Nondo 3 zinafaa kabisa, lakini ziwe za mm 12, asije kukushauri uweke mm 10 hazitafaa. Hizo za mm 12 azisuke katika umbo la pembe 3 (yaani mbili chini kwenye base ya linter na moja juu, yaani ikae umbo la pyramid) lengo hapa ni kupata balance), fundi anaweza akazisuka na binding wire au anaweza asisuke pia; inategemea na ustadi wake katika kuzipanga inavyotakiwa. Mimi nimejenga nyumba yangu kubwa tu ya room 3, sebule kubwa tu, dining, jiko na store; na linter yake nimetumia nondo 3 za mm 12, juu ya linter nimeweka tofali za course 3, so naelezea kitu nnachokifahamu.