Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,360
- 33,204
Wana Bahati sana hawa Wafanyakazi wazembe wa Bandari mjini Dares-Salaam. Laiti kama ningelikuwa ndio mimi Rais wa nchi ninge wasimamisha kazi na huku uchunguzi unafanyika na ikibainika maneno anayo yasema huyu mfanya biashara kijana ni maneno ya ukweli basi ningeliwafukuza kazi wote wanao husika na kumpa onyo kali Waziri wa Mawasiliano na uchukuzi kwa kutofanya kazi yake vizuri.
Inaonyesha Waziri Muhusika nae pia hawajibiki ipasavyo kwani anaonyesha nae Waziri Mhusika ni mzembe wa kazi aliyopewa na Mheshimiwa Rais Mama Samia.
Kwani itafika wakati wafanya biashara watahamia bandari ya Mombasa kutoa mizigo yao wakati Bandari yetu haitpata wateja na Serikali itapata hasara kubwa kwa kukosa kufanya biashara na wafanya biashara .