Ujambazi Mlimani City, Polisi iko wapi?

Ujambazi Mlimani City, Polisi iko wapi?

jojojo

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2013
Posts
923
Reaction score
399
Kuna matukio mengi sana ya ujambazi MLIMANI City, nini tatizo? Mbona wahusika hawakamatwi? Haya matukio yanajirudia rudia, sijaona juhudi ya askari polisi kufanya ulinzi na kuwakamata wahusika.

Ina maana hakuna jinsi ya kuweka mtego, kwa sababu matukio ni ya mfululizo na siyo wanaenda kuwapora wahusika mbali na eneo hili.
 
Kuna matukio mengi sana ya ujambazi MLIMANI City nini tatizo, mbona wahusika hawakamatwi? Haya matukio yanajirudia rudia sijaona juhudi ya askari polisi kufanya ulinzi na kuwakamata wahusika. Ina maana hakuna jinsi ya kuweka mtego, kwa sababu matukio ni ya mfululizo na siyo wanaenda kuwapora wahusika mbali na eneo hili.
Labda police wanahusika wakiweka mtego watakosa pa kula, siamini police ya tz hata siku moja ikitokea umevamiwa afu ukawapigia wanakuja wanauwa majambazi wanachukua kile majambazi wamekijia iwe bahati wasikuone pia Muombe Mungu akulinde tu.
 
Wamefikia huko kweli? SItaki kuamini...
 
Polisi na jambazi mara nying lao moja.usishangae kuwakuta bar wakinunuliana wisk
 
Mtu asije kwambia akukulipie pesa mlimaniciy ni sehemu hatarishi sana nadhani kuna connection ya watu wa bank wa wale watu wa njee wanakunywa juice glasi siku nzima na masimu makubwa hao ndo watakuwa wanawapa mchongo wa nje kwa maana ndani bodaboda haziingii na magari ni mengi wanajuaje huyu ana pesa nyingi?
 
Wamefikia huko kweli? SItaki kuamini...
Ni hatari mkuu, kuna ni nadra sana jambazi kukamatwa na kukutwa hai wengi wanakuwa wameshauawa na police na mali kutoonekana zilipo.
 
Mkuu nikweli unacho kisema away watu wanakuwa na connection na hawa majambaz Mara nyingi unakuna tukio limeisha nawao ndo wanafika wahy?? Wanakuwa wapi
 
Kuna siku jamaa alitoka kutoa Exima Bank, akaona kuna jamaa wanamfuatilia, alipotoka akaingia Game shopping.. akawaona wamo, ikabidi atoe taarifa kwa walinzi wa Game kwamba kuna watu wanamfuatilia, aliweka pesa zake kwenye kibegi kidogo cha mgongoni, alivyokua anakikabidhi alizitoa bila ya hao jamaa kujua ila akawaonyesha askari wa Game.

Baada ya muda walikuja kutaka kuondoka na hicho kibegi baada ya kushindwa kukifungua kwa sababu kilikua kimefungwa.
Hapo ndio hao jamaa kukamatwa na wale walinzi kilichonishangaza wale walinzi wanasema, tunawajua hawa, hua wanakuja kila siku.
 
Mtu asije kwambia akukulipie pesa mlimaniciy ni sehemu hatarishi sana nadhani kuna connection ya watu wa bank wa wale watu wa njee wanakunywa juice glasi siku nzima na masimu makubwa hao ndo watakuwa wanawapa mchongo wa nje kwa maana ndani bodaboda haziingii na magari ni mengi wanajuaje huyu ana pesa nyingi?
Hapo kweli kabisa , wale majamaa wanaokunywa juice siku nzima na masimu yao makubwa ndio wabaya ,
 
Kuna matukio mengi sana ya ujambazi MLIMANI City nini tatizo, mbona wahusika hawakamatwi? Haya matukio yanajirudia rudia sijaona juhudi ya askari polisi kufanya ulinzi na kuwakamata wahusika. Ina maana hakuna jinsi ya kuweka mtego, kwa sababu matukio ni ya mfululizo na siyo wanaenda kuwapora wahusika mbali na eneo hili.

Tazama Boss wao alivyosema hapa chini

Home

Waziri: Siko tayari kufukuzwa kazi kwa uzembe wa idara, taasisi.
By Gwamaka Alipipi
11th January 2016
email.png

Email
printer.png

Print

Charles-11Jan2015.png

Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga, amesema hayuko tayari kufukuzwa kazi kutokana na uzembe wa idara au taasisi yoyote iliyoko chini yake.

Waziri Ktwanga anafanya ziara katika idara mbalimbali anazoziongoza, aliyasema hayo baada ya kufika Jeshi la Zimamoto na Uokoaji jijini Dar es Salaam na kukutana na viongozi mbalimbali waandamizi wa jeshi hilo.

Alisema hatakubali kuona anawajibishwa na Rais John Magufuli, kwa sababu ya uzembe wa idara yoyote iliyoko chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani, hivyo atawawajibisha watendaji wazembe kabla hajawajibishwa yeye.

Katika ziara hiyo, Waziri Kitwanga alilitaka jeshi hilo kuimarisha ukaguzi katika majengo marefu na mafupi ikiwamo vyombo vya usafiri na usafirishaji.

Alisema Jeshi la Zimamoto linapaswa kusimamia sheria ya uokoaji inayowataka wananchi kupisha magari ya Zimamoto pamoja na gari la wagonjwa pindi yanapokuwa katika dharura.

“Si mnafahamu sheria ya uokoaji inavyosema, hata msafara wa Rais unapaswa kupisha gari za Zimamoto au la wagonjwa linapokuwa katika dharura. Iweje wananchi wasipishe gari la Zimamoto? Nataka msimamie sheria,” alisema Kitwanga.

Aliongeza kuwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linapaswa kuhakikisha kunakuwapo na usalama wa mali na uhai wa wananchi kipindi chote kunapotokea janga la moto pamoja na kwenda na wakati kwa kuwa na vifaa vya kisasa kwa sababu nyakati hizi miji imekuwa inajengwa majengo marefu.

Alisema mtu yeyote anayefanya kosa achukuliwe sheria kali kwa kupigwa faini na kwamba gari la Zimamoto halipaswi kusubiri njiani au kulipisha gari lingine linapokuwa kazini.

Naye Kamishna Jenerali Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mhandisi Pius Nyambacha, alisema jeshi hilo linakabiliwa na uhaba wa vifaa vya kutendea kazi.

Nyambacha alisema thamani ya vifaa vya kuzimia moto vinavyohitajika vinafikia Sh.bilioni moja.

Alisema pia jeshi hilo linakabiliwa na upungufu wa wafanyakazi ambapo kwa sasa lina askari 2,357 malengo makuu yakiwa ni kuwa na askari 4,500.

Vile vile, Nyambacha alisema jeshi hilo lina uhaba wa visima vya kujazia maji na halijapewa fedha za maendeleo kutoka serikalini kwa miaka mitano sasa, jambo linalowakwamisha katika utekelezaji wa malengo waliyojiwekea.

SOURCE: NIPASHE
 
Mfano pale crdb, au Nmb. Unaingia nani unakuta mtu kakaa kwenye bench, hakuna anachofanya zaidi ya kuchezea cm, kumbe anaangali nani anatoka na furushi kubwa, ukizingatia hakuna kificho kwa anaechukuwa hela nyingi.
 
Mtu asije kwambia akukulipie pesa mlimaniciy ni sehemu hatarishi sana nadhani kuna connection ya watu wa bank wa wale watu wa njee wanakunywa juice glasi siku nzima na masimu makubwa hao ndo watakuwa wanawapa mchongo wa nje kwa maana ndani bodaboda haziingii na magari ni mengi wanajuaje huyu ana pesa nyingi?

Nimecheka sana ......'wanakunywa juice glass siku nzima na masimu makubwa' you have made my day
 
Mpaka kesho sina imani na jeshi la polisi.

Haiwezekani kila siku watu wanauliwa wakitoka benki kuchuku pesa na polisi wanakaa kimya.

Ilitakiwa huo mtandao uwekwe wazi kuanzia kwa wafanyakazi wa benki hadi hao majambazi.

Zoezi lianzie benki kwanza.
 
Back
Top Bottom