Ngoja niwaibie siri ya enzi zile utotoni; najua wengi humu ni wadogo zangu sana tu, na wengine nii wanangu-stori zao za kileoleo, enzi zetu sisi hata dalalala hazikuwepo unachapa mguu kwenda skuli, au unasubiri kudandia lifti ya karandinga au landrover ya polisi!
Basi zetu ilikuwa kwenda kuogelea Ziwa Tanganyika, kuleee Bangwe, mwanaume umetoka ziwani ukikauka tu unapauka balaaa, na nyumbani wanajua mara1 kuwa ulienda kuogelea.....kibano chake balaa; basi tukagundua kutembea na kipande cha sabuni aina ya MBUNJU mfukoni, mkimaliza kuogelea mnajipakaa povu la sabuni ngozi inakakamaa na kung'aa; hapo basi usiombe ukwaruzwe na kijiti....hahahaaaa!
Enzi za kudoji shule na kuenda kupopoa maembe au kungu kwa kina Manka, hahahaaa, kwenda kuchokoza mbwa kwa "baptist" ahahaaaa! dah, nakumbuka enzi zile ukifanyiwa Birthday mnakunya Vimto na karanga!
Ebanaaaa, nilisahauuu...kupigana vita kwenye msitu wa kule nyuma ya Jeshi karibia na Kigoma Sec (Naskia siku hizi mitaa ile hakuna Msitu tena, ni Majumba tu), basi siku hiyo hamli mnashindia matunda pori na mise kijeshijeshi, kule kulikluwa na kanga wengi sana, mkikuta mtego wa watu umenasa mnaiba na kuchoma!
hhihihiii, eish Kibaba na Mama, basi Amosi (Mfanyakazi wa ndani) ananiambia "Mfanye", mimi sijui hata kufanya naanza kumfanya kinguonguo hahaaa! Enzi zile Mkiona mtu amevaa "Tafu" na Afro Kubwa mnamwita Msela Nondo!
Mojawapo ya mabasi nayakumbuka kipindikile ni Nusu Mkate...hihiiii! Bad Luck sijawahi kukutana na Rafiki yangu wa Utototni hata mmoja, sooooo baad!