Uingereza yapatia Tanzania Sh230 bilioni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uingereza yapatia Tanzania Sh230 bilioni

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MziziMkavu, Sep 19, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 19, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  WAKATI baadhi ya wahisani wakiwa wametangaza kupunguza fedha za kusaidia bajeti ya serikali, Uingereza imetangaza kutoa Sh230 bilioni kwa ajili hiyo katika kipindi cha mwaka 2010/11.

  Hayo yameelezwa na Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Uingereza Stephen O’brien katika taarifa yake iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana.

  Kwa mujibu wa taarifa hiyo, awali waziri huyo alikuwa na mazungumzo ya kina na Waziri wa Fedha na Uchumi Mustafa Mkulo, kuhusu matumizi ya fedha hizo zilizo tolewa na nchi hiyo.

  “Kufuati mazungumzo yangu na Waziri Mkulo, ninayo furaha kutangaza kuwa Kitengo cha Maendeleo cha Kimataifa (DFID) kitaisaidia bajeti ya serikali ya mwaka 2010/11 kwa paundi 103.5 sawa na Sh230 bilioni, fedha hizi zitasaidia kuendeleza vipaumbe vya serikali vilivyoainishwa kwenye Mkukuta,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

  Katika taarifa hiyo, Uingereza iliimiza matumizi mazuri ya fedha hizo huku ikisisitiza kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa ili kufanikisha lengo la kupambana na umasikini.

  Ilisema serikali ya mseto ya Uingerea, imepanga kuongeza misaada yake hadi kufikia asilimia 0.7 ya pato lake la ifikapo mwaka 2013 na kuwa hadi sasa Tanzania ipo katika nafasi ya tatu kwa nchi zinazosaidiwa kwa kiasi kikubwa na nchi hiyo.

  “Tutaendelea kushirikia kwa karibu na Tanzania ili kuhakikisha kuwa tunapambana na umasikini,” ilisema na kuongeza:“Hata hivyo serikali ya Uingereza ipo katika kipindi kigumu cha kuangalia upungufu uliopo katika bajeti yake, kwa hiyo tunatarajia kuwa fedha hizi zitatumika vizuri na kuleta matunda yaliyokusudiwa,” ilieleza.
  Alisema atahitaji muda kuzungumza na Waziri wa Fedha, ili kuona namna ya ufanyaji kazi wa fedha wanazotoa ili kupata matokeo mazuri .
  Kwa mujibu wa taarifa hiyo, fedha zilizotolewa na nchi hiyo katika mwaka wa fedha uliopita zilisaidia watoto 200,000 kwenda shule.
  Pia zilisaidia watoto 30,000 kwenda shule za sekondari katika mwaka 2009, huku watu 50,000 wakipata huduma za maji safi .
  Ilieleza pia kuwa, fedha hizo ziliwawezesha kutolewa kwa vyandarua vyenyedawa 54 na kuwa pia ziliwezesha kupatikana kwa tani 4,000 za mbolea pamoja na tani 200 za mbegu bora.


  Katika hatua nyingine, taarifa hiyo ilieleza kuwa waziri huyo alipata fursa ya kuonana na Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume na kuzungumza mambo mbalimbali ikiwemo mafanikio ya kumaliza mkogoro wa CCM na CUF Visiwani humo.
  Kwa mujibu wa Taarifa hiyo, waziri huyo alimpongez Rais Karume pamoja na Katibu Mku wa CUF Seif Sharif Hamadi kwa kuweza kufnikisha hjambop hilo.

  Aliwataka kuhakikisha uchaguzi wa mwaka huu unafanyika kwa uwazi na amani na kuwa nchi mbalimbali duniani zinafuatilia mambo yanavyo enda visiwani humo.

  Chanzo : Uingereza yapatia Tanzania Sh230 bilioni
   
 2. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #2
  Sep 21, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  waingereza ndo siku zote huwa wanatoa kitu cha kueleweka. hao wengine wanakuwaga na maneno matupu. tunashukuru kwa hilo
   
Loading...