Ujasusi wa Kiuchumi na Kiteknolojia unakuwa kwa kasi, Je Tanzania iko tayari

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,400
Hivi karibuni nchini Marekani shirika la FBI walitoa picha za raia watano wa China ambao wanatuhumiwa kwa kufanya shughuli za ujasusi wa kiuchumi yaani kwa lugha ya kiingereza "economic espionage" au "industrial espionage".

Kwa mujibu wa serikali ya Marekani, raia hawa walikuwa wakishiriki kwa pamoja katika mradi unaoitwa Unit 61398 ambao upo mjini Shanghai na unahusika na kurusha mashambulizi mbalimbali Cyber Attacks kwenda katika sehemu mbalimbali nchini Marekani na barani Ulaya hadi Russia.

Lengo la mashambulizi hayo ni kupata taarifa mbalimbali za kijasusi kuhusu mbinu mbalimbali zinazotumiwa na makampuni makubwa ya biashara duniani na kutaka kuzitumia taarifa hizo katika kufanikisha miradi mbalimbali nchini China na nje ya China.

Hatua hiyo ya kutoa majina ya raia hao wa China imekuja baada ya ya uchunguzi ulofanywa na kampuni ya Mandiant ya nchini Marekani ambayo inajishughulisha na ubunifu wa njia mbalimbali za usalama wa mitandao, kompyuta na vifaa vya mawasiliano.

Mandiant inafanya kazi na ina wateja wengi wakubwa yakiwemo makampuni makubwa duniani na pia inajishughulisha na tafiti mitandaoni na uchunguzi wa uhalifu mitandaoni ikitumia vifaa na zana za hali ya juu kabisa.

Kitendo cha kuwataja raia hao watano ambao wote ni wanajeshi katika jeshi la China yaani Chinese Liberation Army kimeiudhi sana nchi ya China na kumekuwa na majibizano ya chinichini baina ya ubalozi wa China nchini Marekani na maofisa wa wizara ya sheria ambayo FBI ipo chini yake.

China kwa upande wake inadai madai hayo ya Marekani ni ya kutengenezwa na inakumbushia madai ya Edward Snowden aliekuwa mhandisi kwenye idara ya ujasusi wa mawasiliano ya NSA kwamba Marekani nao kupitia NSA wamewahi kufanya mashambulizi na kupenya katika mitandao ya kampuni ya vifaa vya mawasiliano HUAWEI kwenye makao yake makuu nchini China.

Marekani nayo inajibu kwa kusema kwamba ili kulinda usalama wa taifa hilo inabidi wakati mwingine kuwafahamu makampuni kama Huawei na haijihusishi na wizi wa maarifa au intellectual property kama China inavyofanya.

Hatua hii ya mabishano kati ya mataifa haya mawili inatishia uwezo wa makampuni mbalimbali yanayotaka kuwekeza nchini China kwa kuhofia usalama wa mitandao yao na taarifa muhimu za siri kuhusu uendeshaji wa makampuni hayo.

Mwaka 2012 kampuni kubwa ya kutengezeza vifaa vya kusafisha mazuria ya Dyson ilikumbwa na athari za ujasusi wa taaluma na uchumi ambapo aliekuwa mhandisi wake raia wa China bwana Yong Pang alipokwapua taarifa za siri kuhusu utengenezaji wa mota ya mashine na kuiuzia kampuni ingine ya Ujerumani Bosch kwa ada ya Euro 10,000

Bwana Pang alikuwa ni mhandisi wa kifaa hicho cha mota ambacho ndicho kinaendesha mashine hizo au "vacuum cleaners" na zile za kukausha mikono "hand dryes, na aliwahi kufanya kazi kwenye kampuni ya Bosch kati ya mwaka 2006 na 2008. Baadae mwaka 2010 akajiunga na kampuni ya Dyson kwenye makao makuu yake yaliyopo Uingereza.

Ujasusi wa mitandaoni kwa shughuli za kiuchumi au economic espionage umekuwa ni tatizo sana katika miaka ya hivi karibuni. Ukuaji wa matumizi ya mitandao na kiwango cha elimu itolewayo na baadhi ya vyuo vikuu duniani hususan barani Ulaya na Marekani umekuwa ukiwapa faida vijana wadogo wa kutoka mataifa kama ya China.

Pindi warudipo nchini mwao huanza kujipanga na kufanya hizi shughuli za ujasusi ambao unasaidia ukuaji wa uchumi na masuala mbalimbali ya kiteknolojia.

Katika ujasusi wa aina hii nyaraka za taifa, siri za uendeshaji makampuni, siri za ubunifu wa vifaa na mashine mbalimbali na kazi zozote zenye maslahi kwa taifa, pamoja na kazi za Sanaa au ujarisimali yaani intellectual property, zinadukuliwa na majasusi na kutumia katika nchi zao kwa kuzibadili au kuziendeleza ili ionekane ni kazi zao au faida kwa nchi zao.

Hii imekuwa ni changamoto kwa nchi zingine duniani kama Marekani, Russia, na zile za barani Ulaya ambazo kwa kupitia idara zake za ujasusi zimekuwa zikikabiliana na athari za ujasusi wa mitandao yaani counter intelligence.

Ujasusi pingamizi au counter intelligence ni pale ambapo majasusi waliopo ndani ya nchi au nje wanakuwa wakilinda maslahi ya taifa, makampuni yake makubwa kwa kutumia taaluma na teknolojia iliyopo.

Kwa mfano jasusi wa kitanzania anaweza kuwa anamfuatilia raia wa kigeni ambae yupo nchini Tanzania na kama ipo siku raia huyo ana taarifa mbalimbali za wizi alizouziwa na jasusi wa ndani wa kitanzania, anaweza kusimamishwa uwanja wa ndege na kupekuliwa kila kitu alicho nacho.

Katika upekuzi huo kuna vitu vinaweza kugundulika kuwa vinatoroshwa nje ya nchi vitu hivyo vikiwa ni pamoja na madini na vito vya dhahabu, taarifa na ramani mbalimbali kuhusu maeneo nyeti na yake yanayohusu miundombinu mbalimbali na hata wanyama hai.

Lakini katika dunia ya sasa katika karne hii ya 21, kunajitokeza aina mbili za majasusi wa aina hii wa counter-intelligence. Wapo majasusi wa serikali na wale wa jeshi na pia wapo wale majasusi wanaoajiriwa na makampuni mbalimbali na wanashindwa kufahamu kwamba wanafanya kazi za kijasusi.

Kwa mfano makampuni ya simu kama Huawei tangu waingie nchini Tanzania ina taarifa zote kuhusu raia wa Tanzania, matumuzi ya simu za mikononi, mawasiliano yao na mwisho matumizi yao kwa ujumla au "habits".

Lakini inawezekana kabisa kwamba si taarifa zote za makampuni kama Huawei, Acacia, Barrick Gold na hata Vodacom hasa zile za kuhusu mapato yake na faida zinazopata zote zinajulikana na vyombo kama TRA, na hii inahusu makampuni makubwa ya kitanzania kama IPP, Azam na mengine mengi tu.

Hii pia inahusisha mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo yanatumia mwamvuli wa misaada au ushauri lakini kwa siri wanafanya mambo mengine kabisa.

Tanzania ni moja ya nchi changa duniani ambazo zinakabiliwa na changamoto hii ya ujasusi wa kiteknolojia na uchumi yaani technological and economic espionage.

Je, ni vipi namna ya kukabiliana na ujasusi wa mitandaoni na ule wa kiuchumi?

Je, TCRA wamejipanga vipi badala ya kuanza na vidagaa ambavyo zipo sehemu kama JF vikitoa tu madukuduku yao kwa njia ya mitandao bila kuvunja sheria?

Kwanza, kabla ya kuelezeka hatua za kukabiliana na huu ujasusi wa kiuchumi au na kiteknolojia ni budi kufahamu ni vipi unafanyika na unatumia nyenzo gani.

Pamoja na nyenzo kama satellite, simu za mikononi na internet ujasusi wa kiuchumi unataka jasusi atumie vifaa kama drones, ambazo atatumia kupiga picha mbalimbali, kifimbo cha kumbukumbu au USB Stick ambacho kinaweza kuchomekwa kwenye mifumo ya kompyuta au servers za kampuni husika na njia ya intrenet isiyounganishwa kwa waya yaani wireless fidelity au Wifi.

Kwa kutumia WIFI jasusi anaweza kusimama katikati ya mikusanyiko ya watu karibu na majengo ya benki, au balozi au mashirika ya kimataifa au hata ikulu na kudukua taarifa muhimu ambazo atazitumia kwa faida ya nchi yake.

Hivyo majasusi hawa wanaweza kabisa kuvuna siri za makampuni , siri za mifumo ya kompyuta na pia kuweza hata kununua kutoka kwa baadhi ya watumishi au wafanyakazi wasio waaadilifu na waaminifu ambao wanakuwa wawauzia codes za computer majasusi hawa.

Hivyo basi pamoja na jitihada mbalimbali zinazofanywa na nchi kadhaa duniani katika kuhakikisha mitandao yao inalindwa, badi katika baadhi ya nchi kama Tanzania masuala ya ujasusi huu haujasomwa vizuri.

Ni ujio wa raisi John Magufuli ndio ulionipa mwanga kuhusu uwezekano wa kuwepo kwa majasusi wa mitandaoni na wale wa kiuchumi katika nchi yetu na jinsi gani taratibu wameanza kudhibitiwa.

Serikali ya raisi Magufuli imedhitibiti upatikanaji wa habari za ndani za kuhusu Serikali na pia kwa kupitia idara yake ya MAELEZO kumefanywa mabadiliko ya kiuongozi katika kujaribu kusisistiza nia ya serikali katika kudhibiti mwenendo wa taarifa mbalimbali za serikali .

TCRA ndipo inapokuja kutekeleza sera ya kuhakikisha teknolojia na mawasiliano na matumizi ya mitandao yanachungwa kwa uangalifu.

Mbali na jitihada za TCRA kuwapa elimu ya matumizi sahihi ya mitandao, pia imeonekana kama ni chombo tu kinachofuata maagizo ya serikali ingawa taasisi hii inajiita ni ya kujitegemea.

Ili kuondoa dhana hiyo ni budi TCRA wakawa wanafahamu tofauti kati ya kutumia jina bandia kwa lengo jema (Whistle Blowing) au kwa nia mbaya ya uhalifu.

Kuna njia nyingi ambazo TCRA inaweza kuzitumia katika kuendela kutoa elimu na semina kwa raia kuhusiana na hatua za kuchukua kulinda ama siri za makampuni , biashara mbalimbali na hata mashirika makubwa ya umma.

Lakini kuanza kutisha raia kwamba wakitumia majina bandia ole wao, sidhani kama ni njia sahihi ya kuelimishana kuhusu sheria ya mtandao na madhara ya matumizi mabovu.

Tanzania kama taifa linalokuwa linahitaji mhimili mzuri wa mitandao ambayo situ inalinda maslahi ya taifa hili, bali pia inawalinda watumiaji wazuri wa mitandao ambao watakuwa tayari kutoa taarifa za kijasusi zaitakazosaidia kuwakamata wale majasusi wa nje na wale wanaowasaidia.
 
Hivi kuna mtu anaeweza kupoteza mda wake kuidukua Tanzania kweli? labla Rwanda,

Tanzania kila kitu tunacho tumia kinatoka nje! Majasusi wa kimarekani wadukue IPP au Azam waibe tech ya kuchanganya juice? haha Tanzania hatuna kitu cha kuficha bhana
 
Hivi kuna mtu anaeweza kupoteza mda wake kuidukua Tanzania kweli? labla Rwanda,

Tanzania kila kitu tunacho tumia kinatoka nje! Majasusi wa kimarekani wadukue IPP au Azam waibe tech ya kuchanganya juice? haha Tanzania hatuna kitu cha kuficha bhana

Mkuu, utaalam wa kutengeneza juisi za Azam au maji ya Kilimanjaro kwa IPP ni hazina kwa wenye hivyo viwanda.

Unajua kila kila bidhaa inayotengezwa duniani kuna siri Fulani ambayo haipaswi kujulikana kwa washindani wa kibiashara?

Si lazima wawe majasusi wa Marekani.

Kuna uwezekano mkubwa kabisa wakawepo majasusi wa kutoka humuhumu barani Afrika.

Mbona kuna watu wamegunduliwa wanafanya kazi serikalini ilhali si raia wa Tanzania?

Je hilo ni kosa la nani?
 
Marekani,china,Urusi pamoja na nchi zingine wote wanatabia za udukuzi ila kwetu hapa wataalamu wa kada hiyo ndio wanaojua jinsi ya kujilinda
 
Nice article, damn i like it..

Economic intelligence ni muhimu sana kwa maendeleo ya haraka ya kiuchumi kwa nchi iliyojipanga vizuri na ndio imezisaidia nchi nyingi za Asia kufika hapo zilizopo leo hii.

Nasubiri makala ya technological intelligence ambayo ndio msingi wa mapinduzi ya viwanda kwa taifa la china na kuifanya kuwa giant nation kimaendeleo kwa ujumla.

Kimsingi ujasusi unawaisha maendeleo husika. Sisi huku bado tunakamata nyavu za wavuvi haramu ambao ni raia wa tanzania na kuwaacha wauzaji wa nyavu hizo ambao wwngi wao sio raia wa tanzania wakiendelea kufanya biashara zao.
 
Sisi hatuna cha kudukuliwa, nchi ya wachuuzi hii ndio maana mitaa kama kongo na mingineyo kariakoo imejaa wauza kila kitu kutoka nje!

Ndio maana TCRA wanahangaika na majina bandia na vichupi mitandaoni kwakuwa mitambo yao ina program ya kudeal na hivyo tu sio technology au uchumi wetu.
 
Tanzania tumelala, tukija amka tusha lalwa, tumelaliwa na kukojolewa
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Na hawa wachina walivyojaa hapa bongo bila shaka tunadukuliwa mpk uvunguni
Dunia ya sasa ujajusi wa k8uchumi ndo kipaumbele tofauti na huku kwetu aisee tuna invest kwenye vitu vya hovyo ndo mana Ku progress ni ngumu. Tukiwaona wachina wazagaa hovyo, kumbe wana target mengi.
 
Intelijensia yetu ipo imara sana kwenye maandamano ya vyama vya upinzani, kuwashika wanaotukana viongozi waandamizi wa nchi, na kusimamia chaguzi kuu. Hayo mengine siyo kipaumbele.
Hafu hizo nguvu tungezitumia kwa maendeleo tungefika mbali. Wenzetu wametumia hzo intelligency zimewasaidia kwenye nyanja mbalimbali kwa mstakabali wa nchi zao.
 
Mhimu ni kuongeza wadukuaji huko nchi za nje...Sisi tunadukuliwa kwenye nyaraka za siri ikiwemo mipango ya wapi tunataka kuacha kuomba/kukopa wapi tunataka kutoa tender ya kujichimba gas kifupi ile multi-bilion projects ndo tunadukuliwa. Mfano: Juzi kati hapa tulitaka kununua ndege kutoka Russia, lakini mwisho wa siku tumepindishwa kwenda Canada, kwa nini? Pengine jamaa walitudukuwa na kuanza mashambulizi ya kiukweli.
Ukiona nchi inaingia hadi jeshini kwenu wanaingia hadi kwenye kambi zenu basi ujue bado bado sana!!
 
Back
Top Bottom