Ujumbe wa Freeman Mbowe wabadili wengi Houston | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ujumbe wa Freeman Mbowe wabadili wengi Houston

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkwawa, Aug 30, 2012.

 1. Mkwawa

  Mkwawa JF-Expert Member

  #1
  Aug 30, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 195
  Trophy Points: 160
  Mwenyekiti wa Taifa Chadema Bwana Freeman Mbowe akiwa ameongozana na Mbunge wa mbeya mjini bwana Joseph Mbilinyi (Sugu) wametembelea jiji la Houston Texas USA kuanzia tarehe 24 hadi 26 August. Ujio huu ni mwaliko wa Tawi la Chadema Houston TX .

  Tawi la Chadema Houston linaonekana kuwa tishio kwa uhai wa CCM sio Houston pekee bali USA. Wanachadema wa Houston ambao ni wengi wanaojiamini, wenye malengo na nia ya dhati kuikomboa Tanzania kisiasa, kiuchumi na kijamii wamekuwa mstari wa mbele kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya kiuchumi nchini Tanzania kwa kushiriki moja kwa moja.

  Ujio huu wa Mbowe ambao uliingiza wanachama wapya zaidi ya 100 kwenye idadi ya wanachadema wa Houston, ulifana sana. Mkutano huu uliofanyika kwenye hotel ya Marriot Westchase Houston TX ulifanyika kwa utulivu na furaha kubwa sana.

  Mkutano huu ulihudhuriwa na watanzania wengi na kuvunja rekodi ya mkutano wowote wa kisiasa ambao umewahi kufanyika Houston TX kwa historia ya uwepo wa Watanzania jijini hapa.

  Mwenyekiti Mbowe akiwa anajiamni aliweza kuwafanya Watanzania kutokwa na machozi kwa jinsi alivyokuwa akielezea ugumu wa maisha, ubovu wa elimu, afya, barabara nk waliyonayo/walivyonavyo watanzania kila siku. Mwenyekiti aliwaasa watanzania kuacha kulalamika badala yake kuwa chanzo cha ufumbuzi kwa kushirikiana na Chadema.

  Mwenyekiti aliwaambia Watanzania hawa kuwa Chadema inawahitaji Diaspora kwa uwingi wao ili kupeleka nchini ujuzi wao, elimu, utamaduni wa kuwajibika, kuaminiwa, na kila chema walichojifunza kutoka nje. Bwana Mbowe aliwahakikishia watanzania kuwa chadema kinaingia ikulu mwaka 2015 kwani kinafanya na kimefanya maandalizi ya kutosha.

  Wakiwa na hamu ya kushiriki moja kwa moja kusaidia mabadiliko haya ya kisiasa na kiuchumi Tawi la Chadema Houston liliahidi kutoa pikipiki mia ishirini na sita (126), gari la kampeni na vifaa mbali mbali vya computer utaalamu na wataalamu wake kutumika katika njanja mbali mbali ili kusaidia chama na watanzania kwa ujumla.

  Mbunge wa Mbeya Joseph Mbilinyi kwa upande wake alisema, Chadema inawataka na kuwahitaji sana, inawathamini sana diaspora na wakazi wa Houston kama watanzania wote ndio maana imewafuata. Alisema, Chadema hakitaki kumwacha mtu yeyote nyuma kwenye kujenga nchi hususani pale itakapochukua dola 2015.

  Akiongea kwa kujiamini Sugu alisema anajua kazi kubwa iliyofanywa na watanzania na sasa walioko nje nao wanaletewa neno la ukombozi kwa ajili ya nchi yetu.

  Naye Mwenyekiti wa Tawi Bwana Fue Fue akiongea na wananchi aliwaasa kuwa wasiwe waoga kwani makamanda wa Chadema wamepitia mengi ila bado wanasonga mbele. Aliwaambia watanzania wenzake kuwa hakuna wa kuisaidia Tanzania isipokuwa Watanzania wenyewe. Alisisitiza ujasiri, kujiamini na kufanya kwa vitendo. Akiongea kwa msisitizo alisema uongozi ulioshindwa hauwezi tena kuaminiwa, kwa miaka 50 sasa serikali ya CCM imeshindwa na imeishiwa ubunifu hivyo kuwa na ugumu wa kuweza hata kutambua matatizo halisi ya Mtanzania. Lazima kubadili uongozi mzima ili kuweza kusonga mbele kiuchumi, ni kazi yetu kufanya hivyo na wajibu wetu kuindoa CCM madarakani, alisema bwana Fue Fue

  Mbowe aliwaaga watanzania kwa kuwaambia Chama kina wahitaji na kinathamini sana mchango wao.

  Watanzania wengi walimsifia Mbowe kwa uwezo wake wa kuongea kujenga hoja na kujibu maswali ya Watanzania na kumaliza kiu yao. Mkutano huo ulichukua takribani masaa manne.

  Majibu ya watanzania ni kuwa wengi wamehamasika na kukubali kushiriki moja kwa moja kwenye kuikomboa nchi.
   
 2. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #2
  Aug 30, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Asante kwa taarifa mkuu...
   
 3. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #3
  Aug 30, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Ahsante kwa kutujuza yaliyojiri mdau!! Ni ajabu kusikia mtanzania mwingine anakuja hapa akijaribu kufumba macho kusahau mamilioni ya watanzania wanatuhitaji sie ambao angalau tumeweza kubofya keyboard ili kuwapa matumaini.
   
 4. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #4
  Aug 30, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Nilisha sema na leo narudia tena! Hakuna mwenyekiti wa chama chochote cha siasa kwa sasa anae tema madini mdomoni akiongea kama kamanda Mbowe! Jamaa anaongea issues zinazogusa watanzania. Asie amini atafute audio ya speech yake pale Serena Hotel au hata akiwa anahojiwa.

  Kamanda amekomaa ajabu ya maulana!
   
 5. Steven Robert Masatu

  Steven Robert Masatu Verified User

  #5
  Aug 30, 2012
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 2,395
  Likes Received: 729
  Trophy Points: 280
  hongera sana kamanda kwa kutupa taarifa. mh mbowe ni kamanda sana,speech zinagusa watanzania wote achana na hawa wenzetu speech zao zinagusa udini,ukabila na ukanda. wonderfull singo zao zote za kutugawa zinakwama. devide and rule,if u dont convice them confuse them hizi ni technic za kizaman sana but now hawa magamba bado wanaaply.

  aluta continua  sent from my htc chacha via jamiiforums
   
 6. Mkwawa

  Mkwawa JF-Expert Member

  #6
  Aug 30, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 195
  Trophy Points: 160
  mkubwa umesema kweli tupu
   
 7. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #7
  Aug 30, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Matawi nje ya nchi??

  Bado huwa sielewi sana mantiki yake.
   
 8. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #8
  Aug 30, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Utaelewa tu mkuu! Ni kutwanga kotekote Tanzania na Ulaya! Huoni kuwa hizo pikipiki 126 zitasadia sana kwenye M4C? Stay tuned!
   
 9. S

  Sipendi Ubepari JF-Expert Member

  #9
  Aug 30, 2012
  Joined: Jan 12, 2012
  Messages: 249
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Höngera CDM,,, Hongera Watanzania Wote Wapendamageuzi ndani na nje ya nchi.
   
 10. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #10
  Aug 30, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,785
  Likes Received: 2,395
  Trophy Points: 280
  vikao vya wana ccm kwa sasa ni kuilaumu chadema tuu!huu moto wa M4C hawakuutegemea!MBOWE kafanya mabadiliko makubwa
   
 11. M

  Molemo JF-Expert Member

  #11
  Aug 30, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Asante Mbowe,asante sana baba....
   
 12. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #12
  Aug 30, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Taratibu. Siku moja utaelewa tu.
   
 13. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #13
  Aug 30, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Kuna lifala moja eti linasema Mbowe anauzoefu wa kuongoza Madisco kanichefua sana leo.

  Mbowe ni Kamanda na ninachomkubali hanaga muda wa kuzunguzia mipasho wala kejeli.
   
 14. only83

  only83 JF-Expert Member

  #14
  Aug 30, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Kamanda Mbowe ni mjengaji mzuri wa hoja, na kwa siku za karibuni amekuwa ni mwalimu mzuri kwa wabunge wengi na vijana wa CHADEMA.
   
 15. kinya

  kinya JF-Expert Member

  #15
  Aug 30, 2012
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 483
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Jembe limepitia mengi kama dhahabu kadiri inavyo unguzwa motoni ndivyo ubpora wake unavyo ongezeka
  wacha wakina 6 waweseke huu moto si mchezo
   
 16. Mkwawa

  Mkwawa JF-Expert Member

  #16
  Aug 30, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 195
  Trophy Points: 160
  Tanzania sio kisiwa ina watanzania wengi wanaoishi ndani ya nchi na wengine wachache wametapakaa duniani. Watanzania waliopo nje wanafaida kubwa sana kwa taifa letu, hawa Watanzania wenzetu huko walipo ama wanasoma, wanafanyakazi, au biashara vile vile wanafamilia zao.

  Manufaa yao kwetu sisi, kila mtanzania anafamilia yake Tanzania, mara nyingi huwatumia fedha ndugu zao za kigeni kama sikosei kwa miaka miwili iliyopita Watanzania hawa walituma zaidi ya dola za kamarekani milioni mia sita zikaingia kwenye mzunguko wetu kama foreign income, kupitia ndugu, jamaa, au biashara zao.

  Watanzania hawa wengi wanafanyakazi kwenye viwanda na makampuni yaliyoendelea hivyo kuchota utaalamu na vitendo. Watanzania wanapata elimu na kujifunza mambo mbali mbali amabyao ni muhimu kwa kukua kwa Taifa lolote duniani.

  Mapinduzi ya kiuchumi ya nchi kama Singapore, Italy, Israel, Ghana nk ni Diaspora zao.

  Tukiwatumia Diaspora wetu vizuri tutasonga mbele. tutoe mawazo mgando ya CCM kuwaogopa kwani wanaogopa changamoto zao.
   
 17. MKANKULE

  MKANKULE JF-Expert Member

  #17
  Aug 30, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 422
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Matawi nje ya nchi maana yake ni kwamba chadema kwa kuwa ni chama makini kinahakikisha kinawawekea uzalendo watanzanzania walioko nje ya nchi,wale waliokata tamaa baada ya kuona uozo wa uongozi legelege wa chama cha magamba,kuwapa tumaini jipya ili waisaidie nchi yao kwa kutumia taaluma zao waliozopata wakiwa nje ziwasaidie na ndugu zao watanzania, watumie pesa zao kwa kusaidia mabadiliko makubwa yanayoenda kutokea. Ukumbuke kuwa chadema sio omba omba kama chama cha magamba ambao wanaenda kuwakenulia meno watu weupe ili wawasaidie jinsi ya kupora pesa za walipa kodi na kwenda kuziweka uswisi. Hii ndio maana halisi ya kuanzisha matawi nje ya nchi. ili kuhakikisha kuwa roho ya vuguvugu la mabadilikoni inaambukizwa dunia nzima na wa tz wenzetu watusaidie kuitangazia dunia kuwa tz na wa tz wamechoshwa na magamba. umeelewa kaka au niendeleee kutoa darasa la bure hadi unielewe.
   
 18. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #18
  Aug 30, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  At least hapa naona kuna diaspora wanaojitambua. Kuna wengine nimesoma mahali kwamba wanatekwa na ccm kwa kumtumia diamond na bia na nyamachoma.
  Kazi nzuri sana kamanda Mbowe endelea kuwafundisha siasa na uzalendo.
   
 19. Chilisosi

  Chilisosi JF-Expert Member

  #19
  Aug 30, 2012
  Joined: Oct 19, 2008
  Messages: 3,055
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Halafu anapoongea huwa hatoki povu kama magamba
   
 20. Chilisosi

  Chilisosi JF-Expert Member

  #20
  Aug 30, 2012
  Joined: Oct 19, 2008
  Messages: 3,055
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  hahah muraaa,
  amang'ana gasarikiye,
  huku UK kuna wengine bado wanadanganywa na nyama choma lakini najua wataeleimika tu
   
Loading...