Guus
JF-Expert Member
- Jul 16, 2013
- 1,167
- 907
Wiki iliyopita nilikuwa Dodoma (Dodoma Mjini kabisa).
Jioni moja nikachanganya makongoro kwenda kumsabahi rafiki wa muda mrefu mitaa fulani anayoishi, panafahamika kama Iringa Road.
Muda wa kutoka, tutoke na jamaa, shemeji akamkumbusha kuhusu tangazo lililotolewa la uwepo wa mkutano wa mtaa, lililoitishwa na viongozi wa mtaa. Tukakubaliana kwa vile mimi si mkazi, nimuwache yeye aende halafu anikute katika kijiwe fulani cha jirani na wanapoishi, wanapaita Capital Pub.
Jamaa alivyokuja hapo Pub namuona sura imemuiva vibaya, kumuuliza akanieleza hoja iliyowekwa mezani huko kwenye mkutano. Viongozi waliwataarifu wananchi wao, ya kwamba ofisi ya Kata haina majengo ya ofisi, na sasa wamefanikiwa kupata kiwanja hivyo wanataka kujenga jengo la ofisi za Kata.
Wakawaainishia gharama walizofanyiwa makadirio na Injinia wao, kisha wakagawanya kwa kila kaya na kutaka kila kaya ichangie kiasi cha Sh. 43,000/-. Jamaa akaniambia watu wakajaribu kujadili kwa hoja tofauti, lakini mwisho ikahitimishwa kuwa viongozi wa Mitaa wataratibu ukusanyaji huo wa michango.
Nikamuuliza jamaa, wenzetu ninyi katika Kata yenu hamlipi kodi Serikalini?! Akanijibu ndiyo hoja kubwa iliyokuwapo kwenye mkutano, lakini viongozi wao waliwaambia waanze mdogomdogo, wasiwe wanaitegemea sana Serikali!
Swali ambalo nimebaki nalo ni kuwa, sasa kama hadi ofisi za serikali nazo wananchi wanatakiwa kuchangia kazi ya kodi ni nini!!??