Ujumbe kwa wanaume

Ujumbe kwa wanaume

Sasa si unipe hilo andiko? Duuh waalimu wana kazi lete andiko mkuu

Kumbu 21;15
Akiwa mtu yuna wake wawili, mmoja ampenda, mmoja hampendi, nao wamemzalia watoto, ampendaye na asiyempenda wote wawili; na yule mzaliwa wa kwanza akiwa ni wa mke asiyependwa;
If a man have two wives, one beloved, and another hated, and they have born him children, both the beloved and the hated; and if the firstborn son be hers that was hated:
 
Mkuu hebu kasome kitabu cha Mwanzo Sura ya 16:4-6. Kisha soma mwanzo hiyo hiyo sura ya 26:34-35. Halafu urudi hapa tufunge mjadala km ulivyosema.
Ila wewe jamaa ni mgumu kuelewa aisee nimekwambia nipe andiko ambalo Mungu ameruhusu usinipe mifano ya watu sasa Ibrahim ndo Mungu? Na nimetoka kukwambia hapo juu kuwa hao kilichowafanya wabarikiwe ni imani zao za kuhamisha milima na mioyo yao ya kukiri makosa na kutubu Ibrahim hadi leo anaitwa baba wa imani na hicho ndicho kilichofanya Mungu ampende na siyo kuzaa na huyo kijakazi na kwanza umesoma baada ya hapo nini kiliendelea au umeishia hapo hapo tu? Hapo umefeli jaribu tena
 
Kumbu 21;15
Akiwa mtu yuna wake wawili, mmoja ampenda, mmoja hampendi, nao wamemzalia watoto, ampendaye na asiyempenda wote wawili; na yule mzaliwa wa kwanza akiwa ni wa mke asiyependwa;
If a man have two wives, one beloved, and another hated, and they have born him children, both the beloved and the hated; and if the firstborn son be hers that was hated:
Duuh aisee mkuu nimekwambia nipe andiko ambalo Mungu karuhusu hapo sijaona sehemu aliyoruhusu bali ameongelea kama imeshatokea yaani amewapa mbinu ambao tayari sasa ndo wameshakuwa na wake wawili ila hajaruhusu yaani bado mnarudi kule kule kwa kina Ibrahim na Solomon nipe andiko mkuu siyo mifano ya watu wale ni binadamu siyo malaika
 
Kutokuwa sawa na wanawake na kuwadharau wanawake ni vitu viwili tofauti binadamu hatuko sawa na Mungu lakini Mungu hajawahi kutudharau sasa niwashangae nyie wanaume sijui mnajihisi ni akina nani haswa kutudharau wanawake kwa kisingizio cha kuwa hatuko sawa tuko chini yenu hata Mungu anawashangaa
Utakua unachuki na wanaume wewe, hata muundo wa tendo la ndoa/ngono linaonesha hatuko sawa
 
And here comes another fool hivi umeielewa hiyo post yangu au umekurupuka tu? Tena naona kama wewe ndo umejibu kwa chuki na mihemko zaidi try again
 
Duuh aisee mkuu nimekwambia nipe andiko ambalo Mungu karuhusu hapo sijaona sehemu aliyoruhusu bali ameongelea kama imeshatokea yaani amewapa mbinu ambao tayari sasa ndo wameshakuwa na wake wawili ila hajaruhusu yaani bado mnarudi kule kule kwa kina Ibrahim na Solomon nipe andiko mkuu siyo mifano ya watu wale ni binadamu siyo malaika

Mkuu ukiona Mungu kalitolea maelezo jambo fulani kulisapoti ujue tayari kaliruhusu mbona unashindwa kuelewa mantiki ya teolojia.

Ili uone kama karuhusu ndio maana alitoa sheria isemayo Kuhani au askofu awe mume wa Mke mmoja. Kumaanisha wasio maaskofu na makuhani wanayoruhusa ya kuoa wake zaidi ya mmoja.

Sasa unakwama wapi. Mtu akitaka kuoa wake wengi anaruhusiwa kwa utaratibu maalumu ili kuepusha zinaa.

Haya embu nipe andiko linalosema mtu awe na mke moja mbali na lile linalomhusu Askofu.
 
Mkuu ulichokisema ni umezungumzia upande mmoja nafikiri pamoja na mwisho wa ushauri wako umezungumzia upande mwingine ila ungeshusha NONDO pande zote ili kila atakayesoma imguse yeyote yule... Unless otherwise awe hana jinsia kati ya hizo zote mbili... Asante ni mtazamo wangu tu....
 
Ila wewe jamaa ni mgumu kuelewa aisee nimekwambia nipe andiko ambalo Mungu ameruhusu usinipe mifano ya watu sasa Ibrahim ndo Mungu? Na nimetoka kukwambia hapo juu kuwa hao kilichowafanya wabarikiwe ni imani zao za kuhamisha milima na mioyo yao ya kukiri makosa na kutubu Ibrahim hadi leo anaitwa baba wa imani na hicho ndicho kilichofanya Mungu ampende na siyo kuzaa na huyo kijakazi na kwanza umesoma baada ya hapo nini kiliendelea au umeishia hapo hapo tu? Hapo umefeli jaribu tena
Mbona umesoma sehemu moja pekee wakati nimekupa vifungu viwili!?? Ngoja nikuongezee upate home work ya kutosha kwa leo. Kuoa wake wengi au kuchepuka kwa mwanaume siyo issue mkuu soma pia hapa.Mwanzo:29:15-35. Yakobo mbali na kuoa mabinti wawili wa labani,lkn bado aliwatafuna hata wafanyakazi wa ndani.
 
Wanatolea mifano ya kina Suleiman kuoa wake wengi bila kujua mwisho wao ulikuwaje wanashikilia hapo tu pa kuoa wake wengi Suleiman alifanya dhambi nyingi siyo uzinzi tu pia aliua baadhi ya ndugu zake ili apate ufalme na kweli Mungu alimbariki akawa mfalme sasa wanataka kusema kwamba kuua siyo dhambi tena kwa sababu tu Suleiman aliua na Mungu akamsamehe? Ni wachache wanaojielewa kama wewe
Yaani dunia hii wanaume wasiochepuka wako wengi tu na wanafurahia nmo wake zao
 
Mwanzo.26:34-35 inazungumza habari za Essau kuoa mke wa pili mbona hujasoma ukiacha hiyo ya ibrahimu!?? Huyo Essau ukisoma huko mbele alioa hadi mke wa tatu. Nimekuwekea hapo usome pia habari za yakobo kuoa mke zaidi ya mmoja.
 
Mkuu ulichokisema ni umezungumzia upande mmoja nafikiri pamoja na mwisho wa ushauri wako umezungumzia upande mwingine ila ungeshusha NONDO pande zote ili kila atakayesoma imguse yeyote yule... Unless otherwise awe hana jinsia kati ya hizo zote mbili... Asante ni mtazamo wangu tu....
Upande niliouzungumzia ni upi?
 
Mkuu ukiona Mungu kalitolea maelezo jambo fulani kulisapoti ujue tayari kaliruhusu mbona unashindwa kuelewa mantiki ya teolojia.

Ili uone kama karuhusu ndio maana alitoa sheria isemayo Kuhani au askofu awe mume wa Mke mmoja. Kumaanisha wasio maaskofu na makuhani wanayoruhusa ya kuoa wake zaidi ya mmoja.

Sasa unakwama wapi. Mtu akitaka kuoa wake wengi anaruhusiwa kwa utaratibu maalumu ili kuepusha zinaa.

Haya embu nipe andiko linalosema mtu awe na mke moja mbali na lile linalomhusu Askofu.
Sasa sikupi andiko bali nakupa maandiko ambayo yanaonyesha kwamba Mungu alitaka ndoa ya mume mmoja na mke mmoja tu

Moja Mungu aliona kwamba si vema Adam awe peke yake akamfanyia msaidizi wake akamlaza usingizi kisha akautoa ubavu wake mmoja na akautumia kumuumba mwanamke mmoja tu naye ni Evah na hakumuongezea mke mwingine

Mbili mwanamume atawaacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe nao watakuwa mwili mmoja kumbuka ni mkewe siyo wakeze

Tatu mwanamume ampende mkewe na mwanamke amtii mumewe kumbuka tena ni mkewe siyo wakeze Nne kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe

Haya hayo yote ni maandiko nimeyatoa kwenye biblia kiufupi vile ambavyo Mungu alimuumbia Adam mwanamke mmoja tu ambaye ni Evah ndivyo alivyotaka ndoa zote ziwe hiyo ya kusema karuhusu makuhani na wachungaji tu ndo uone jinsi gani alivyoweka msisitizo kwamba kuwa na mke mmoja ndo muhimu

Kwahiyo wewe ubavu wako ni mwanamke mmoja tu na siyo zaidi hao wengine utakaowaongeza utakuwa unawadanganya wao na unajidanganya wewe pia na ukibishia hayo maandiko maana yake unabishia kwa jinsia zote mbili na nimekwambia Mungu hawezi kuhalalisha dhambi eti hata ingekuwa imefanywa na nani au na watu wengi kiasi gani yeye siku zote atasimamia amri zake tu
 
Mbona umesoma sehemu moja pekee wakati nimekupa vifungu viwili!?? Ngoja nikuongezee upate home work ya kutosha kwa leo. Kuoa wake wengi au kuchepuka kwa mwanaume siyo issue mkuu soma pia hapa.Mwanzo:29:15-35. Yakobo mbali na kuoa mabinti wawili wa labani,lkn bado aliwatafuna hata wafanyakazi wa ndani.
Daah wewe mkuu hebu endelea tu na mambo mengine maana kile ambacho ninakwambia usifanye ndo unafanya nimekwambia USINITOLEE MIFANO YA BINADAMU WALIOFANYA HIZO DHAMBI NIPE ANDIKO LILILOSIMAMA PEKE YAKE AMBALO MUNGU KARUHUSU KUSALITI NDOA AU KUOA MKE ZAIDI YA MMOJA tukianza kutolea mifano ya kila mtu na dhambi zake tujikuta tunahitimisha kuwa kila kitu siyo dhambi maana pia wapo wanawake walikuwa makahaba na waliolewa na wanaume zaidi ya mmoja
 
Mwanzo.26:34-35 inazungumza habari za Essau kuoa mke wa pili mbona hujasoma ukiacha hiyo ya ibrahimu!?? Huyo Essau ukisoma huko mbele alioa hadi mke wa tatu. Nimekuwekea hapo usome pia habari za yakobo kuoa mke zaidi ya mmoja.
Kwahiyo hao ulionitajia ndo Mungu au? We mbona umekazania mifano ya binadamu hebu lete andiko linaloeleweka bwana acha kumbwelambwela
 
Hebu acha basi kutaka kuleta miujiza hapa..hayo maandiko si yanatoka kwenye Biblia!?? Kwani Biblia si ni kitabu cha Mwenyezi Mungu!?? Kama Biblia inajipinga kwamba kuna sehemu inayohusu binadamu tu na kuna sehemu inayohusu wanadamu tu tuishie hapa. Biblia nzima hakuna mahali hata fungu moja aliloandika Mungu. Biblia yote ni mkusanyiko wa vitabu vilivyoandikwa na wanadamu. Halafu hao wanadamu waliohusika wewe unawakataa unataka andiko la Mungu tuletee basi wewe andiko la Mungu.
 
Hebu soma hiyo post yangu hapo juu nimetoa mifano ya maandiko ambayo yalitolewa na manabii na mitume wa Mungu ambayo ni kama ujumbe ambao walitakiwa waulete duniani kwa wanadamu wengine hata kina Solomon walikuwa ni manabi

Lakini wao kuoa wake wengi haukuwa ujumbe waliotumwa waulete duniani bali hayo yalikuwa ni matendo yao binafsi ambayo yalikuwa ni dhambi na ndo maana walikuja kutubu hizo dhambi tofautisha na kina mtume Paulo ambao walikuja kusambaza injili yaani ujumbe jinsi Mungu anayotaka binadamu waishi
Hebu acha basi kutaka kuleta miujiza hapa..hayo maandiko si yanatoka kwenye Biblia!?? Kwani Biblia si ni kitabu cha Mwenyezi Mungu!?? Kama Biblia inajipinga kwamba kuna sehemu inayohusu binadamu tu na kuna sehemu inayohusu wanadamu tu tuishie hapa. Biblia nzima hakuna mahali hata fungu moja aliloandika Mungu. Biblia yote ni mkusanyiko wa vitabu vilivyoandikwa na wanadamu. Halafu hao wanadamu waliohusika wewe unawakataa unataka andiko la Mungu tuletee basi wewe andiko la Mungu.
Sasa sikupi andiko bali nakupa maandiko ambayo yanaonyesha kwamba Mungu alitaka ndoa ya mume mmoja na mke mmoja tu

Moja Mungu aliona kwamba si vema Adam awe peke yake akamfanyia msaidizi wake akamlaza usingizi kisha akautoa ubavu wake mmoja na akautumia kumuumba mwanamke mmoja tu naye ni Evah na hakumuongezea mke mwingine

Mbili mwanamume atawaacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe nao watakuwa mwili mmoja kumbuka ni mkewe siyo wakeze

Tatu mwanamume ampende mkewe na mwanamke amtii mumewe kumbuka tena ni mkewe siyo wakeze Nne kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe

Haya hayo yote ni maandiko nimeyatoa kwenye biblia kiufupi vile ambavyo Mungu alimuumbia Adam mwanamke mmoja tu ambaye ni Evah ndivyo alivyotaka ndoa zote ziwe hiyo ya kusema karuhusu makuhani na wachungaji tu ndo uone jinsi gani alivyoweka msisitizo kwamba kuwa na mke mmoja ndo muhimu

Kwahiyo wewe ubavu wako ni mwanamke mmoja tu na siyo zaidi hao wengine utakaowaongeza utakuwa unawadanganya wao na unajidanganya wewe pia na ukibishia hayo maandiko maana yake unabishia kwa jinsia zote mbili na nimekwambia Mungu hawezi kuhalalisha dhambi eti hata ingekuwa imefanywa na nani au na watu wengi kiasi gani yeye siku zote atasimamia amri zake tu
 
Hebu soma hiyo post yangu hapo juu nimetoa mifano ya maandiko ambayo yalitolewa na manabii na mitume wa Mungu ambayo ni kama ujumbe ambao walitakiwa waulete duniani kwa wanadamu wengine hata kina Solomon walikuwa ni manabi

Lakini wao kuoa wake wengi haukuwa ujumbe waliotumwa waulete duniani bali hayo yalikuwa ni matendo yao binafsi ambayo yalikuwa ni dhambi na ndo maana walikuja kutubu hizo dhambi tofautisha na kina mtume Paulo ambao walikuja kusambaza injili yaani ujumbe jinsi Mungu anayotaka binadamu waishi
Mkuu hebu acha basi kutulisha matango pori..! Kwenye hilo andiko lako Biblia inasema Adamu na Eva waliwazaa Kaini na Abel. Hebu tuambie wao nao waliumbiwa mwanamke au walioa wapi maana Biblia inataja uzao wao tu au walikuwa wanamgonga mama yao!?? Hebu tuambie Kaini alizaa na nani!??
 
Ninapowashangaa wanawake ni 1. Mnazaa watoto wote,lakini nyie wanawake utasikia watoto ni mwanaume,kwa nini watoto wawe ni mwanaume wakati mmezaa wote? Au ndio namna ya kumshika huyo mwanaume kwamba watoto ni wake? Kama ni wake anawapamba wapi? Mbona mnawaringia wote halafu na mwanamke unasema una watoto kadhaa? Kwa nini usiseme ni watoto wa mwanaume? Wakikua watoto na kuanza kazi mtu wa kwanza kumkumbuka ni mama. Kwa nini mnawavisha kilemba cha ukoka?
 
Zamani watoto wa kike walikuwa hawahesabiki katika uzao wowote ule na ndo maana hata Yakobo anahesabika ana watoto 12 wakati alikuwa na watoto 13 ila yule wa kike Dina hakuhesabika kwahiyo hata kina Adam walizaa watoto wa kike ila hawakuhesabika wala hawakuongelewa kwahiyo probably hao kina Cain na Abel waliwaoa na kuzaa na dada zao

Mungu siyo mjinga kama binadamu kuna vitu Mungu kaviruhusu yeye mwenyewe kupitia manabii na mitume wake kwa kutuhubiria injili na siyo kuangalia matendo yao na ukiangalia Solomon alipozeeka aliandika vitabu vya Mithali na Wimbo Ulio Bora na katika hivyo vitabu vyote hakuna sehemu aliyowaambia watu wengine eti wasaliti ndoa au waoe mke zaidi ya mmoja kama alivyofanya yeye

Zaidi kwenye kitabu cha mithali asilimia kubwa anaelezea anavyojuta na anavyotubu kwa yale yote aliyofanya ujanani ikiwa ni pamoja kuua ndugu zake ili apate ufalme na kusaliti ndoa na kuoa wake wengi na anaelezea alivyongundua kuwa yale yote yalikuwa ni anasa na ubatili na kwenye kitabu cha wimbo ulio bora anaelezea jinsi mume na mke wanavyotakiwa kusifiana katika ndoa

Na unaona dhahiri pale kuwa mume anamsifia mke mmoja na mke anamsifia mume mmoja kwahiyo fuata yale waliyoyahuburi hao mitume na manabii ila yale waliyoyatenda usiyafuate sababu wao nao ni binadamu kama sisi hawakukamilika kila sehemu nao walitenda dhambi na huko baadaye walikuja kutubu hata wao wenyewe hawakuwahi kuwaambia watu wafuate matendo yao bali waliwaambia wafuate maneno yao sasa endeleeni kujidanganya na kudanganyana maana binadamu akitaka lake atalazimisha liwe hata kama ni uongo atajipa moyo kuwa ni ukweli
Mkuu hebu acha basi kutulisha matango pori..! Kwenye hilo andiko lako Biblia inasema Adamu na Eva waliwazaa Kaini na Abel. Hebu tuambie wao nao waliumbiwa mwanamke au walioa wapi maana Biblia inataja uzao wao tu au walikuwa wanamgonga mama yao!?? Hebu tuambie Kaini alizaa na nani!??
 
Mkuu kumbuka mwanamke ndo anawalea wale watoto peke yake hivi unadhani kulea ni kazi rahisi enh? Wanasema kuzaa si kazi kazi kulea mwana wewe uko mbali inaweza ikapita hata wiki haujui wamekula nini na wamevaa nini ila mama yao ndo yupo nao kila siku

Yeye ndo anatakiwa ajue kila siku wanakula nini wanavaa shule wanaendaje na likitokea tatizo yeye ndo wa kwanza kujua sasa mwanaume wewe hakuna unalofanya kati ya hayo basi hata kutuma hela ya matunzo na kuhudumia napo unataka msaidiane nusu kwa nusu mbona wewe haumsaidii kulea nusu kwa nusu?

Na kuhusu wanawake kuwalisha sumu watoto wenu juu yenu hayo pia mnayataka wenyewe siku hizi wanaume wengi mnaona kuzalisha ni sifa na ni kama kumpa adhabu mwanamke aliyekusumbua utasikia mwanaume anasema yule demu alichonifanyia lazima nimzalishe halafu nimuache hapo unategemea nini?

Lazima mtoto wako alishwe sumu tu kuna kitu kinaitwa karma yaani what goes around comes around hiyo ni principle ambayo ipo kwa kila mtu uikubali uikatae kila unachofanya haijalishi ni kizuri au kibaya lazima kikurudie kwa namna moja au nyingine wakati wowote ule sasa nyie wanaume mnayapenda maovu yenu ila matokeo ya maovu yenu hamyapendi

Back
Top Bottom