua inatumbuiza.

Tulitafuta sehemu na kukaa na mpenzi wangu akaagiza pombe alianza kunywa huku akinionjesha, nilikataa kwa sababu nilikua sijawahi kunywa pombe katika maisha yangu yote, hata sijui alinishawishi vipi nilijikuta nakunywa kidogo kidogo na kwa kuwa tulikaa pale kwa muda zaidi ya masaa 5 nadhani nikunywa kama bia 3 au 4 japokua nilikua nakunywa kidogo kidogo tu tena kwa kunywesha na mpenzi wangu maana nikama nikua nanyweshwa kila baada kama ya dakika 25 ndipo nakunywa mara moja na sikujuia kama nakunywa pombe ila niliihisi tu naonja ili kumlizisha mpenzi wangu.

Ilipofika saa 10 alfajiri nilihisi usingizi na pia nilijiona wa tofauti najua nililewa hata kama sikujua kama nimelewa maana nakumbuka tulitoka pale huku amenishika mkono huyo mpenzi wangu. Tulikodo tax na kuondoka na siku hiyo aliniambia twende kwake alikokua amepanga chumba maana tulikua na usingizi sana nilikubali huku nikidhani hatuwezi kufanya mapenzi.

Tulifika salama na kuingia ndani ukweli pombe ni kichocheo cha ngono na ningekua mimi ndio Raisi wa Tanzania ningefunga bar zote.

Nilijikuta natamani kufanya mapenzi na huyu mpenzi wangu hata alikua hana nia maana alijua atanichukiza sana na uhusiano ungekufa siku hiyo lakini kwa sababu ya pombe nilimwambia siku hiyo tufanye kidogo maana mwili wangu unataka.

Ni kweli siku hiyo kwa sababu ya pombe nilifanya mapenzi na huyo mpenzi wangu na baadae akanipeleka nyumbani baada ya wiki mbili maana tulikaa wiki mbili bila kuonana alikuja na kunieleza habari ambayo sikuihitaji katika maisha yangu maana nilikua nasikia tu kwa watu wengine lakini sio kwangu alisema "JANE ISHI KWA MATUMAINI KUANZIA SASA" Nilidhani utani lakini aliniambia kuwa yeye ana UKIMWI tangu miaka mitano iliyopita na anapenda tu ngono maana hawezi kuacha.

Nililia sana na baada ya wiki moja baadae nikaenda kupima na kukutwa nina ugojwa ambao niliusikia tu kwa watu na chanzo cha yote ni pombe, kupenda starehe,disko na upagani unaotusumbua wanadamu wengi.

Nilikua na UKIMWI na kwa hasira maana mpenzi wangu alihamia Arusha huku akisema neno moja la mwisho kwamba "shetani amemtuma kuwaambukiza wanadamu UKIMWI" Sikujua, sikujua, sikujua, sikujuaaaaaaaaa, basi tu ooh YESU nihurumie mimi leo.Nilibebeshwa mzigo ambao haukunistahili mimi.

Hata leo hua najiuliza kwamba nilijitunza kwa miaka 23 yote lakini pombe na huyu wakala wa shetani wamenifanyia hivi. Baada ya kujua nina UKIMWI na hali hiyo nikaikubali na kulikua na kundi kubwa sana la wanaume ambao walikua wamewahi kunitongoja na niliwakataa sana kwa sababu hii niliwakubali ili nami nife na wengi.

Nilianza kumkubali kila mmoja na kuna baba mmoja ambaye ana wake 3 niliwahi kumtukana sana kipindi cha nyuma kila aliponitongoza lakini wakati huu nilimkubali na hakuamini na tukafanya ngono tena bila kinga na akaniaachia pesa laki 6 kama zawadi ya kumkubali kumbe naye hakujua kuwa namwambukiza na hata leo hua nawahurumia tu wale wake zake ambao wana UKIMWI uliotoka kwangu.

Kiukweli tangu may 2009 hadi 2012 nimeshatembea na wanaume zaidi 1500 maana ilifika kipindi nala na wanaume 3 kwa siku na lengo langu niwakomeshe kama mimi nilivyokomeshwa na nina uhakika kutokana na mimi wameambukizwa UKIMWI wanadamu zaidi ya 10,000 na hili tangazo la "TUKO WANGAPI" huwa linaniliza kila siku maana hata mimi najua kabisa nilianzisha mtandao kama huo wa ngono kwa idadi kubwa sana ya watu.

Nimeokoka miezi 7 iliyopita na siku naombewa nilikutwa na mapepo mengi sana na hata waombeaji wakashangaa. Ningejua ningeokoka tangu nikiwa na miaka 5 lakini ndio hivyo sina jinsi wala uwezo wa kubadirisha hali hiyo. Na naomba kila atakayesoma ujumbe huu ajue kuanzia leo kuwa pombe ni dhambi pia kwenda disko ni dhambi,kuuza pombe ni dhambi na kila kichochoe chochote cha dhambi ni dhambi. Hadi sasa mtu yeyote hawezi kujua kama nina UKIMWI na sijui MUNGU ana mpango gani na mimi maana kwake yote yanawezekana.

Nauamini uponyaji wake na sijawahi kutumia ARV hata siku moja na afya yangu iko sawa tu na huwezi hata wewe kujua kama uovu huu nimefanya mimi. Ndugu zangu kama una UKIMWI nenda kanisani ukaombewe na kama una akili mpe YESU maisha yako maana pia baada ya kifo ni hukumu. Yasalimishe maisha yako kwa YESU na usiambukize wengine tena.

Mimi tangu niokoke sijawahi kufanya mapenzi tena na sitafanya hivyo wala sitaolewa na mtu yeyote maana yatosha kwa uovu niliofanya na hadi sasa wapo ninaowajua zaidi ya 15 wameshafariki na nilihudhulia misibani huku nikijua kabisa chanzo ni mimi.

Mwisho nawashauli wababa kulidhika na wake zao na wamama pia lidhikeni na waume zenu, vijana ambao hamjaoa wala kuolewa subiri hadi utakapooa au kuolewa na kabla ya kuolewa au kuoa kapimeni kwanza kwani wenye UKIMWI ni wengi kuliko unavyozani.

Fuata unachofundishwa kanisani na pia soma BIBLIA na uwe mtakatifu.

MUNGU akubariki Ni mimi Jane, Mwenge, Dar es salaam Tanzania
 
hadithi nyingine bwana! lakin YESU NI BWANA wacha iwe hivyo.
 
Huyu Jane, mbona uzi wake uko hapa JF tangu mwaka jana?
Topic: UJUMBE WA JANE WA MWENGE KWA MLIO LALA NAYE.
 
Uzi wa Jane alishakuwepo JF muda sema hii habari ni vizuri iwepo kila mara kutuweka alert na VVU. Tumekwisha.
 
Ukimwi after 1 week..?!

Ametolewa mapepo mangapi vileee ?! Lakini bado analo pepo la uongo. Aseme labda ukimwi aliupata kabla ya huyo x bf wake ataeleweka. Ama aseme aliamua kutudanganya na pepo hilo aliosalia nalo..EVEN DNA PCR CAN NEVER DO THAT PERFECTLY.
MT TAKE:Ndugu anza ARV. Tumia maarfa ambayo Mungu ametupa wanadamu. UKIMWI SIO ISHU NDOGO ILA PIA SIO ISHU KUBWA KAMA UNAVYOTAKA WATU WAIBEBE.HUO NI UNYANYAPAA.
 
Nani akupe Fedha Halali kwa Malipo ya Shilingi Laki Sita maisha haya?

NO THANK YOU.
 
Ametolewa mapepo mangapi vileee ?! Lakini bado analo pepo la uongo. Aseme labda ukimwi aliupata kabla ya huyo x bf wake ataeleweka. Ama aseme aliamua kutudanganya na pepo hilo aliosalia nalo..EVEN DNA PCR CAN NEVER DO THAT PERFECTLY.
MT TAKE:Ndugu anza ARV. Tumia maarfa ambayo Mungu ametupa wanadamu. UKIMWI SIO ISHU NDOGO ILA PIA SIO ISHU KUBWA KAMA UNAVYOTAKA WATU WAIBEBE.HUO NI UNYANYAPAA.

unaweza kugundulika na maambukizi ya vvu ndani ya masaa 72 baada ya maambukizi kinacho julikana kwa jina la PCR,kama mlikuwa hamjui hilo basi mlijue kuanzia sasa na kinapatikana mahospitalini ingawa gharama ya kuata kipimo hiki ni zaidi kidogo ya ile ya kawaida.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom