Uislamu hauna uniform-Mhadhiri

Uislamu hauna uniform-Mhadhiri

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
25,176
Reaction score
48,460
Kwa muda mrefu sana haikumbukiki ilianza lini, ilizoeleka kuwa aina fulani ya nguo au uvaaji kuwa ndiyo alama ya Uislamu.

Kuvaa matarabushi, misuli, barghashia, kanzu, sandali, baibui na Abaya ilihesabiwa kama ndiyo alama za uislamu.

Lakini siku za hivi karibuni wameibuka wahadhiri mbali mbali wanasema kuwa hakuna "sare" ya Uislamu iliyoamrishwa kwenye Quran bali watu wanachanganya kati ya Mila za uvaaji za kiarabu na uislamu.

Hebu msikilize huyu mhadhiri wa kiislamu hapo chini.

Uislam hauna mavazi
Makazi na hijab niavazinya tamaduni za uarabuni
Yaani hainiingii akili kuwa mtu asivae jeans au suti na tai kisa ni muislam
 
Kwa muda mrefu sana haikumbukiki ilianza lini, ilizoeleka kuwa aina fulani ya nguo au uvaaji kuwa ndiyo alama ya Uislamu.

Kuvaa matarabushi, misuli, barghashia, kanzu, sandali, baibui na Abaya ilihesabiwa kama ndiyo alama za uislamu.

Lakini siku za hivi karibuni wameibuka wahadhiri mbali mbali wanasema kuwa hakuna "sare" ya Uislamu iliyoamrishwa kwenye Quran bali watu wanachanganya kati ya Mila za uvaaji za kiarabu na uislamu.

Hebu msikilize huyu mhadhiri wa kiislamu hapo chini.

View attachment 3568789
Malaria 2 unasemaje
 
Ninachowapendea washia wenyewe wanasema Uislamu upo kwenye Quran na siyo kwenye hadithi.

Washia wanasema waislamu waongozwe na Quran na kila muislamu aisome na kuitafsiri Quran bila kuingiza mambo ya Hadithi.
Hujui lolote kuhusu Uislamu wala Ushia.Washia hawasemi waislamu waongozwe kwa Quran tu.Wanaamini hadithi za Mtume Muhammad(SAW).Wanajiita Aluh Bayt watu wa nyumba ya Mtume Muhammad (SAW).
Huwezi kuwa muislamu bila kuamini na kufuata hadithi kwani ndio zinatumika kufafanua Quran kwenye masuala ya ibada kwa mfano Kuswali.
 
bashe kwenye sakata la mgoigoro wa mazao dhidi ya malawi na afrika kusini alizua mjadala mkubwa sana kwa kutoa tamko huku akiwa kavaa kanzu. wabongo tuna changamoto nyingi sana
 
Hujui lolote kuhusu Uislamu wala Ushia...
Ni kweli siwezi kujua mengi kuhusu Uislam lakini akili yangu Ina uwezo wa kutofautisha mantiki mbalimbali.
Huwezi kuwa muislamu bila kuamini na kufuata hadithi kwani ndio zinatumika kufafanua Quran kwenye masuala ya ibada kwa mfano Kuswali.
Wenyewe wanasema hizo Hadithi hazina uhalali.
 
Ni kweli siwezi kujua mengi kuhusu Uislam lakini akili yangu Ina uwezo wa kutofautisha mantiki mbalimbali.

Wenyewe wanasema hizo Hadithi hazina uhalali.
Wenyewe ni kina nani?Hadithi za Mtume kwa Waislamu ni wahyi.Hivyo hakuna muislamu muumin anayeweza kusema hazina uhalali.Akisema haziamini basi huyo sio muislamu.
 
Kwa muda mrefu sana haikumbukiki ilianza lini, ilizoeleka kuwa aina fulani ya nguo au uvaaji kuwa ndiyo alama ya Uislamu.

Kuvaa matarabushi, misuli, barghashia, kanzu, sandali, baibui na Abaya ilihesabiwa kama ndiyo alama za uislamu.

Lakini siku za hivi karibuni wameibuka wahadhiri mbali mbali wanasema kuwa hakuna "sare" ya Uislamu iliyoamrishwa kwenye Quran bali watu wanachanganya kati ya Mila za uvaaji za kiarabu na uislamu.

Hebu msikilize huyu mhadhiri wa kiislamu hapo chini.

View attachment 3568789
Ni kweli kabisa...
Kinachotakiwa ni kujisitiri
Kuna baadhi ya vitu watu wanachanganya na mila za Kiarabu...wakifikiri ndio Uislam
Mungu mwenyewe alisema ametuletea dini rahisi....ili watu waweze kuishi nayo.
 
Hawa washia ndio hao hao wairan? Maana iran ni washia na wasaudi ni wasuni. Ndio kusema BAKWATA ni wasuni? kwa hiyo ndugu zao wa imani ni wasaudia. na hawa mabohara, ismalia, aga khan, wahabi ni waislam wa aina gani?
 
Dini ni utamaduni tu kama zilivyotabia zingine. Hakuna usupesho wowote kiasi cha kutaka iwe universal na haiwezekani.
 
Aisee! Hapa si tunawazungumzia washia. Sasa hili swali linakujajje tena?

Hii ya kusema Hadithi ni wahyi wewe umeitoa wapi tena.. unataka kusema Hadithi nazo ziliteremshwa kama ilivyoteremshwa Quran?
Ndio sababu nilikuambia hujui chochote kuhusu Uislamu.Fanya utafiti kwanza ujue Wahyi ni ujumbe wa aina gani?Baada ya hapo ndio utaweza kuzungumzia Uislamu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom