Ujauzito wa jf

ma jery

Senior Member
Jun 15, 2011
171
64
naombeni tips jamani jinsi ya kuishi kipindi hiki cha ujauzito niliopata hapa jf ili niweze kijifungua maxence wangu salama
nashukuruni
 

AshaDii

Platinum Member
Apr 16, 2011
16,219
17,980
Ma Jery wee kiboko!!! lol... Historia yako ya jinsi mlivooanana hunikosha na hatimae mtoto..... Hongera bana.
 

Kaunga

JF-Expert Member
Nov 28, 2010
12,540
13,439
Kula matunda na mboga mboga, kunywa Maziwa kila siku na maini atleast once a week! Acha pombe sigara, mikorogo na madawa ya nywele kipindi chote cha ujauzito!

Usilale lale; be active, punguza/epuka stress!

Utazaa mtoto mzuri mwenye afya ya mwili na akili! Ukitaka afya ya roho pia; sali na mkabidhi huyo mzaliwa wa kwanza kwa Mungu yeyote unayemuamini!

Ni hayo tu!
 

ma jery

Senior Member
Jun 15, 2011
171
64
kula matunda na mboga mboga, kunywa maziwa kila siku na maini atleast once a week! acha pombe sigara, mikorogo na madawa ya nywele kipindi chote cha ujauzito!

usilale lale; be active, punguza/epuka stress!

Utazaa mtoto mzuri mwenye afya ya mwili na akili! Ukitaka afya ya roho pia; sali na mkabidhi huyo mzaliwa wa kwanza kwa mungu yeyote unayemuamini!

Ni hayo tu!
nashukuru kwa ushauri ivo vitu vya pinki mi wala situmii
 

ndyoko

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,975
1,639
Kula matunda na mboga mboga, kunywa Maziwa kila siku na maini atleast once a week! Acha pombe sigara, mikorogo na madawa ya nywele kipindi chote cha ujauzito!

Usilale lale; be active, punguza/epuka stress!

Utazaa mtoto mzuri mwenye afya ya mwili na akili! Ukitaka afya ya roho pia; sali na mkabidhi huyo mzaliwa wa kwanza kwa Mungu yeyote unayemuamini!

Ni hayo tu!

Hapo kwenye red n bolded. Acha kumhatarisha mtoto wa mwenzio. Kula vyote ulivyoambiwa ila hiyo ya maini sikushauri kabisa dada. maini is one of the most poisonous organ of any living organisms. Sumu nyingi hukusanywa kwenye ini na kupunguzwa ukali wake kabla haijaenda sehemu nyngine za mwili. Fanya tafiti na utaniambia kwamba daktari yeyote mjanja huwa hali maini iwe ya ng'ombe au mdudu mwingine yeyote.

Usitumie hiyo kitu, kuna uwezekano, japo kidogo, ukasababisha mwanao apate hizo sumu, teratogens, zikapelekea kuzaa mtoto mwenye kasoro bure dada, acha hiyo kitu mbona mboga ziko nyingi tu.

Ubaki salama na mimba yako dada.
 

LiverpoolFC

JF-Expert Member
Apr 12, 2011
11,169
2,996
Mmmmmhh! Kweli Jf mambo ni mazuri kama 2navyoona ktk thread za wenyewe! Ijapo kuwa Mi si msemaji sana ktk jukwaa hii lakini kwangu Mimi ninachoweza kusema kutokana na uzoefu wangu wa takrban mwaka wa kumi tatu ya kuwa na familia,Mi nao ID ya (kaunga) ni muhimu sana jamani na ktk zile aya ulizomwekea ishara ktk rangi kama kweli hau2mii Mi naona kilichopo ni kumshukuru MUNGU katika hali uliyonayo na bila shaka usipoteze mipango yote ya Dr wako ktk calendar utakayopewa. Sina mengi zaidi ya Kheri na bila shaka humu tu wataalam wengi na utapata nasaha nzuri. NB: Mi ningependelea uwe na ASALI ambayo haijachakachuliwa na hawa watoto wa magamba.
 

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,861
30,279
Utunzi wa mama kabla ya kuzaa

Huu ni utunzi ambao hutolewa kwa mama wakati wa uja uzito ili kuhakikisha ya kwamba mama anabakia kuwa mwenye afya na anajifungua mtoto mwenye afya.Hujumuisha mambo yafuatayo:
 • Ukadiriaji wa hatari zinazoweza kumkumba
 • Ukadiriaji unaondelea wa ustawi wa kijuzi
 • Ukadiriaji unaoendelea wa utata
 • Elimu kuhusu usumbufu wa kawaida wakati wa uja uzito,hali ya hisia (ukijumuisha huzuni wa baada ya kujifungua),vikao vya darasa kuhusu kabla ya kujifungua.
 • Majadiliano kuhusu kujifungua na jinsi ya kujifungua
Kujipatia matibabu
Historia ya uvutaji sigara, unywaji wa pombe na matumizi ya madawainafaa kutathminiwa. Pia wanawake wanashauriwa kutojitibu kabla ya kuangalia kwanza usalama wao na wa mtoto aliyetumboni. Ni bora kutaja kwamba vitamini na tiba za kutumia mitishamba zinafaa kupunguzwa wakati wa uja uzito. Kwa mfano, matumizi ya zaidi ya vidonge viwili vyaVitamini A kila siku kunaweza kusababisha dosari za kuzaliwa kwa mtoto atakayezaliwa.

Mlo
Ushauri kuhusu mlo unafaa kutilia mkazo mlo kamili na vyakula tofauti tofauti ukisisitizia kabohaidreti changamani na protini, pamoja na kiasi cha kutosha cha foliate(miligramu 0.5), chuma (miligramu 15) ,kalshiamu(miligramu 1200) na maji (lita 2-3) kila siku.

Tembelea kituo cha afya ya mama wajawazito
Tembelea ktuo cha afya ya mama wajawazito kila mwezi katika kipindi cha kwanza cha wiki 28, baadaye nenda baada ya kila wiki mbili mpaka wiki ya 36. Kutoka hapa nenda kila wiki mpaka siku ya kuzaa. Kila wakati unapotembelea kituo cha afya, hali ya afya yako na ya mtoto wako inaangaliwa.
Usumbufu wa kawaida wakati wa ujauzito
 • Ongezeko la kutaka kwenda haja ndogo ni kawaida lakini linafaa kufanyiwa uchunguzi kwani 8% ya wanawake waja wazito watakuwa na maambukizo katika eneo wanalotumia katika haja ndogo ambayo hayaonyeshi dalili.
 • Uvimbe katika kifundo cha mguu unaweza kuhusishwa na kushinikiza kwa mishipa itwayo inferior vena cava. Ikiwa kuvimba hakuambati na shinikizo la damu, tiba huwa kupumzisha miguu ikiwa imewekelewa juu kama vile ya kiti au kwa kutumia vyakula kama Celery au Vitamin B6 ambazo kwa kawaida huondoa maji mwili kupitia kukojoa mara nyingi.
 • Kufura kwa mishipa kwa sababu zizo hizo na kupata nafuu baada ya kufuungiwa kunaweza kuwa kwa kushtua. Pindi tu inapotambulika, matumizi ya mapema ya stokingi za kushikilia ni jambo la busara; ilhali matumizi ya mda mfupi ya kiinua fupanyonga na vipande vya barafu vinaweza kumaliza dalili hizi za kufura kwa mishipa katikaa tupu.
 • Kiungulia husababishwana kupwa kwa tumbo na umio pamoja na ongezeko la shinikizo la tumbo.Ushauri wa mkao na mlo pamoja na matumizi ya vimaliza asidi humaliza mengi ya haya, lakini mpinzani wa H2 (kitengo cha B katika uja uzito) anahitajika mara moja moja.
 • Uyabisi wa tumbo (kuwa na gesi kwa tumbo) unaweza kutokea mapema lakini angalau husababishwa na homoni lakini unaweza kuzidishwa na ongezeko la yaliyomo kwenye fupanyonga.Ongezeko la ukubwa wa mishipa na kushinikizwa kwa mishipa katika fupanyonga kunaweza kusababisha kufura kwa mishipa. Wanawake wanapaswa kushauriwa kuongeza matumizi yao ya uoevu na
 • ufumwele na ikiwa dawa za kuharisha zinahitajika zinapaswa ziwe za aina ya ufumwele k.m Metamucil ama Fybogel.
 • Kuumwa na sehemu ya chini ya mgongo ni jambo la kawaida kwa sababu ya kubadilika kwa hali ya mkao.
 • Kuoza kwa meno na magonjwa ya tishu zinazozunguka meno huongezeka wakati wa uja uzito na unafaa kushughulikiwa na dakitari mapema.
 • Mabadiliko katika ngozi yanajumuisha madoa ya hudhurungi kwenye ngoziambayo hutoweka baada ya ujauzito.
 • Mikwaruzo hutokea katika 17% ya wanawake waja wazito. La kuvutia ni ya kwamba 50% ya wanawake wenye ugonjwa wa ngozi
 • huonyesha dalili za kupata afueni wakati wa uja uzito. Ikiwa hakuna kipele, zingatia ukosefu wa chuma ama hali inayoweza kuwa hatari ya kusimama ama kupunguza kasi ya mtiririko wa nyongo wakati wa uja uzito. Dawa za kuzuia mzio zinaweza kuwa za manufaa.
 • Alama zinazobakia kwenye ngozi ya tumbo, mapaja, makalio ilinyooka baada ya uja uzito ikiwa ukuaji umekuwa wa haraka. Ukavu na kujikunakuna kunaweza kutulizwa na mafuta ya mboga ama krimu ya Vitamini E na kutotumia sabuni.

 

fxb

Senior Member
Jun 22, 2011
123
24
Pamoja na uchauri mzuri Ukumbuke kwenda kliniki RCH mapema iwezekanavyo na ukitaka kuona raha zaidi usimwache mwenzio mnapokuwa cliniki
 

Lizzy

Platinum Member
May 25, 2009
26,536
37,902
Hapo kwenye red n bolded. Acha kumhatarisha mtoto wa mwenzio. Kula vyote ulivyoambiwa ila hiyo ya maini sikushauri kabisa dada. maini is one of the most poisonous organ of any living organisms. Sumu nyingi hukusanywa kwenye ini na kupunguzwa ukali wake kabla haijaenda sehemu nyngine za mwili. Fanya tafiti na utaniambia kwamba daktari yeyote mjanja huwa hali maini iwe ya ng'ombe au mdudu mwingine yeyote.

Usitumie hiyo kitu, kuna uwezekano, japo kidogo, ukasababisha mwanao apate hizo sumu, teratogens, zikapelekea kuzaa mtoto mwenye kasoro bure dada, acha hiyo kitu mbona mboga ziko nyingi tu.

Ubaki salama na mimba yako dada.

Asante Ndyoko....
Watu wengi tu hawajui kwamba maini sio mazuri kwa mama mjamzito....nadhani ni muhimu wamama wanapoenda clinic kwa mara ya kwanza wakawa wanataarifiwa kuhusu vyakula ambavyo wanatakiwa kuavoid ili kutohatarisha afya ya mtoto.
 

King'asti

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
27,802
24,505
kinachotuponza ni hizi haki tunazogombea. zamani issues za kushindwa kuzaa ama kupata big baby hazikuwepo kiviile. wajawazito waliambiwa wasile maini (wasipate still birth) wala mayai (wasizae watoto wasio na nywele). wazee hawakujua exactly what happened lakini it worked for them. khabari yake beijing!!
Asante Ndyoko....
Watu wengi tu hawajui kwamba maini sio mazuri kwa mama mjamzito....nadhani ni muhimu wamama wanapoenda clinic kwa mara ya kwanza wakawa wanataarifiwa kuhusu vyakula ambavyo wanatakiwa kuavoid ili kutohatarisha afya ya mtoto.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom