Ujenzi wa barabara Arusha nani apewe sifa?

Ujenzi wa barabara Arusha nani apewe sifa?

Uongozi uliopo madarakani upewe sifa, kwakuwa sio kila anayepeleka maombi huko WB anakubaliwa wengine wanapigwa chini maana funds zao ni limited na mahitaji ni unlimited after all mkopo hapewi mtu asiyeweza kurejesha.
 
CDM wanahitaji pongezi, mabadiliko haya yameletwa na sera/uongozi thabiti wa CDM wakishirikiana na wananchi wa Ar. Tukisema ni wananchi tutakuwa tunakosea coz even b4 multipatism wananchi walikuwepo na ka-ccm chao ila viongozi wa haka ka-ccm waliwafanya wananchi ni mitaji ya matumbo yao ndiyo maana mpaka leo Ar hakuna barabara mpya mahitaji yanaongezeka na matumbo yao yanaongezeka barabara ziko palepale foleni za magari zinaongezeka.

Kinachofanyika sasa hivi ni kuweka lami tena feki kwenye barabara zilezile baada ya CDM kuweka wazi nini watakifanya kama wakimata dola. CDM na wananchi ndiyo wanastahili pongezi
 
bila lema hizi barabara zisingetengenezwa nakumbuka kuna siku aliwachana meya na mbunge aliyepita kuwa wanahusika kutafuna pesa za wahisani

bila lema kwenda manispaa kuwaletea jambajamba hakuna kitu kingefanyika zaidi ya kujineemesha na kujenga majumba olerien na njiro kwa pesa zetu!

Salute kwa Hon.Lema
mbunge wa Arusha mjini
 
vyuo vikuu unavyovisema ni vya serikali? La hasha! Hivyo huwezi kumsifia jk kwa hilo na kuhusu barabara hela zilishatoka wakazitumia wajuavyo, baada ya lema kutuma barua kuulizia hiyo hela ndio serikali imeanza kuzitengeneza,wamepewa miezi 3 baada ya hapo kuna watu kutoka wb watakuja kukagua

Nadhani huelewi kuwa sera ndio zinafanya hata vyuo vya binafsi viwepo. Uliviona wakati wa Nyerere?
 
bila lema hizi barabara zisingetengenezwa nakumbuka kuna siku aliwachana meya na mbunge aliyepita kuwa wanahusika kutafuna pesa za wahisani

bila lema kwenda manispaa kuwaletea jambajamba hakuna kitu kingefanyika zaidi ya kujineemesha na kujenga majumba olerien na njiro kwa pesa zetu!

Salute kwa Hon.Lema
mbunge wa Arusha mjini

Hayo ya kuropoka hovyo na bila ushahidi ndio yalimkosesha ubunge, au umesahau?
 
Kama nisivyoweza kumsifu baba kwa wajibu wake wa kuleta chakula nyumbani ndivyo nisivyoweza kumsifu mleta lami, kwa sababu hii haki kwa miaka zaidi ya 40 angetakiwa awe anafanya kitu kingine si barabara tena

Yeye ndio kwanza miaka saba, kabla yake alikuwepo nani na nani? kuna mmoja kisha kuwa Rais miaka 24, alifanya nini?
 
kwa muda wa mwezi mmoja na nusu nimeshuhudia barabara za katikati ya mji wa arusha zikiwekwa lami kwa kasi ya ajabu.tukifumbia macho mambo mengine mengi tunaweza kuita haya yanayoendelea arusha nimafanikio makubwa.
Swali langu ni moja na jepesi tu,
je kwa mafanikio haya ni chama kipi kinastahili sifa kati ya ccm na chadema?

wb...lakini tulioarusha huu mradi unasuasua..mfano barabara inayopita karib na hosp ya seliani ujenz wake umesimama na mashimo yanaanza kujitokeza kwa kasi
 
Jakaya Mrisho Kikwete anastahili kila pongezi jinsi alivyobadili sekta ya barabara Tanzania, hakuna wa kabla yake aliyefanya hata nusu ya anayoyafanya yeye, si katika barabara tu, katika nyanja zote. Leo Arusha kuna vyuo vikuu.

Vyuo vilivyopo Arusha kipi ni cha Serikali?,pia kumbuka kabla ya kumsifia baba yako(Jk) kuwa ana mbio pia msifie anaemkimbiza(Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA).
 
Vyuo vilivyopo Arusha kipi ni cha Serikali?,pia kumbuka kabla ya kumsifia baba yako(Jk) kuwa ana mbio pia msifie anaemkimbiza(Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA).

Sera za Serikali iliyopo madarakani ndio unaona hata vyuo binafsi vinachipuka haraka haraka, uliviona hivyo wakati wa Nyerere?

Nawasifu sana madiwani wa chadema Arusha kwa kutekeleza ilani za CCM.
 
pamoja na WB kutoa hela kuna msukumo wa wanasiasa,kwani barabara ngapi zimepewa hela na WB lakini zimeliwa?
 
Mtu atakaye sema ni chadema ujue kuwa huyo ni mnafiki ni si mwenyeji wa arusha, huo ulikuwa mpango wa mda mrefu sana..ndio umekuja kutekelezwa mwaka huu kama unavyoona, yaani nakumbuka waaaaaaaay back miaka ya 2000 kipindi cha mkapa hii plan ilikuwepo..mnazidi kuipa chadema sifa ambazo haistahili??
 
Ushaambiwa juu huko ni mkopo wa World Bank ulioombwa zamani za sasa umefanikiwa, ni kipi unachoshindwa kuelewa?

Na zile Kilomita zaidi ya 11,000 Tanzania nzima ni shinikizo pia? Nenda kaone Singida mitaa yote inatiwa lami, Magufuli anakwambia katika Afrika kwa sasa Tanzania ndiyo inaongoza kwa miradi ya barabara za lami, uko wapi wewe?

N ama highway yanayokuja Dar? au hujapita Morogoro Road Dar., kuona ujenzi ulivyoanza kwa kasi?

Kula ccm ya JK kura CDM???
 
Sera za Serikali iliyopo madarakani ndio unaona hata vyuo binafsi vinachipuka haraka haraka, uliviona hivyo wakati wa Nyerere?

Nawasifu sana madiwani wa chadema Arusha kwa kutekeleza ilani za CCM.

Mi nawasifu waislamu kwa kuanzisha vyuo tofauti na wakati mwingine. Elimu ni kila kitu hata mimi sasa naweza kula digrii ya namna fulani ahsante JK na uamsho.
 
pamoja na WB kutoa hela kuna msukumo wa wanasiasa,kwani barabara ngapi zimepewa hela na WB lakini zimeliwa?

Zitaje wewe. World Bank ule hela yao halafu upewe tena mkopo? unaota.
 
Mi nawasifu waislamu kwa kuanzisha vyuo tofauti na wakati mwingine. Elimu ni kila kitu hata mimi sasa naweza kula digrii ya namna fulani ahsante JK na uamsho.

Jakaya Mrisho Kikwete kahakikisha kwanza Sekondari zinajazana kiasi hakuna kuchaguwana, kahamia vyuo vya ufundi na vyuo vikuu nako anahakikisha vinajazana na anaeingia huko ni kwa merits na si kwa kuchaguliwa.

Mkaona mbinu zenu zinapanguliwa scientifically, mkaanza hila za wazi wazi za kupunguza marks za mitihani, nalo tumewastukia. Tunakula sahani moja siku hizi. Kwi kwi kwi teh teh teh.

Kwani sisi hatujui chuki zenu kwa Kikwete ni zipi? tunajuwa sana, lakini ndio anafanya hivyo, nyie bakini na vijiba vya roho.
 
kwa muda wa mwezi mmoja na nusu nimeshuhudia barabara za katikati ya mji wa arusha zikiwekwa lami kwa kasi ya ajabu.tukifumbia macho mambo mengine mengi tunaweza kuita haya yanayoendelea arusha nimafanikio makubwa.
Swali langu ni moja na jepesi tu,
je kwa mafanikio haya ni chama kipi kinastahili sifa kati ya ccm na chadema?

mwenye kutoa hela. Hela hiyo itakuwa ni kodi ya wananchi au kutoka kwa wafadhili.
 
Back
Top Bottom