Ujue Mti chonganishi

Kama ulikuwepo mkuu Nyati!
 
Ni wakati wa kupanda miti yenye kuleta tija. Nyumba sio vizuri ikajazwa miti ya kivuli na mapambo tupu huku wenyewe mna uwanja wa kutosha mnaishia kununua matunda magengeni na juice za mabox. Mimi kwangu mti pekee wa kivuli ni muarobaini tu. Sikutaka uvivu kwenye matunda nimepanda mengi sana ya aina karibia zote.
 
Hongera sana mkuu
 
Asante mkuu nikihamia tu nitakualika uje tule matunda kuna niliyoanza kula
.

Kwa sasa niko bado uswazi ila huwa naenda kuvuna yanayowezekana .
Asante tena ntakuja unisaidie miche ya mitunda ambayo sinayo hapa kwangu
 
Nitakupa ila mimi mingi sana ninaibeba Morogoro. Ilikuwa kila nikienda nabeba miche yangu. Migomba nitakugawia pia kama una eneo la kufaa migomba.
Migomba ninayo aina zote naishi migombani mkuu, napenda matunda hapa mitunda niliyonayo haizidi kumi coz Nina miti ya maparachichi, miembe, machungwa zambarau mananasi mafenesi mapera makomamanga,
Machenza sitafeli sinayo na matunda mengineyo mkuu
 
Migomba ninayo aina zote naishi migombani mkuu, napenda matunda hapa mitunda niliyonayo haizidi kumi coz Nina miti ya maparachichi, miembe, machungwa zambarau mananasi mafenesi mapera makomamanga,
Machenza sitafeli sinayo na matunda mengineyo mkuu

Stafeli ninao na nimeanza kula , mlimao ,mndimu pia. Nilipata miche SUA.
 
Huu mti nmeuontesha lakini zaidi ya watu wawili wananiambia huumti ukiotesha una mikosi, yani hapo nyumbani itakua ni mikosi na ugomvi tuu.

Anaeujue hii habari ya huu mti anieleweshe
 
Huu mti, Mshana Jr alishauelezea sana humu jukwaani. Tafuta thread "mti chonganishi"
 
Huo mti tunaita "Uzazi wa Mpango" sitaki kuamini kama mti wenye mizizi ya kuleta nyufa ni mwaru40.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…