Ujenzi holela wa Vituo vya Mafuta ni bomu linalosubiri kulipuka

Ujenzi holela wa Vituo vya Mafuta ni bomu linalosubiri kulipuka

Joined
Apr 1, 2017
Posts
16
Reaction score
25
ChatGPT Image Jan 29, 2026, 08_42_50 PM.png

Picha: Akili Mnemba
Licha ya sharia na kanuni za mazingira na biashara ya mafuta kuweka utaratibu wa ujenzi wa vituo vya mafuta, kumekuwa na ujenzi holela wa vituo vya mafuta hususani kwa jiji la Dar es Salaam.

Sheria ya Mafuta Na. 21 ya mwaka 2015 inaipa nguvu EWURA, kusimamia shughuli za mkondo wa kati na mkondo wa chini wa sekta ya mafuta ya petroli. Kifungu cha 126 (1) cha sheria hiyo kinamtaka mtu yoyote anayetaka kujenga miundombinu ya mafuta kuomba kibali cha ujenzi kutoka EWURA.

Aidha, Kifungu cha 131 (1) cha sheria hiyo kinawataka wote wanaojihusisha na sekta tajwa kuwa na leseni iliyotolewa na EWURA.

Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA), imekuwa mara kwa mara ikisisitiza kanuni namba 27 ya usimamizi wa biashara za vituo vya mafuta ya mwaka 2022 kama ilivyochapishwa kwenye gazeti la serikali Na. 150.

Kanuni za mipango miji na Sheria ya Usimamizi wa Mazingira, 2004 inakataza vituo vya mafuta kuwa karibu na makazi ya watu.

Kwa mujibu wa utaratibu wa mipango miji, umbali wa kituo hadi kituo ni mita 200.

Hata hivyo, kumekuwa na ujenzi holela wa vituo vya mafuta tena karibu na makazi hali inayohatarisha usalama wa wananchi endapo moto utalipuka.

Ujenzi huo holela umeonekana katikabarabara ya Tandale/ Sinza, kuanzia Tandale SweetyKona utaanza na kituo cha mafuta cha ATN, upande wa kushoto ukiwa unatoka Sinza kuelekea Magomeni, mbele kidogo hatua upande wa kulia utakutana na kituo cha Victori (ushahidi upo kwenye video chini).

Ukisogea mbele Tandale kwa Mtogole eneo la Chama utakutana na kituo cha mafuta cha Olympic upande wa kulia hata chache mbele upande wa kushoto utakutana na kituo cha KSK Oil, ukisogea mbele mita 30 karibu na Tandale Kwa Tumbo upande wa kulia kuna kituo cha kujaza gesi asilia upande wa kushoto kituo cha OilCom, barabara hiyo hiyo eneo la Magomeni kwa Bibi Nyau utakutana na kituo cha Total Energy.

Umbali kutoka Magombeni Kanisani mpaka kufikia Sinza Madukani ni Kilometa nne, lakini kuna vituo vitano vya mafuta.

Kanuni hiyo inawataka wamiliki wote kuhakikisha wanachukua tahadhari juu usalama wa afya, mali na mazingira ili kuepusha milipuko.

Mwandishi wa habari alizungumza na baadhi ya wakazi wa maeneo ya, amesema kuwa licha ya kuwa biashara imechangia ukuaji wa eneo lao lakini wanawasiwasi wa usalama wao eneo ikitokea mlipuko wa moto.

Mkazi mmoja wa Tandale Chama aliyezungumza kwa sharti ya kutotajwa jina lake, alisema, “hebu fikiria duka langu lipo karibu na hiki kituo cha mafuta siku ikitokea la kutokea tunalipuka sote sio mimi hata makazi ya wananchi yapo karibu kabisa.

“Hivi vituo wakati vinajengwa wananchi hatujashirikishwa sisi tumeona tu ujenzi hatimaye kituo na isitoshe hivi vituo vimetufuata sisi,” alisema.

Ali Kipulizo mkazi wa Mtongani, wilayani Temeke, alisema anastaajabishwa kuona kila uchao vituo vya mafuta vinajengwa kwa wingi katika eneo moja.

“Najiuliza mimi kwanini wajenge kwa mlundikano ikwa kuna sehemu huko mikoani wanahitaji huduma hizi kwanini wanatufanya tuishi kwa hofu,” alisema.

Oktoba 2012 Policy Forum na Chama cha wanasheria wa Mazingira (LEAT) walipendekeza wakati taifa likielekea kwenye katiba mpya kipekee yaingize ibara zitakazosisitiza suala la mazingira wananchi kuingi kwenye mazingira salama kuwa moja ya haki ya msingi kwenye katiba.

PrayGod Sallema, Mwanasheria pia mwanaharakati wa mazingira amemwambia Mwandishi wa habari kuwa uholela wa ujenzi wa vituo vya mafuta ni bomu ambalo likilikupuka hatutakuwa na wa kumlaumu.

“Tazama hii njia ya Tandale humalizi hata nusu kiwanja pale chama kuelekea kwa Tumbo unakutana na takribani vituo vitano vya mafuta kwa pamoja lakini ajabu makazi ya watu yapo karibu yaani nyumba za watu na vituo vya mafuta zipo karibukaribu kiasi ambacho moto ukiwaka kwanza vile vituo vya mafuta vinne pale vitakuwa vikipokezana kisha kwenye makazi ya watu yaani kutawaka moto ambao hata fire watashindwa kujua waanzie wapi kuzima,” alisema Sallema.

Alisema kuwa mambo kama hayo hayatokie bila rushwa.

“Hapa ni wazi kuna mashaka kwamba kuna mazingira ya rushwa isingekuwa rushwa hakuna mtu angekubali kutoa vibali hivyo au kama sio rushwa basi ni uzembe watafakari upya.”
ChatGPT Image Jan 29, 2026, 08_50_16 PM.png
Hata hivyo jitihada za Mwandishi wa habari hizi kuwatafuta EWURA zimegonga mwamba ziadi ya kuambiwa na maofisa ambao sio wasemaji wa Mamlaka hiyo wakisema kuwa ni kinyume cha sheria kwa vituo vya mafuta kuwa karibu karibu.
 
Uzi huu usomwe na Mamlaka maana sisi hapa wakazi wa Tandale Chama kuelekea kwa Tumbo hivi vitu ipo siku vitatufanyia kitu mbaya
 
Umbali kutoka magoneni kanisani hadi Sinza ni km5 ila kuna vituo vinne vya mafuta shida iko wapi hapo iwapo umesema sheria kati ya kituo na kituo ni mita 200( kumbuka hii ni upande nnoja haihusu kituo upande wa pili)
 
Tujadili bila jazba.
Vituo visijengwe kwenye makazi ya watu vijengwe wapi? Mfano hapa Dar vituo ijengwe wapi ambapo hamna makazii ya wath? Vikajengwe Kimbiji Kigamboni au Fukayosi Bagamoyo? Kwahio kana uko Magomeni au Manzee utoke hapo uende porini kuweka mafuta sio?
 
Vipi kuhusu hivyo vituo kuwa maegesho ya vyombo vya moto nyakati za usiku??

Hakuna muongozo wowote?
 
Shida kwani nini, biashara ya mafuta si biashara kama zingine zikifuatana shida ni nini
Kuhusu usalama watu hofu ni zitalipuka wakati October 29, vituo vingapi vimechomwa moto? Kipi kimelipuka
Vituo vya mafuta vinageuza sana madhali ya miji, vinatoa ajira na uchumi, pia vinatoa huduma tuache mawazo ya kizamani
 
Tujadili bila jazba.
Vituo visijengwe kwenye makazi ya watu vijengwe wapi? Mfano hapa Dar vituo ijengwe wapi ambapo hamna makazii ya wath? Vikajengwe Kimbiji Kigamboni au Fukayosi Bagamoyo? Kwahio kana uko Magomeni au Manzee utoke hapo uende porini kuweka mafuta sio?
Hoja si kutokuwepo kabisa kwa vituo vya mafuta hoja hapa ni kukiukwa kwa sheria za mazingira kwa kujenga vituo vingi sehemu moja mfano wa hapo barabara ya Tandale pale Chama hazijafika mita 50 unapata vituo zaidi ya vitatu miongozo yetu inasemaje, kuna haja gani ya kuwa na sheria ?
 
Sheria umbali baina ya kituo na vituo ni 200m upande mmoja. Sasa niambie kituo gani hio njia ya tandale vipo chini ya 200m. Kumbuka ni upande mmoja.
Kusema hazijapita 50m kuna vituo vitatu ni uongo. Hivyo viwanja vina upana gani 10m ?
 
Hoja si kutokuwepo kabisa kwa vituo vya mafuta hoja hapa ni kukiukwa kwa sheria za mazingira kwa kujenga vituo vingi sehemu moja mfano wa hapo barabara ya Tandale pale Chama hazijafika mita 50 unapata vituo zaidi ya vitatu miongozo yetu inasemaje, kuna haja gani ya kuwa na sheria ?
50m vituo zaidi ya vitatu huu uongo sasa
 
Tujadili bila jazba.
Vituo visijengwe kwenye makazi ya watu vijengwe wapi? Mfano hapa Dar vituo ijengwe wapi ambapo hamna makazii ya wath? Vikajengwe Kimbiji Kigamboni au Fukayosi Bagamoyo? Kwahio kana uko Magomeni au Manzee utoke hapo uende porini kuweka mafuta sio?
Hoja si kutokuwepo kabisa kwa vituo vya mafuta hoja hapa ni kukiukwa kwa sheria za mazingira kwa kujenga vituo vingi sehemu moja mfano wa hapo barabara ya Tandale pale Chama hazijafika mita 50 unapata vituo zaidi ya vitatu miongozo yetu inasemaje, kuna haja gani ya kuwa na sheria ?
Sheria umbali baina ya kituo na vituo ni 200m upande mmoja. Sasa niambie kituo gani hio njia ya tandale vipo chini ya 200m. Kumbuka ni upande mmoja.
Kusema hazijapita 50m kuna vituo vitatu ni uongo. Hivyo viwanja vina upana gani Olympic upande wa kulia hata chache mbele upande wa kushoto utakutana na kituo cha KSK Oil, ukisogea mbele mita 30 karibu na Tandale Kwa Tumbo upande wa kulia kuna kituo cha kujaza gesi asilia upande wa kushoto kituo cha OilCom,
 
Hoja si kutokuwepo kabisa kwa vituo vya mafuta hoja hapa ni kukiukwa kwa sheria za mazingira kwa kujenga vituo vingi sehemu moja mfano wa hapo barabara ya Tandale pale Chama hazijafika mita 50 unapata vituo zaidi ya vitatu miongozo yetu inasemaje, kuna haja gani ya kuwa na sheria ?
Pale Chama kuna Olymipic, KSK Oil, mbele yake hufika hata mita 20 kituo cha kujaza gesi hufiki tena hata mita 30 unakutana na kituo cha Oil Com , ukienda Kilwa Road Pale Mtoni mtongani upande wa kulia kama unakwenda Mbagala kuna vituo vipya viwili vimefuatana pale hata mita 0 hazifiki .
 
Sahivi imehamia Songea hiyo kitu, hasa barabara ya kutoka stendi kuu mjini kwenda shule ya tanga.
Jamaniii shell zinawekwa km njugu, afu ni kwenye makazi ya watu.
Duuuuh
 
Hoja si kutokuwepo kabisa kwa vituo vya mafuta hoja hapa ni kukiukwa kwa sheria za mazingira kwa kujenga vituo vingi sehemu moja mfano wa hapo barabara ya Tandale pale Chama hazijafika mita 50 unapata vituo zaidi ya vitatu miongozo yetu inasemaje, kuna haja gani ya kuwa na sheria ?
Mkuu Kilwa Road kuna Sabasaba kwa Mpili (Mbagala), yaani vituo viwili vimeyengenisha na ukuta yaani PetroAfrika imetengenisha na ukuta wa Olake upande wa kulia kama unakwenda mjini pia eneo la Mtongani kuna vituo viwili upande mmoja pande wa kushoto ukiwa unakwenda mjini kuna kituo cha mafuta kinaitwa Afroil ukuhesabu nyumba 13 mbele unakutana na kituo kingene cha Olake kama ilivyo pale Biafra upande wa kushoto kama unakwenda Moroko unanza kituo ya Olake kisha mbele yake unakutana na OOMCO.
 
Back
Top Bottom