Ujenzi unaoendelea Barabara ya Kilwa uzingatie afya za watumiaji

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,606
29,754
Unapoelekea Mbagala kupitia barabara ya Kilwa utaona ujenzi unavyoendelea kwa kujenga pia njia ya mwendokasi, kuna daraja la juu pale Uhasibu na kwa kweli inapendeza haswaa.

Mkandarasi anajitahidi kukimbizana na deadline ya kazi. Lakini kuna tatizo kubwa la vumbi litokanalo na kifusi kitumikacho kwenye ujenzi huo

Masaa yote kumekuwa na foleni kibwa lakini vumbi kama tupo jangwani. Watu wengi wameanza kuugua vifua na mafua ambapo inawezekana wengi wakafa kwa hofu wakidhani wameambukizwa CORONA.

Mshauri mwelekezi anapaswa kukagua kama vigezo kuhusu afya na usalama wa wanaoitumia sasa na wanaoishi pembezoni umezingatiwa.

Kuhusu foleni nawasihi wahusika wafungue njia mbadala zitakazopunguza adha za foleni kwa wanatumiaji.

Mkuu wa Wilaya ya Temeke tusaidie kwenye hili
 
mkandarasi analipwa pesa ya miamala 😆 hiyo shughuli itachukua mwaka maana hapa kuna mtu ananidai pesa yake tumekubaliana nitampa mtu ampelekee 😄 alieanzisha hizi tozo atajua hajui 😄
 
Back
Top Bottom