Unataka kujaza nini, kama ni maji, haya twende pamoja,
Nenda kapime urefu wa tanki(height), na kipenyo cha mduara(diameter)
Halafu tumia hii formula kupata ujazo, lakini formula inatumia nusu kipenyo, maana yake gawanya kipenyo kwa 2 ndio upate radius r
Jibu litakua la ujazo, yaani cubic centimeter au cubic meter , inategemea ulichukua vipimo kwa meter au centimeter
badilisha ujazo wa kuwa lita
1 cubic meter = 1000 litre
1cubic centimeter = 0.001 litre
Jibu utakalopata la litakuwa la lita
Sasa kwa kuwa lita moja ya maji (nakazia ya maji) ni kilogram 1,
badilisha hizo lita kuwa tani, kumbuka kwa kila kilogram 1000(litre 1000 za maji) ni tani 1